'Magari ya Makonda' yakwama kukarabatiwa, mwenyewe agoma kutoa ushirikiano

Unataka kutuambia kuna mgogoro wa kiutendaji kati ya CCM na serikali yake?

Kwani ni mara ya kwanza magari ya serikali kutumika kwenye shughuli za chama chenu?

Kama sio mara ya kwanza, kwanini Makonda apate kigugumizi kuwajibu hao wanaomuuliza hayo maswali?

Hayo magari yameachwa hapo TEMESA kwa sababu maalum, wanatafuta gap waje kutupiga mbele ya safari, wao watachota pesa za umma wakanunue magari mengine mapya muda wao ukifika.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Hapo mpaka sasa hivi kuna vigogo wamesha chagua V8 zao tayari. Nchi hii ngumu sana.
 
Mleta mada muongo chama hakiwezi jieleza kwa sababu ya magari ya serikali wale waliongozana kwenda kwenye
mkutano kusikiliza kero za wananchi na kuzipa majibu

Kiongozi wa serikali kusikiliza.kero za wananchi ni moja ya majukumu yake
Kuna mifumo ya kusikiliza kero serikalini.... Sidhani kuambatana na kiongozi wa siasa ni sahihi
 
Upo
Na hapo ndio utajua uongo wa mtoa mada yani anajaribu kutuambia kuwa magari hayo yalikwenda kwenye msafara wa Makonda bila ruhusa? Huu ndio uongo mkubwa! Yani CCM na serikali walumbane kukarabati magari?
Yani hapa ni sawa kutuambia CCM na CCM wana lumbana!

Kiufupi huu ni uongo kwani CCM ni wale wale na tamesa hawana uwezo wa kupingana na CCM maana wanalipwa na CCM…
Mtoa mada huwa hampendi Makonda sema sasa ndio yupo pale na sasa ana jifariji……
Sahihi kabisa. Mtoa mada ni CHAWA wa Chongolo
 
Nadhani mleta mada ni mbumbumbu wa mambo mengi sana, Ajali aliyepata ni dereva unadanganya watu eti maelezo yanatakiwa kutolewa na mkuu wa msafara, Huu ni ulongo wa hali ya juu. Hivi ni nani anayejua chanzo cha ajali zaidi ya dereva aliyepatwa na ajali husika?

Ulongo mwingine ni kuhusu kukwama kwa matengenezo ya gari etuli kwa sababu idara za Serikali zinahoji kwanini magari husika yalikuwa kwenye ziara ya Makonda!!

Ifahamike kuwa ziara ya kiongozi yeyote wa CCM ni ziara ya kukagua utendaji wa Chama na Serikali, kwa upande wa Serikali wanaokaguliwa ni Watumishi wa Serikali wanaotekeleza Ilani ya Chama kilichoko madarakani, sasa kwa akili yako ulitarajia kwenye msafara wasiwepo wanaokaguliwa? Hapa huna hoja zaidi ya chuki binafsi kwa Makonda. Bahati mbaya sana unakuja kuposti utumbo kwenye ukrasa wa Jamiiforum sehemu ambayo tunaamini wamejaa intellectuals jitahidi ukumbi huu uwe unauposti Facebook, TikTok au Instagram kule.
Mleta mada ni tapeli anayeutumia ujuzi wake wa uandishi ili kuwapotosha wenye akili ndogo!!

Anataka kutuambia siku gari la RAIS likipata ajali basi Samia ndo akatoe maelezo?

Bottom line ni kwamba mtoa mada ana chuki iliyopitiliza kwa Makonda!! Na hoja ni ndogo tu, Makonda anawabana wezi wanaomlisha huyu Mzee asiyetaka kufanya kazi.
 
Umesema Kweli, mtoa HOJA ana Chuki na kijana,

Lakini pia UKWELI usemwe, kijana Hana Uadilifu wowote.
 
Mleta mada ni tapeli anayeutumia ujuzi wake wa uandishi ili kuwapotosha wenye akili ndogo!!

Anataka kutuambia siku gari la RAIS likipata ajali basi Samia ndo akatoe maelezo?

Bottom line ni kwamba mtoa mada ana chuki iliyopitiliza kwa Makonda!! Na hoja ni ndogo tu, Makonda anawabana wezi wanaomlisha huyu Mzee asiyetaka kufanya kazi.
Kumfananisha mwenezi wa chama na Rais ni ujinga wa hali ya juu sana
 
Mimi bado najiuliza ile ilikuwa ni ajali ya kawaida au ya Kisangoma ??!

Gari 6 zigongane kwa mpigo ?!!!
Duh 🙄 !
Madereva walikuwa wamefumba macho ?? Au gari zilikuwa na Breki hafifu ??
Naona na ile amsha amsha imeishia pale !
Ngoja Tusubiri tuone 🙏🙏
 
Hakuna wakuwahoji na hakuna wa kugoma kutengeneza magari hayo…yani wewe unafikiri kuna taasisi yenye uwezo wa kuigomea CCM?
Hakuna wa kuigomea CCM ila wanaweza kuwepo wa kumgomea aliyekuwa akiyatumia maana alikuwa akiwazingua wengi huko Chamani !!
Lakini ngoja Tusubiri tuone 🙏🙏 !
 
Back
Top Bottom