VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Unakaribia mwezi mmoja sasa tangu msafara Ndugu Paul Makonda, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, upate ajali kule Sululu, Masasi mkoani Mtwara. Ajali hiyo iliyohusisha magari yapatayo 10, ilitokea tarehe 11 mwezi uliopita na kusababisha uharibifu wa magari kadhaa yakiwamo ya serikali.
Katika kile kinachosemwa kama kiburi na jeuri ya kimadaraka chamani, Makonda amegoma kutoa ushirikiano kufanikisha marekebisho ya magari hayo yaliyohifadhiwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA). Ushikirikiano utakiwao ni ripoti ya mkuu wa msafara juu ya ajali hiyo ambayo hadi sasa haijatolewa.
Makonda amewaambia maafisa wa kichama na kiserikali kuwa wakitaka kujua lolote wakakiulize chama kwakuwa ndicho kilichoruhusu na kuwezesha ziara yake mikoani-ikiwemo hiyo ailiyokuwa akitokea mkoani Ruvuma. Mkwamo wa matengenezo hasa unazikumba gari za serikali ambazo huhitaji ripoti kamilifu ili ziweze kutengenezwa.
Idara ambazo zinamiliki magari hayo ya serikali zilizopata ajali hiyo zinawataka maafisa wake na madereva wao waseme kwanini walikuwepo kwenye msafara huo wa kichama; hoja ambayo inapaswa kujibiwa na Makonda aliyegoma kufanya hivyo. Ripoti haijatolewa na magari hayajashughulikiwa.
Makonda, chama ni nani ili akaulizwe hata ajali yako ya Masasi?
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Sombetini, Arusha)