Maendeleo ya Mgomo wa Madaktari na Mwitikio wa Serikali

viongozi wa wizara ya afya wangekubali kukutana na ma Dr. na kuwasikiliza hoja zao kisha kuwatolea majibu, yale yanayowezekana yakubalike na yale ambayo kwa sasa hayatekelezeki apewe muda zaidi, ma Dr. ni binadamu nao wanaelewa wanapoelimishwa vizuri kuliko kuwakimbia, mwisho wa siku sisi walala hoi ndiyo tutakuwa victim
 
Wakigoma seriously wataifundisha adabu serikali. Tumekuw tukiwaambia muda mrefu kuwa mgomo ndiyo njia mbadala ya kupata suluhisho la matatizo yap lakini kama kawaida ya wabongo UWOGA umewagubika.
 
kweli ziumiazo ni nyasi, wenyewe wanakwenda kuangalia afya tu London, matibabu india

Kiburi cha wao kuangalia afya London wakati sisi tunaishi kwa kudra za Mwenyezi tunawapa sisi. Tungejua kuwa hata sisi tuna uwezo wa kuwanyima hicho kiburi cha wao kwenda India basi ni suala la kuacha kufikiria kitumwa, kwamba wao wanapaswa kututumikia sisi. Madaktari sasa wanaonyesha ni njia gani itumike kuifanya serikali iwatumikie wananchi.
 
Yaani hawa madaktari nawafagilia kwa msimamo wao. Ila wakilegeza huo msimamo wao huo watakuwa ndio the last cadre kujidhalilisha beyond imaginable boundaries. Msiwe kama walimu ambao kila uchao hawajui destiny yao,onyesheni kuwa mnamaanisha mnachokiongea na kukidai.
 
Labda niwatoe khofu. Wanapogoma madaktari huwa wanabakia skeleto staff kuangalia emergencies sio kama madaktari wana roho mbaya lakin kudai haki ni sawa. I am still with my fellow doctors until the end. Madaktari wamedharauliwa sana hasa tokea wakati wa mkapa. Sio kama serkali hawawezi kumaliza adha za madaktari ni sababu ya khiyana zao tu.
 
Acheni roho mbaya kuufagilia mgomo ni kuwakomoa wananchi ambao kodi zao zimewasomesha madaktari. Siku zote muafaka unapatikana kwa njia ya meza ya majadiliano
 
tatizo watu hajui historia, madaktri na waalimu yaleyale wala usiwasifie, kuna wakati walifukuzwa wakaanza kuililia serikali oh tunaomba tuonewe huruma maisha magumu, ngoja tuone ngoma ya kitoto kama itadumu
 
Acheni roho mbaya kuufagilia mgomo ni kuwakomoa wananchi ambao kodi zao zimewasomesha madaktari. Siku zote muafaka unapatikana kwa njia ya meza ya majadiliano

siipend hyo kauli ETI KODI ZAO ZIMEWASOMESHA!
KUNA WALE WANAOJSOMESHA,KUNA WALE WANAOKOPESHWA,INAKUWAJE?
 
Huyu Blandina Nyoni sijui yukoje, na pengine najiuliza kwa nini wanawake wakishika madaraka ya juu huwa na kiburi sana?

huyo mama i wish atokee kwenye anga zangu,imagne nmeajiriwa tokea mwezi wa saba mwaka jana mpaka leo cjaiingia kwenye payrol ananiboa kweli!
 
Acheni roho mbaya kuufagilia mgomo ni kuwakomoa wananchi ambao kodi zao zimewasomesha madaktari. Siku zote muafaka unapatikana kwa njia ya meza ya majadiliano

Kusomesha wananchi ni wajibu wa serikali yoyote kwa hiyo serikali haiwezi kukwepa kuwalipa watumishi wake eti kisa iliwasomesha. Kama imeshindwa ijiuzuru wengine waendeshe na walipe watumishi vyema.
 
Hata kama haupendi, somo la uzalendo litabidi lifundishwe kwa madaktari na watu kama wewe

Mkuu we ni mzalendo sio?
Uzalendo upi unaouzungumzia kwamba hata kama haki yako inabanwa uendelee kuwa mzalendo! La hasha huo utakuwa ni UJUHA..
 
Wao wapeleke watoto wao kusoma majuu, wa madktari ndo
waende shule za msondo ngoma! kama serikali inamwaga
mboga acha madaktari wamwage ugali tena wasiumwage tu
wautie na mafuta ya taa kabisa wasije wakauokota wakaula bure.
 
Acheni roho mbaya kuufagilia mgomo ni kuwakomoa wananchi ambao kodi zao zimewasomesha madaktari. Siku zote muafaka unapatikana kwa njia ya meza ya majadiliano

Hakuna mtu anayeufagilia mgomo huu,watu wanashangaa jinsi serikali sikivu inavyotatua matatizo,kuhusu kodi kama tuna uchungu
nazo tungeanza kupambana na ufisadi,kumbuka wapo wanaojisomesha na wengine wanakopeshwa hao unawaweka kundi gani??wanaowakomoa wananchi ni serikali,umesema vema kuwa muafaka ni meza ya majadiliano kumbuka kuwa mawaziri husika wanakimbia hayo mazungumzo hapo unategemea nini??serikali ikikosea ni bora ikubali kukosolewa,wao si miungu kuwa mara zote wapo sahihi.
 
CCM imefikia ukomo wa kufikiri....... hata PCCB eti wanashindwa kugundua forgery kwenye majina ya wadakopeshwaji hewa HESLB????
 
Acheni roho mbaya kuufagilia mgomo ni kuwakomoa wananchi ambao kodi zao zimewasomesha madaktari. Siku zote muafaka unapatikana kwa njia ya meza ya majadiliano
Ni kweli, nadhani hawa jamaa wangetafuta namna nyingine ya kuikomoa serikali maana njia hii itatuathiri sisiw ananchiw a kawaida. Hao vigogo serikalini wala hawatapata athari za moja kwa moja za mgomo huu, lakini leo hii kuna watu watakaokuwa wanalilia ndugu zao waliofariki kutokana na mgomo
 
Nasikia selikali imekataa kujibu hoja.Wamegoma hata kusikiliza chanzo cha matatizo sasa wafanyeje?kama ni kodi na wao wanalipa kodi kama wafanyakazi wengine.Ni vyema serikali isikilize madai yao kama inasema siyo ya msingi ijulikane badala ya kuwatusi kupitia vyombo vya habari
 
Back
Top Bottom