Maendeleo ya Mgomo wa Madaktari na Mwitikio wa Serikali

Mkuu we ni mzalendo sio?
Uzalendo upi unaouzungumzia kwamba hata kama haki yako inabanwa uendelee kuwa mzalendo! La hasha huo utakuwa ni UJUHA..

mafilili si kwamba ni mzalendo ni mmoja kati ya wale wanaudhurumu wafanyakazi nchi hii,naomba atambue kuwa uzalendo si kwa raia tu bali hata serikali inatakiwa kuwa na uzalendo kwa raia wake,kauli hizi ni za kukwepa kuwajibika kwa wananchi,posho ya elfu 10 kwa miaka 7 mbona hapo uoni kama madaktari wamekuwa wazalendo sana?tusiwe wavivu wa kufikiri kwa kuangalia tulipoangukia badala ya kuangalia kulipojikwaa!!!
 
Labda niwatoe khofu. Wanapogoma madaktari huwa wanabakia skeleto staff kuangalia emergencies sio kama madaktari wana roho mbaya lakin kudai haki ni sawa. I am still with my fellow doctors until the end. Madaktari wamedharauliwa sana hasa tokea wakati wa mkapa. Sio kama serkali hawawezi kumaliza adha za madaktari ni sababu ya khiyana zao tu.

My friends....one think I would like to know from you guys!!!!! This time are you serious????? I doubt......unless some of your members are from Kenya!!!!! ha ha ha ha ha ha am joking but Fellows this Time be serious.....sure...haya bana don`t allow them to manipulate you guys.........haya bana lakini kuwa ngangari eeeh
 
Hivi hili la kutaka wizara and viongozi wake wabadilishwe pengine sio strategy nzuri sana maana kwa namna fulani inakuwa rahisi sana kwa serikali kukwepa na kusema ni madai ya kisiasa/au the whole issue ina harufu ya "siasa"! au pengine ni long term sio kitu wanachoweza kupewa fumba na kufumbua.

Wangeanza zaidi na suala la maslahi yao (ingawa najua kuna mwingiliano na viongozi na structure ya wizara) kama mishahara, posho na mazingira ya kazi halafu hilo la wizara likaja baadae.

Well, ngoja tuangalie usikivu au ubabe wa serikali sasa!
Ni kweli mkuu ki mkakati hii wamekosea kwa kuwa katika majadiliano kuna kitu wanaita "give and take" suppose serikali inaanza na hili la structure ya wizara bila kuzingatia mambo muhimu yanayogusa maslahi si itabidi mgomo upige pause kwa kuwa itaonekana kwamba serikali "imeshaanza kushughulikia" ki mtaji wa hoja hii haijakaa sawa.

Na kikweli mkulu akiamua kutumia kama kichaka watakuwa wame buy time unnecessary.
 
gazeti la chama leo limesema mhimbili mambo shwari sasa mgomo huo unatoka wapi?:wacko:
 
naunga mkono huo mgomo . madaktari kazeni buti hakuna kurudi nyuma kama walimu. serikari ilidhani nyie nao ni walimu hambao huwa wanaigiza mgomo huku hawawezi zaidi ya kupiga kelele bila vitendo . kazeni buti
 
Hospitali za Amana, Mwananyamala na Temeke pamoja na Muhimbili huduma zinatolewa kama kawaida
 
Mgomo wa wagonjwa kuanza siku ya alhamisi wataanza wagonjwa walioko Muhimbili kuelekea wizarani, temeke kuelekea wizarani, mwananyamala kuelekea wizarani, ocean road kuelkea wizarani na manesi na msalaba mwekundu mnaombwa kuwasindikiza, FFU ulinzi wenu ni muhimu
 
Hakuna mgomo wowote. Wafanyakazi wa sekta ya afya wote wanamuogopa JK, wakikumbukia ule mkwala aliowapiga kina Mgaya walipoorganize mgomo wa wafanyakazi wote nchi nzima. Nenda tu katibiwe, lakini kuwa makini huenda wapo kwenye mgomo baridi.
 
Bado siamini kama masrahi ya madaktari wanayolipwa sasa hayatoshi,mimi naamni madaktari mmesahau kuwa kazi yenu siyo kazi pekee hapa tanzania na kwamba hakuna serikali ambayo itawabagua watumishi wake.

Mmekiri wenyewe kwamba mwaka 2005 mlikuwa mnaloipwa 124,000 leo mnalipwa 700,000 kwanza nampongeza jk na nawataka mfahamu kuwa kuomba nyongeza kwa kujilinganisha na wanasiasa ni ujinga, kama mnataka posho za siasa nendeni mkagombee, dunia nzima posho za wanasiasa ziko juu na watumishi wanalipwa kwa scales zao kulingana na policy.
 
Ni kweli Nchii hii mambo hayaendi bila ya migomo. Hali hii ikiendelea tutashuhudia migomo mingine mingi ya ajabu pia. Jamani watanzania kila mtu kwa nafasi yake atimize wajibu wake.Tusingoje migomo ili tutekeleze wajibu wetu. Hilli halihitaji utaalamu wa ziada kutoka nje.


Mungu tubariki watoto wa Tanzania
 
hawa watakuwa wafuasi wa CDM tu, tangu uhuru migomo kama hii haikuwapo kabisa leo hii nani anawafundisha kugoma tena kwa jeuri ili hali wanajua kuna sekta haziruhusiwi kugoma kabisa ikiwemo na hii ya afya. (mhhh..)
 
CDM bwana ni wachochea vurugu nchini,
1. Walianza kutoka bungeni wakati rais akiwepo
2. Maandamano Arusha
3. Kususia vikao vya bunge juu ya mswada wa katiba
4. Kuwaunga mkono TUCTA na Mgaya
5. Kuwaunga mkono CWT na Mkoba
6. Kuunga wa interns Muhimbili,
7. Leo wapo na madaktari

Itapobidi tutaitisha maandamano nchi nzima kuwalaini CDM na MAT kwa kukosesha huduma ya afya wananchi wa TZ
 
Kwani serikali haiwezi kwenda mahakamani kuomba hati ya dharura kusimamisha mgomo kama kipindi kile ilivyofanya kwa walimu? Serikali legelege...
 
Hakuna mgomaji hapo,tishia nyau tu.
Mbona nimepita rufaa mbeya na nimepewa huduma au mgomo ni
kwa baadhi ya siku tu?
 
Back
Top Bottom