Hakuna mbunge yeyote anayeleta maendeleo, maendeleo huletwa na Serikali

BrownRange

JF-Expert Member
Dec 25, 2020
927
1,190
Kwa mfumo wa nchi za kiafrika, hakuna mbunge anayeleta maendeleo, Kama Serikali haina kipaumbele na eneo husika, hata mbunge ufanyeje, huwezi kupata hayo maendeleo

Naomba kuwasilisha
 
Kwa mfumo wa nchi za kiafrika, hakuna mbunge anayeleta maendeleo, Kama Serikali haina kipaumbele na eneo husika, hata mbunge ufanyeje, huwezi kupata hayo maendeleo

Naomba kuwasilisha
Huo ndio ukweli, Kuna wanasiasa wachovu wanahadaa wananchi kuwa maendeleo yanaletwa na mbunge. Kibaya zaidi hata wasomi huwa wanaamini huo utapeli wa kijinga.
 
Kazi za msingi za mbunge zinajulikana:
1. Kuwakilisha wananchi bungeni
2. Kutunga sheria
3. Kusimamia serikali

Ujenzi wa miundombinu ni jukumu la serikali. Hata hivyo mbunge mzuri anaweza kufanya lobbying kwa serikali ili itoe kipaumbele cha maendeleo kwenye jimbo lake.

Wananchi wengi ni mbumbumbu wakiona maendeleo wanasema kaleta mbunge. Pia bungeni nimewahi kumsikia spika Job anahoji tangu Tundu Lissu na Lema wamechaguliwa wamefanya nini cha maana kwenye majimbo yao.

Huu ni ujinga wa mtu mweusi. Ndungai alijua wazi serikali ya CCM haiwezi kupeleka maendeleo kwa wakati kwenye majimbo yenye wapinzani.
 
Kazi ya Mbunge/Bunge ni kuisimamia serikali. Lakini pia anawajibu wa kusaidia wananchi wake kufikisha kero zao kwa serikali.

Hawaleti fedha za maendeleo ila inatakiwa wawe na mchango katika dira ya maendeleo.

Ni kwa vile nchini kwetu bunge ni toothless

Sent from my CPH1819 using JamiiForums mobile app
 
Kama wabunge hawaleti maendeleo wa kazi gani sasa??
 
Kuna hili la kuwashukuru viongozi kama wao ni miungu.mfano kiongozi flani anasema kwa wananchi mshukuruni sana rais kwa kuwaletea maji au barabara.
Wakati hivyo vyote ni sehemu ya wajibu wake.
 
Kazi za msingi za mbunge zinajulikana:
1. Kuwakilisha wananchi bungeni
2. Kutunga sheria
3. Kusimamia serikali

Ujenzi wa miundombinu ni jukumu la serikali. Hata hivyo mbunge mzuri anaweza kufanya lobbying kwa serikali ili itoe kipaumbele cha maendeleo kwenye jimbo lake.

Wananchi wengi ni mbumbumbu wakiona maendeleo wanasema kaleta mbunge. Pia bungeni nimewahi kumsikia spika Job anahoji tangu Tundu Lissu na Lema wamechaguliwa wamefanya nini cha maana kwenye majimbo yao.

Huu ni ujinga wa mtu mweusi. Ndungai alijua wazi serikali ya CCM haiwezi kupeleka maendeleo kwa wakati kwenye majimbo yenye wapinzani.
Hapo kwenye kusimamia serikali ndio pasua kichwa!, Unamsimamia anayekulipa mshahara! :oops:
 
Kama wabunge hawaleti maendeleo wa kazi gani sasa??
Mbunge ni muwakilishi wa mahitaji ya wananchi walioko jimboni kwake huko bungeni ili serekali ifanyie kazi mahitaji hayo. Pia ana wajibu wa kuisimamia serekali na kuishauri ndani ya bunge. Na kazi nyingine ni kutunga Sheria ndani ya bunge, japo kwa bunge letu, hii ipo kinadharia zaidi.
 
Wabunge ndio wanaopanga bajeti, kama wanaona bajeti haina maslahi au haileti maendeleo katika majimbo yao husika wanapaswa waikatae.
 
Wabunge ndio wanaopanga bajeti, kama wanaona bajeti haina maslahi au haileti maendeleo katika majimbo yao husika wanapaswa waikatae.
Bajeti inapangwa na serekali mkuu, huko bungeni inaenda kupata uhalali tu. Lakini kwa bunge hili linalopatikana kwa hisani ya serekali, usitegemee wakatae kinachotakiwa na serekali.
 
Kwa mfumo wa nchi za kiafrika, hakuna mbunge anayeleta maendeleo, Kama Serikali haina kipaumbele na eneo husika, hata mbunge ufanyeje, huwezi kupata hayo maendeleo

Naomba kuwasilisha
Kule Morogoro Abood huwa anatoa bus kwa ajili ya msiha, nazani ndio maendeleo yenyewe
 
Kwa mfumo wa nchi za kiafrika, hakuna mbunge anayeleta maendeleo, Kama Serikali haina kipaumbele na eneo husika, hata mbunge ufanyeje, huwezi kupata hayo maendeleo

Naomba kuwasilisha
Siyo kweli!
Mbunge anapaswa kuwa na Dira ya Maendeleo ya watu wake kwa kuweka vipaumbele vya Jimbo lake vizuri!

Siyo kila kitu kinafanywa na Serikali!

Watu wakijiongoza vizuri na kuweka malengo ya pamoja kama watu wenye nia ya kwenda kwenye hatua fulani walioichagua basi Wanajimbo wanaweza kufaulu kusogea mbele kimaendeleo.

Chukulia Mfano tu wa Jimbo ambalo Maendeleo yake huletwa na Kilimo.

Halafu Mbunge wao hana Shamba na akiwa nalo basi liko hoi...huyo hafai kuwa Muwakilishi wa watu wake kwa Sababu alipaswa kuwa na Shamba la Mfano kwa ajili ya kunyanyua wananchi wenzake.

Mbunge ana influence sana kwenye Jimbo lake hata kama Serikali haina pesa!

Hata kwa tabia ya Usafi wa Mazingira tu; hilo halihitaji Pesa ya Serikali lakini linahitaji kuwa na Kiongozi mwenye Dira...!
 
Kwa mfumo wa nchi za kiafrika, hakuna mbunge anayeleta maendeleo, Kama Serikali haina kipaumbele na eneo husika, hata mbunge ufanyeje, huwezi kupata hayo maendeleo

Naomba kuwasilisha
Tuliyaona Haya Kwenye Utawala Wa Jiwe
Songwe Waliambiwa Msipomchagua Silinde Basi Mjue Hata Maji Siyaleti Nimechoka Kuwabembeleza Mimi

Yaani Mchague Upinzani Utegemee CCM Ilete Maendeleo
 
Siyo kweli!
Mbunge anapaswa kuwa na Dira ya Maendeleo ya watu wake kwa kuweka vipaumbele vya Jimbo lake vizuri!

Siyo kila kitu kinafanywa na Serikali!

Watu wakijiongoza vizuri na kuweka malengo ya pamoja kama watu wenye nia ya kwenda kwenye hatua fulani walioichagua basi Wanajimbo wanaweza kufaulu kusogea mbele kimaendeleo.

Chukulia Mfano tu wa Jimbo ambalo Maendeleo yake huletwa na Kilimo.

Halafu Mbunge wao hana Shamba na akiwa nalo basi liko hoi...huyo hafai kuwa Muwakilishi wa watu wake kwa Sababu alipaswa kuwa na Shamba la Mfano kwa ajili ya kunyanyua wananchi wenzake.

Mbunge ana influence sana kwenye Jimbo lake hata kama Serikali haina pesa!

Hata kwa tabia ya Usafi wa Mazingira tu; hilo halihitaji Pesa ya Serikali lakini linahitaji kuwa na Kiongozi mwenye Dira...!

Hii siyo kazi ya mbunge … Wewe unataka kulazimisha ila mbunge kazi yake siyo kuleta maendeleo .

Ulichoandika hapa ni sawa na useme kila mwananchi ana wajibu wa kuleta maendeleo. Kama eneo lina mashamba na mbunge lazima awe na shamba ? Hilo hilo eneo likiwa na biashara ya petrol station maana yake mbunge pia awe na station ? Kama kuna ufugaji pia mbunge afuge? Atafanya vingapi maana majimbo ni makubwa na yana kazi mbali mbali

Kuhusu usafi tayari serikali ina mabwana afya wapo kila mahali kifupi serikali ina kila mtu katika kila eneo na kila sekta na serikali ina information nyingi za kila eneo kitu ambacho mbunge hana.
 
Mada nzuri kwa upande wangu, nimebahatika kutembelea wilaya ya Lushoto kwa mara ya kwanza, Mwenyezi Mungu kawapa kila kitu isipokua greedy, corrupted leaders, wilaya ina wabunge 3 wameshindwa kabisa kukarabati ile pass kutoka Mombo hadi mlalo, yaani mpaka Germany aje tena kuikarabati ile pass, wao wamewekeza miradi mingi na kupiga usd huku wakiwalipa wale poor of the poorest vicenti, maisha ya wengi ni way below poverty line, yaani wamekata tamaa wakati wamezungukwa na utajiri mkubwa mno, elewa kila watalii 12 wana creat nafasi moja ya ajira,sasa wakifanikiwa kupata watalii 300,000 kwa season, ni kiasi gani cha ajira kitakua created, nilitamani niwapige viboko wabunge wa wilaya hii
 
Dunia nzima kazi ya Bunge sio kuleta Maendeleo,labda unataka iwe tofauti kwa Tanzania
Sio dunia nzima, labda Africa, nchi za kifalme na kidikteta.
Bunge ndilo linalopanga bajeti ya nchi na kuisimamia serikali. Kwenye demokrasia imara kama ya Marekani ambapo unakuta vyama vinatofautina kwa idadi ndogo ya wabunge, wabunge wanakwamisha bajeti ya serikali kama haina maslahi kwa wapiga kura wa majimbo yao. Wabunge wanaweza kuwamisha teuzi za serikali na mipango yake kama baadhi ya mahitaji yao hayazingatiwi.
 
Back
Top Bottom