Waziri Mkuu Majaliwa tunakuomba uende ukamalize mgomo wa daladala Arusha

Deleted01

JF-Expert Member
Sep 28, 2018
1,411
3,458
Hii nchi bado ina rule of law ila watu wachache ambao wana maslahi binafsi wanashindwa kufata na kusimamia sheria kwa personal benefits zao.

Tunaomba Waziri Mkuu Majaliwa, mtumishi wa watu uende Arusha ukamalize mgomo ulioanza tarehe 14/8 na ambao utaendelea bila kikomo hadi madereva wa daladala wasikilizwe na kutatuliwa kero zao, kitu ambacho serikali ya mkoa imeshindwa hadi hivi sasa.

Inaumiza sana kuona Mgomo wa soko la kariakoo ulitatuliwa kwa haraka sana ila kadha ya mgomo wa daladala Arusha inaachwa bila utatuzi na mbunge Gambo yupo, mkuu wa mkoa yupo, mkuu wa wilaya yupo na wananchi bado hawaskilizwi, hizi double standards ni mpaka lini..?

Tunaomba tu ufike Mh. Majaliwa, pengine sasa labda mkoa umewashinda viongozi wake.

Pia soma: Arusha: Daladala zagoma tena Arusha, leo Agosti 14, 2023
 
Waambie ccm waache kuteua watoto kuongoza na wasifanye nafasi za uteuzi kama njia ya kutunuku watu kujipatia kipato..tatizo hili ni dogo ambalo hata mkuu wa mkoa hastahili kushughulikia, ni la ngazi ya wilaya..
Kuna haja gani ya kuwa na DC km vitu vidogo km hivi hawezi kushughulikia, kwa nini unamtoa mtu wa LATRA unamuacha DC? Rais wa awamu ya 5 alijua kudeal viongozi walioshindwa kusimama kwenye nafasi zao..
Chagueni watu wenye sifa kuongoza, sifa kuu kwa mazingira ya sasa ni ukomavu kifikra na uwezo wa kutenda pasina kuumiza watu..
Kwa hiyo migomo km hii ikitokea wilaya zaidi ya 5 waziri mkuu atakwenda wapi aache wapi?
 
Back
Top Bottom