Boramaisha
JF-Expert Member
- Apr 29, 2009
- 820
- 18
Mkuu,
Nashukuru kwa hii habari ambayo imejaa mengi ambayo nimekuwa nikiandika leo hii. Wengine walisema nina majungu ila wewe umeiweka vizuri sana na kuwa NEUTRAL.
Hao Task Force nimewasikia habari zao. Wametembeza UBABE wa waziwazi na kibaya ni kuwa vyombo vya DOLA viliwaangalia tu wakitesa na utemi wao. Nashindwa kuamini kama kweli Kyela wamechagua au mtu kawachagulia.
Maadamu wao wenyewe wanakiri kuwa Mwakalinga kawaletea vitu vingi vya maendeleo na Mwakyembe hakuleta ila tu kasaidia Kuwafanya kuwa MAARUFU Tanzania, basi nawarudisha kwenye wimbo wa Marehemu Maneti na Mwalimu wangu Msasa pale Mazengo alishawahi kuutumia katika mfano kama huu akisema "....... Najuta umaarufu umeniponza............ amejenga nyumba kwao, mimi kwangu midabwada".
Mkataa pema................. Kila la kheri wana Kyela na umaarufu wenu.
Mwakalinga nilikuambia hamia Sikonge, ukakataa. Watani zako tungeliheshimu kazi yako.
Mwanamtama, naona hii ya Lipstick umeipenda sana tangu nikushushie juzi, heheheeee
Mkuu Sikonge,
Rafiki yako Mwakalinga WanaKyela wamemuingiza mjini ama wamemkaribisha nkayani. Kabla hata hajakuwa Mbunge, kuamua kujenga ghorofa, kuanzisha kituo cha radio na kugawa jezi zilizoandikwa Kyela FM aliona ndio maendeleo, hiyo si rushwa outright?! Angelifanya hayo bila ya kuwa na agenda yoyote behind tungelimwita ni mpenda maendeleo ya Kyela lakini kujenga na kugawa vitu halafu kutaka Ubunge in return ni rushwa tu.
Mwakyembe ni moto wa kuotea mbali! Hata kama angelikuwa anapigiwa kura za maoni na Watanzania wote angepeta tu bila ya kutoa jasho kujinadi. Kama walikuwepo wapambe wa Mwakyembe ni katika kulinda haki za chaguo lao asidhulumiwe wala kuhujumiwa kwa sababu tunaambiwa tayari 'Mmasai" mmoja alishasema kama Mwakyembe akirudi kwenye ubunge basi yeye si Mmasai! Tunasubiri wamuengue Dr. Mwakyembe waone kitakachotokea. Nawapa tano ndugu zangu wa Kyela kwa kuonyesha ushujaa dhidi ya Mwakipesile na genge lake. Tunataka Mkoa wa Mbeya na Tanzania isiyo na majungu wala visasi.
Mbona mwanzishaji habari hii hajaeleza jinsi ambavyo katika kampeni mahasimu wa Mwakyembe walijaribu kutumia ujanja wa kutaka Dr. Mwakyembe aanze kuzungumza ili watakapozungumza akina wagombea 'wao' wampiku. Matokeo yake, baada ya kuzungumza Dr. Mwakyembe watu walikuwa wakitawanyika wakidai tayari shughuli imekwisha na wagombea wengine kuachwa wakihutubia mashabiki wao tu! Ilipodhihirika hivyo, Dr. Mwakyembe akawa anawekwa kuzungumza mwisho ili watu wasiondoke. Haikufua dafu, baada ya kuzungumza wananchi walisema waziwazi kwamba tumeishakupitisha MBUNGE WETU Mwakyembe! Pia, sehemu zingine Dr. Mwakyembe alikuwa anazuiwa na wazee kuzunguza wakidai kwamba hana haja ya kuzungumza kwa sababu tayari keshapita!
Mkuu Sikonge,
Kama tunaitakia nchi hii mema kwa dhati tuwashabikie watu wa aina ya Dr. Mwakyembe warudi bungeni kuleta changamoto waliyokwisha kuionyesha kwa kung'oa visiki kwa maslahi ya Taifa. Naamini kabisa kama Dr. Slaa atafanikiwa kuupata urais, watu wenye msimamo kama Dr. Mwakyembe watampa support kubwa katika masuala yanayohusu maslahi ya taifa. Kwa maana nyingine msimamo utakuwa TAIFA MBELE, vyama nyuma!