2025: CHADEMA njia nyeupe Kyela, ni baada ya Mwakyembe kuutaka tena Ubunge wa Jimbo hilo

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,753
218,366
Ikiwa uchaguzi wa 2025 utakuwa huru na haki, kama tunavyotarajia kutokana na matarajio ya wananchi ya kupatikana kwa katiba mpya na tume huru ya uchaguzi, basi miongoni mwa majimbo ya mwanzo kabisa ambayo CCM itaangukia pua ni Jimbo la Kyela.

Hii ni kwa sababu chama hicho hakipendwi na wananchi wa jimbo hilo, kwa vile kinatajwa kuwa chanzo cha umaskini unaowakabili wananchi wa jimbo hilo tangu enzi na enzi. Sababu nyingine inayorahisisha kuondolewa kwa CCM kwenye jimbo hilo ni minyukano inayoendelea ndani ya chama hicho, hasa baada ya Harisson Mwakyembe kuwaambia wapambe wake kwamba anataka kurejea bungeni 2025 kwa udi na uvumba.

Tayari Mwakyembe alishaanza mipango yake hiyo mapema baada ya kufanikiwa kupanga safu ya viongozi wa CCM wa wilaya hiyo, mmoja wapo wa wapambe wa Mwakyembe waliofanikiwa kuukwaa uongozi ni Elias Mwanjala ambaye alishinda uenyekiti wa wilaya, huku pia akifanikiwa kusimika viongozi kwenye jumuiya zote za chama hicho wilayani humo.

Kimsingi ni kama mbunge wa sasa aitwaye Kinanasi anamalizia tu muda wake kutokana na kutengwa na wananchi kwa kinachodaiwa kwamba ni dharau aliyonayo kwa kila mwananchi, hasa baada ya kuwa mbunge. Inasemekana amelewa madaraka kiasi cha kupuuza kila mtu, jambo ambalo Wanyakyusa wanasema kwa lugha yao kwamba "ikwite," ambayo kwa tafsiri ya Kiswahili ni 'ameshiba'. Inafahamika kwamba mtu aliyeshiba hatakiwi kuendelea kula, hivyo anapaswa kuwekwa kando. Wanadai hata yale maboresho ya barabara chache za mji wa Kyela si juhudi za mbunge bali ni huruma tu ya serikali kwa wilaya hiyo kongwe zaidi nchini Tanzania.

Mparanganyiko huu wa CCM Kyela umewapa mwanya mkubwa sana Chadema, ambao kwa Kyela ni wengi zaidi kuliko CCM (inakadiriwa kwamba zaidi ya 70% ya wana Kyela wanaunga mkono Chadema), na wanatajwa kwamba wako karibu zaidi na wananchi kuliko CCM na wana watu makini, wasomi, na wenye uchungu na Kyela.

Ngoja tuendelee kuangalia mtifuano wao ikiwemo hata jinsi wanavyologana.

Usiondoke JF.
 
Ikiwa Uchaguzi wa 2025 utakuwa huru na haki , kama tunavyotarajia kutokana na matarajio ya Wananchi ya Kupatikana kwa Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi basi miongoni mwa Majimbo ya mwanzo Kabisa ambayo CCM itaangukia Pua ni Jimbo la Kyela .

Hii ni kwa sababu Chama hicho hakipendwi na Wananchi wa Jimbo hilo , kwa vile kinatajwa kuwa chanzo cha Umasikini unaowakabili Wananchi wa jimbo hilo tangu enzi na enzi , sababu nyingine inayorahisisha kuondolewa kwa ccm kwenye jimbo hilo ni Minyukano inayoendelea ndani ya Chama hicho hasa baada ya Harisson Mwakyembe kuwaambia wapambe wake kwamba anataka kurejea bungeni 2025 kwa udi na uvumba .

Tayari Mwakyembe alishaanza mipango yake hiyo mapema baada ya kufanikiwa kupanga safu ya viongozi wa ccm wa Wilaya hiyo , mmoja wapo wa Wapambe wa Mwakyembe waliofanikiwa kuukwaa uongozi ni Elias Mwanjala ambaye alishinda Uenyekiti wa Wilaya , huku pia akifanikiwa kusimika viongozi kwenye Jumuiya zote za Chama hicho Wilayani humo .

Kimsingi ni kama Mbunge wa sasa aitwaye Kinanasi anamalizia tu muda wake kutokana na kutengwa na Wananchi kwa kinachodaiwa kwamba ni dharau aliyonayo kwa kila Mwananchi , hasa baada ya kuwa Mbunge , inasemekana amelewa madaraka kiasi cha kupuuza kila mtu , Jambo ambalo Wanyakyusa wanasema kwa lugha yao kwamba "IKWITE" ambayo kwa tafsiri ya kiswahili ni 'AMESHIBA" , inafahamika kwamba mtu aliyeshiba hatakiwi kuendelea kula , hivyo anapaswa kuwekwa kando , Wanadai hata yale maboresho ya barabara chache za mji wa kyela si juhudi za Mbunge bali ni huruma tu ya serikali kwa wilaya hiyo kongwe zaidi nchini Tanzania .

Mparanganyiko huu wa ccm Kyela umewapa mwanya mkubwa sana Chadema , ambao kwa Kyela ni wengi zaidi kuliko ccm (Inakadiriwa kwamba zaidi ya 70% ya wana Kyela wanaunga mkono Chadema) , na wanatajwa kwamba wako karibu zaidi na wananchi kuliko ccm na wanao watu makini , wasomi na wenye uchungu na Kyela .

Ngoja tuendelee kuangalia mtifuano wao ikiwemo hata jinsi wanavyologana .

Usiondoke JF
Mungu Ibariki CHADEMA
 
Nina degree 4, sasa wewe darasa la saba utazungumza nini na mimi....................by Mwakyembe. Kweli ni IKWITE
 
Msiende na matokeo mfukoni,

Mwakyembe ametoka kupinga USHOGA na JAMII imemuunga mkono Kwa jambo Hilo la kishujaa.

By the way hajatia Nia maana uchaguzi Bado mbali,

Na maamuzi ya nani awe mbunge ni ya wananchi.
Kyela haina wala haijawahi kuwa na shoga
 
Mbona Lowassa alipata? Maridhiano Yana KAZI Gani sasa kama Kuna watu katu hawawezi PATA nafasi CDM hata wakitubu?
Mwakyembe alilidanganya Taifa , akatubu kwa Mungu , halafu unawezaje kuamini mtu anayedanganya hata kwao ?
 
mkuu wewe ni mwanamke au mwaname?
nataka kujiunga chadema ilanataka kujua kwanza kuhusu wewe..
 
Back
Top Bottom