Wana JF,
Nilibahatika kushuhudia uchaguzi wa Kyela.
Nilichogundua
1.Hata uwe na pesa kiasi gani-huwezi kuwaridhisha wana Kyela, jamaa wanapenda pesa kuliko wachaga, wanavuta kwa kila mtaka kura, siku ya mwisho hawakulala mpaka kunakucha.
2.Nilipowauliza kwanini wanampendelea yupi:
1-Dr. wanampenda tuuuuu kwa sababu pamoja na kuwa hakuleta cha maana lakini aliiweka Kyela kwenye ramani ya TZ na kikubwa wana amini alileta daraja 1. hivyo ana kila haki ya kurudi. Na yeye anasema ana uzoefu kwa hiyo wengine wasipewe.Pamoja na mengine alikuja na wapambe wa nguvu na anasema anaomba ridhaa ya wananchi kusudi aanze kazi ya kuwahudumia.
2. George Mwakalinga-huyu wanaamini pamoja na kushiriki kimaendeleo kuwaletea radio ya jamii-Kyela FM,kujenga ghorofa na kuchangia miradi mingi ya maendeleo-mashuleni etc,wanasema wanampenda lakini asubiri mpaka siku Dr. akichoka ndio watampa
3.Palikuwa na dada mmoja anaitwa Rhoda-huyu alinifurahisha kwa ushujaa wake akitegema angepewa kura kwa sababu ni dada.lakini inaelekea wanyakyusa hawathamini kina dada wala kule, gender haipo-alizunguka kila sehemu peke yake na hakutoa rushwa sana lakini aliambuliwa % ndogo sana
4.Palikuwa na m sure mmoja anaitwa Elias-huyu alikuja na gari za nguvu kama za ma waziri, pesa(anazo) na alizimwaga sana lakini kama wenzake yeye alituhumiwa kuwa anajua sana mapenzi ingawa niliona kama ni mfanya biashara mkubwa,matokeo akavuta sana kura kijijini kwao tu.
Maajabu niliyoona
a)inadaiwa kuna kundi linaitwa Task Force , wanadai hili ni la Mbunge aliyepo-lilikuwa zaidi ya sungu sungu, likilinda wengine wasiende kwenye maeneo fulani kuhonga au kuleta fujo sehemu ambazo walikuwa hawana uhakika kama mbunge wao angepita.
b)Inadaiwa pia kuwa Mbunge aliyepo na watu wake ndio walileta kadi feki ambazo wagombea wengine walizibaini na ikaleta mtafaruku lakini baadae ikasemekana zitumike,kwa hiyo sehemu zingine zilizutumika na sehemu zingine hazikutumika.
c)Takukuru walifanya kazi chini ya viwango-wakizifuatilia gari za wagombea tu na kuzi sachi wakitafuta rushwa za pesa au vitenge nk.
d)Inasemekana sasa watu hawagombei nafasi ya kwanza kwa sababu kuna uwezekano mkubwa wa mbunge aliyepo akafutwa, kwa hiyo sasa ni hongo kusudi mtu apate nafasi ya 2 kusudi lolote likitokea basi aangukiwe yeye.
e)La kusikitishisha kama ni kweli-nafasi za udiwani nyingi zimechukuliwa na watu ambao sio tu kuwa hawana elimu lakini hawana pia uwezo wa kuiletea Kyela maendeleo.
f)Vyama vingine kwa Kyela ni kama havipo,hivyo nguvu ya nani awe mbunge inategemea NEC ya CCM
h)La mwisho inasemekana ni jambo ambalo si la siri kuwa Mh.mbunge na RC na viongozi wengi hawaelewani, nikajiuliza kwa hali hii patakuwa na maendeleo Kyela?
Na nilipowaangalia wagombea wote ni kama wana nguvu(Kipesa) hawa wote kama waliyokuwa wakijinadi nayo wangechangia mawazo na pesa wakazimwaga kwa pamoja -loooh Kyela ingekuwa mbali, lakini naona pale kila atakayeondoka ndio itakuwa mwisho(Kwa maoni yangu)
Mengi tuliyoyatategemea kuwa kutakuwa na pesa za nguvu kutoka kwa mafisadi hazikuonekana na kiujumla amani ilikuwepo.