Katiba mpya sio muarobaini, katiba mpya sio kikombe cha babu kinachoweza kutibu magonjw ayote kwa mkupuo, ni mchakato wa kuweka dira wa kusema trunaenda wapi, tunelekea wapi? kujadiri matumaini yao, manung'uniko yao, ndiom maana mchakato ni muhimu kuliko katiba yenyewe.
Nafikiri mantiki kubwa ya huu mjadala ni kuangalia jinsi Azimio la Arusha lilivyokuwa, malengo yake na athari za kufa kwake...na pia unatoa nafasi ya kutathiimni nini tunaweza kujifunza kutoka kwa azimio hili
Ukitaka mtu asikae kwenye kiti lazima ukipashe moto, ili watu wafanye kazi lazima watu wasikae chini.
Mwalimu akapasha kiti moto akapasha kiti moto akaleta azimio la Arusha.
Sisi wananchi ndio wenye nchi, Rais ni mkurugenzi mtendaji, na sisi ndio wenye mali.
Mchangiaji wa nne nime mis jina lake ni Profesor some body anasema inapaswa tuangalie yale ambayo bado tunayaamini kwenye Azimio ili yaingie kwenye katiba.
Anasema wakati ule mambo yalikuwa na nguvu kwa sababu yalikuwa yanalindwa na chama, baada ya upinzani wa vyama vingi yale mambo yaliyoukua kwenye chama yaliachwa na serikali.
Mwenyekiti wa CCK anasema kuwa wakati huu wa mchakato wa katiba ni wakati sasa wa kuweka vipaombele vya taifa, kwa sababu hapa tulipofika ni kama nchi/taifa halina vipaumbele.
Anasema viongozi wanaogopa kufika hata kwenye makongamano kwa sababu wanaogopa kuwa critisized.
Kuna kitu wachangiaji bado hawajagusa nacho ni tofauti ya vipato, tukianzia mishahara wa mtu mmoja unaweza kuwa wa watu kumi wenye elimu sawa na yeye je katiba mpya haiwezi kukopa kwenye AA?
Steven Owawa ex-student UDSM anasema kuwa enzi za Azimio kulikuwa na mwelekeo wa nchi...baada ya azimio kufa nchi ikakosa mwelekeo.
Anawakumbusha CCM kabla hawajafukuzana warudi kwanza kwenye misingi ya kuanzushwa kwa chama chao....anasisitiza chama chochote chenye maono ya kushika Dola ni lazima kirudi kwenye misingi ya Azimio
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.