Maamuzi ya Zanzibar (1991) - Mwinyi Azimio la Arusha Halijageuzwa

Logikos

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
12,494
19,533
Maamuzi ya Zanzibar
Mwaka 1991 Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ilikutana mjini Zanzibar na kufanya mabadiliko ya Azimio hilo.

Akizungumza na wazee wa chama, viongozi wa Taifa, mashirika ya umma na watu binafsi Februari 25, 1991 jijini Dar es Salaam, aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM hicho na Rais Ally Hassan Mwinyi aliwatoa hofu wale wanaodhani kuwa Azimio la Arusha linageuzwa.

“Inaelekea kuna hofu kwamba Azimio la Arusha linageuzwa. Kwa hiyo tangu mwanzo, kabla ya kusema lolote, nataka tuelewane kwamba siasa yetu bado ni ile ile ya Ujamaa na Kujitegemea,” anasema na kuongeza:

“Halikugeuka wala hatutazamamii kuligeuza. Kwa hali yoyote sisi wanachama wa Chama cha Mapinduzi hatutaweza kuigeuza siasa hii. Kule Zanzibar tulizungumza mengi, miongoni mwao ni kutoa tafsiri ya baadhi ya vipengele vya Azimio ili vifanane na wakati tulionao.”

Akifafanua zaidi, Mwinyi anasema tangu azimio hilo lilipoanzishwa mwaka 1967 hadi mwaka 1991 ilikuwa imepita zaidi ya miaka 20, hivyo kulikuwa na mabadiliko mengi duniani.

“Hali yetu ya sasa hasa ya kiuchumi, siyo ile ya mwaka 1967. Ndiyo maana mishahara ya wafanyakazi ingawa imeongezeka sana, lakini bado haikidhi mahitaji yao, haiwatoshi hata wale wanaopokea mishahara mikubwa miongoni mwetu,” anasema na kuongeza:

“Isitoshe, wakati wa Azimio idadi ya Watanzania ilikuwa ndogo, sasa hivi idadi yetu imeongezeka zaidi ya mara mbili . Kwa sababu ya wingi wetu, mahitaji yameongezeka sana, wakati mapato yetu yamekuwa yakipungua wakati wote.”

Mwinyi anaongeza kuwa kila zama na mwongozo wake:
“Msahafu wa Waislamu unasema “Likulli ajalin kitab’, yaani kila zama ina kitabu chake,” anasema na kuongeza:
“Sisi wana CCM tunakubali kuwa kila zama zinahitaji kuwa na mwongozo wake. Azimio la Arusha ni mwongozo wetu wa msingi. Ni dira inayoongoza mwelekeo wa jamii yetu. Lakini tafsiri zake inabidi zirekebishwe kila inapohitajika ili zisipitwe na wakati.”

Akisisitiza kuhusu ufafanuzi wa maamuzi ya Zanzibar anasema baada ya kutangazwa kwa azimio la Arusha mwaka 1967 lilifuatiwa na matamko kama vile Azimio la Iringa la mwaka 1971 la ‘Siasa ni Kilimo’ na mwongozo wa mwaka 1981 uliotolewa kwa lengo la kukuza tafsiri ya Azimio la Arusha.

Anaongeza kuwa hata mwaka 1974 kulikuwa na agizo la Musoma kuhusu Elimu ya Kujitegemea.
“Maandiko hayo yote hayakupingana na Azimio la Arusha, ila yaliongeza mambo ambayo yalihitajika yafanane na wakati wake,” anasema.

Akizungumzia sababu ya kuanzishwa kwa Azimio la Arusha mara baada ya nchi kupata uhuru, anasema baadhi ya viongozi walianza kutumia uongozi wao kama mradi wa kujineemesha.

Msimamo wa Nyerere
Licha ya Rais wa awamu ya pili kufafanua umuhimu wa uamuzi wa Zanzibar, bado Mwalimu Nyerere aliendelea kutoridhika kuhusu msimamo mpya wa CCM.

Akizungumza na waandishi wa habari mwaka 1999, Mwalimu Nyerere alisema bado alikuwa hajaona kasoro ya Azimio la Arusha. “Mimi bado natembea nalo (Azimio la Arusha). Nalisoma tena na tena kugundua kama kuna cha kubadili. Labda ningeboresha Kiswahili nilichokitumia, lakini Azimio lenyewe bado ni thabiti. Nisingebadili hata neno moja,” anasema Mwalimu Nyerere.

Akizungumzia chimbuko lake, Mwalimu Nyerere anakubaliana na Mwinyi kuwa ilitokana na kukua kwa mgawanyiko kati walionacho na wasionacho.

“Azimio la Arusha ndilo lililoitambulisha Tanzania kama taifa. Tuliweka wazi msimamo wetu, tukatoa mwongozo wa maadili na miiko ya uongozi na tukafanya jitihada za dhati za kutimiza malengo yetu. Bado naamini kuwa mwishowe Tanzania tutarejea kwenye misingi ya Azimio la Arusha.”

Source: Gazeti la Mwananchi
 
Ataonaje dosari kwenye 'makala ' yake!!
Nikiangalia hili suala kwa macho ya CHAMA CHAKE ambacho bado kinajificha kwenye kichaka cha Ujamaa na Kujitegemea na nikiangalia kwamba Azimio hili liliwafunga viongozi wa Chama Hicho, na kwa kuona kwamba Misingi ya Chama chake inavunjika..., ukiangalia kwa muktadha huo utaona kwanini alisema haoni tatizo na Kubwa zaidi sio kwamba waliwaambia wanachama walienda wakakubaliana Zanzibar wakaja kimya kimya - ila wenye akili waliyoona yanayotokea wakajua tayari mambo yashabadilika....

Hiki chama bado kinajinasibu kwamba ni Chama cha Wakulima (Peasants) na Workers (Wafanyakazi) but since then nothing was further from the Truth.....

Ataonaje dosari kwenye 'makala ' yake,

Kulazimisha watu wawe ni vipato sawa hakuakishi fikra jadidi,hata kabla ya azimio la Zanzibar,mpwa wake akiwa na cheo Cha juu alikua rushwa toka ushirika
 
Na hio ndio unadhani ilikuwa Ujamaa kwamba mishahara sawa ?. Kwahio wewe na Peasant muuza karanga ungekuwa na kipato sawa na Julius Kambarage ?. Hilo Azimio liliweka sheria kwa viongozi ili kufanya hicho Chama chao kuwa Chama cha Wakulima na Wafanyazi na sio kabisa Mabepari na Makabaila...

Tukija kwenye Ubepari na Ujamaa; hizo pure system zinapatikana kwenye maandiko tu; practically duniani hakuna nchi ambayo 100 ni ubepari wala Ujamaa nchi zote ni mixed economies, inategemea unachanganya vipi hio mixture ili kuhudumia watu (wellfare); na huenda kwa sasa USA unaweza kusema ilikuwa / ina elements za ki-ujamaa kuliko hata Tanzania (Wakulima kupewa ruzuku, watu kupewa food stamps; au UK National Health kwa kila mtu jambo ambalo huku hata watu wanakimbia maiti za jamaa zao kwa kushindwa kuzikomboa)....

Unasema Soko Huria wakati unapangia mtu auze Korosho zake wapi, unapangia mitandao ya simu bei ya bundle ?....., Huko USA ukifanya kampuni yako ikawa kubwa itavunjwa vunjwa kwa kuambia eti ni monopoly (umekuwa mkubwa sana) waulize kina Rockefeller na Bill Gates na hata Google na Amazon watu wameanza kuitolea macho...., Unaongelea mtu kupata kutokana na nguvu zake (wakati sheria zinatungwa kumu-favor mwenye nacho) angalia mfumo wa Kodi au fuatilia watu wenye pesa nyingi duniani kama wanatoa equivalent (percentage-wise) sawa na mtu mwenye kipato kidogo ?

Na amini nakwambia mambo huwa hayahita sheria wala kuambiwa state..., wealth inavyokuwa accumulated sehemu moja mwisho wa siku wananchi wanachukua sheria mkononi na kui-redistribute hio mali...

NB: By the way tuseme hilo swala la Ujamaa halifai vipi la Kujitegemea ?!!!, Na Vipi kurudisha hiki Chama cha Wakulima na Wafanyakazi mikononi mwa hao Wakulima na Wafanyakazi ? (And since kwa sasa wafanyakazi wamekuwa kazi kuwapata (extinct) niseme Peasants na Wabangaizaji
 
Na hio ndio unadhani ilikuwa Ujamaa kwamba mishahara sawa ?. Kwahio wewe na Peasant muuza karanga ungekuwa na kipato sawa na Julius Kambarage ?. Hilo Azimio liliweka sheria kwa viongozi ili kufanya hicho Chama chao kuwa Chama cha Wakulima na Wafanyazi na sio kabisa Mabepari na Makabaila...

Tukija kwenye Ubepari na Ujamaa; hizo pure system zinapatikana kwenye maandiko tu; practically duniani hakuna nchi ambayo 100 ni ubepari wala Ujamaa nchi zote ni mixed economies, inategemea unachanganya vipi hio mixture ili kuudumia watu (wellfare); na huenda kwa sasa USA unaweza kusema ilikuwa / ina elements za ki-ujamaa kuliko hata Tanzania (Wakulima kupewa ruzuku, watu kupewa food stamps; au UK National Health kwa kila mtu jambo ambalo huku hata watu wanakimbia maiti za jamaa zao kwa kushindwa kuzikomboa)....

Unasema Soko Huria wakati unapangia mtu auze Korosho zake wapi, unapangia mitandao ya simu bei ya bundle ?....., Huko USA ukifanya kampuni yako ikawa kubwa itavunjwa vunjwa kwa kuambia eti ni monopoly (umekuwa mkubwa sana) waulize kina Rockefeller na Bill Gates na hata Google na Amazon watu wameanza kuitolea macho...., Unaongelea mtu kupata kutokana na nguvu zake (wakati sheria zinatungwa kumu-favor mwenye nacho) angalia mfumo wa Kodi au fuatilia watu wenye pesa nyingi duniani kama wanatoa equivalent (percentage-wise) sawa na mtu mwenye kipato kidogo ?

Na amini nakwambia mambo huwa hayahita sheria wala kuambiwa state..., wealth inavyokuwa accumulated sehemu moja mwisho wa siku wananchi wanachukua sheria mkononi na kui-redistribute hio mali...

NB: By the way tuseme hilo swala la Ujamaa halifai vipi la Kujitegemea ?!!!, Na Vipi kurudisha hiki Chama cha Wakulima na Wafanyakazi mikononi mwa hao Wakulima na Wafanyakazi ? (And since kwa sasa wafanyakazi wamekuwa kazi kuwapata (extinct) niseme Peasants na Wabangaizaji
Mimi nimezaliwa nimekuta athari za ujamaa,yaani watanzania wote vipato havijaachana na nchi ikipata mabadiliko taratibu, unaweza toka mji mmoja miaka kumi ukirudi Pako vilevile,hilo ni miongoni mwa malengo ya ujamaa, highest stage ya ujamaa(socialism) ni communism,ambapo properties zinakupa za wote,CCM siyo chama Cha wakulima na wafanyakazi,Wala tanu haikua hivyo,ni chama Cha siasa,kikianzishwa na wakulima(Kama walikuwepo dar) wafanyakazi na wachuuzi wa dar
 
Mimi nimezaliwa nimekuta athari za ujamaa,yaani watanzania wote vipato havijaachana na nchi ikipata mabadiliko taratibu, unaweza toka mji mmoja miaka kumi ukirudi Pako vilevile,hilo ni miongoni mwa malengo ya ujamaa,
Miongoni ya Malengo ya Ujamaa ni kutoka sehemu ukirudi miaka kumi pako vilevile ? China ni Nchi ya Kijamaa au kibepari (Kumbuka nimekwambia practically hakuna nchi ya kijamaa 100% wala Capitalists 100%) hizo ni ideology.., na Ideology ambayo inaweka People's Welfare before Profits Kwangu mimi its more of a Socialist - Ndio maana watu wana-argue hata Sweden kwamba ni Social Democracy kutokana na Kodi zake na welfare na it being a welfare state
highest stage ya ujamaa(socialism) ni communism,ambapo properties zinakupa za wote,CCM siyo chama Cha wakulima na wafanyakazi,Wala tanu haikua hivyo,ni chama Cha siasa,kikianzishwa na wakulima(Kama walikuwepo dar) wafanyakazi na wachuuzi wa dar
Again usiende kwenye Theory sana hata gwiji wa Communism (Leninism ) alisema katika Hotuba yake kwamba Free Market inaweza ikaruhusiwa lakini Commanding Heights of the Economy lazima ziwe chini ya State

Lenin used the military metaphor to justify NEP, proposing that free markets could be permitted so as long as the government retained control of certain commanding heights like heavy industry and transport.
In Marxian economics, the "commanding heights of the economy" are certain strategically important sectors of private industry. Some examples of industries considered to be part of the commanding heights include public utilities, natural resources, and sectors relating to both foreign trade and domestic trade.
 
Miongoni ya Malengo ya Ujamaa ni kutoka sehemu ukirudi miaka kumi pako vilevile ? China ni Nchi ya Kijamaa au kibepari (Kumbuka nimekwambia practically hakuna nchi ya kijamaa 100% wala Capitalists 100%) hizo ni ideology.., na Ideology ambayo inaweka People's Welfare before Profits Kwangu mimi its more of a Socialist - Ndio maana watu wana-argue hata Sweden kwamba ni Social Democracy kutokana na Kodi zake na welfare na it being a welfare state

Again usiende kwenye Theory sana hata gwiji wa Communism (Leninism ) alisema katika Hotuba yake kwamba Free Market inaweza ikaruhusiwa lakini Commanding Heights of the Economy lazima ziwe chini ya State

Lenin used the military metaphor to justify NEP, proposing that free markets could be permitted so as long as the government retained control of certain commanding heights like heavy industry and transport.
In Marxian economics, the "commanding heights of the economy" are certain strategically important sectors of private industry. Some examples of industries considered to be part of the commanding heights include public utilities, natural resources, and sectors relating to both foreign trade and domestic trade.
Kwa nini ume-highlight hapo badala ya hoja yangu yote!?..china siyo taifa la kijamaa Bali soko huria,ujamaa huenda bado uo Korea kaskazini ambako serikali inafanya kila biashara Kama tulivyokua hapa na maduka ya kaya
 
Kwa nini ume-highlight hapo badala ya hoja yangu yote!?..
Ujamaa ni nini ? Nime-highlight sehemu ya kwanza nikajibu kwa qoute ya kwanza; objectives za Ujamaa au chochote kile sio Umasikini - hii inaweza ikatokana na inefficiencies au impracticability ya jambo lakini sio objectives.., hayo mengine nimejibu chini kwamba hata Kina Lenin hawakusema kila mali iwe ya kila mtu bali Commanding Heights za Economy.....
china siyo taifa la kijamaa Bali soko huria,
Ndio maana nikakuuliza Ujamaa ni nini ? Kama Ujamaa ni Kampuni / Mali nyingi kuwa chini ya State / UMMA unajua Kampuni ngapi china ni State owned ? Na State ina mandate kiasi gani..., Kama Socialism ni Welfare State basi Sweden nayo unaiweka wapi... Ndio maana nikakwambia nchi zote ni mixed economies ila inategemea ipo mixed to what extent... Hakuna a 100 Capitalist Country hata USA sio.... Ukinibana sana takwambia China ni Social Market Economy.....
ujamaa huenda bado uo Korea kaskazini ambako serikali inafanya kila biashara Kama tulivyokua hapa na maduka ya kaya
Kwamba unasema hakuna mtu aliruhusiwa kumiliki Duka ? au kuwepo kwa Maduka machache kulisababishwa na inefficiency na sio necessarily a political system?, Kwahio hayo maduka ya Kaya yangekuwa ni Malls na Huge Supermarkets kama vile ASDA na Walmart tungekuwa Mabepari ? My point being ni kipi kinatufanya tuwe wajamaa State / Public Ownership au inefficiency of what is being done ?

Kwahio nakuuliza kwako wewe ujamaa ni nini; Private Ownership of Commanding Heights, Welfare State au ni all inefficiency na Police State without any freedom ? Sababu there is a difference - (Mfano hai ni kama Extremism ya Magaidi inavyolipa jina Baya Uislamu ingawa sio Kweli kwamba Ugaidi na yale mambo ya Ajabu ni Manifesto ya Islam)
 
Ujamaa ni nini ? Nime-highlight sehemu ya kwanza nikajibu kwa qoute ya kwanza; objectives za Ujamaa au chochote kile sio Umasikini - hii inaweza ikatokana na inefficiencies au impracticability ya jambo lakini sio objectives.., hayo mengine nimejibu chini kwamba hata Kina Lenin hawakusema kila mali iwe ya kila mtu bali Commanding Heights za Economy.....

Ndio maana nikakuuliza Ujamaa ni nini ? Kama Ujamaa ni Kampuni / Mali nyingi kuwa chini ya State / UMMA unajua Kampuni ngapi china ni State owned ? Na State ina mandate kiasi gani..., Kama Socialism ni Welfare State basi Sweden nayo unaiweka wapi... Ndio maana nikakwambia nchi zote ni mixed economies ila inategemea ipo mixed to what extent... Hakuna a 100 Capitalist Country hata USA sio.... Ukinibana sana takwambia China ni Social Market Economy.....

Kwamba unasema hakuna mtu aliruhusiwa kumiliki Duka ? au kuwepo kwa Maduka machache kulisababishwa na inefficiency na sio necessarily a political system?, Kwahio hayo maduka ya Kaya yangekuwa ni Malls na Huge Supermarkets kama vile ASDA na Walmart tungekuwa Mabepari ? My point being ni kipi kinatufanya tuwe wajamaa State / Public Ownership au inefficiency of what is being done ?

Kwahio nakuuliza kwako wewe ujamaa ni nini; Private Ownership of Commanding Heights, Welfare State au ni all inefficiency na Police State without any freedom ? Sababu there is a difference - (Mfano hai ni kama Extremism ya Magaidi inavyolipa jina Baya Uislamu ingawa sio Kweli kwamba Ugaidi na yale mambo ya Ajabu ni Manifesto ya Islam)
Ok,sijasoma essay yako,Ila endelea na ujamaa wako
 
Back
Top Bottom