Kongamano la Azimio la Arusha

Shivji ansema ktk katiba mpya ni laZima tujadili muundo wa dola....ansema inapaswa kuwepo kwa mfumo wa ushirikshi toka chini kwenda juu
 
Katiba mpya sio muarobaini, katiba mpya sio kikombe cha babu kinachoweza kutibu magonjw ayote kwa mkupuo, ni mchakato wa kuweka dira wa kusema trunaenda wapi, tunelekea wapi? kujadiri matumaini yao, manung'uniko yao, ndiom maana mchakato ni muhimu kuliko katiba yenyewe.
 
Anaonya kuwa katiba mpya sio mwarobaini wa kutibu kila tatizo lililopo.....itakuwa ni nafasi ya wananchi kutoa malalamiko yao
 
Anasema kuwa katika mjadala huu, mzimu wa azimio la Arusha utaendelea kutusumbua.....amemaliza sasa ni zamu ya watu kuchangia
 
Shivji amemaliza kwa kufunga kwa kusema mzimu wa azimio la arusha litatutesa sana
 
Nafikiri mantiki kubwa ya huu mjadala ni kuangalia jinsi Azimio la Arusha lilivyokuwa, malengo yake na athari za kufa kwake...na pia unatoa nafasi ya kutathiimni nini tunaweza kujifunza kutoka kwa azimio hili
 
Kwa kweli Prof. Shivji ni mkali anasema chama hakikushika hatamu tu bali kilishika UTAMU
 
Mchangiaji wa kwanza anasema kuwa watawala walizima azimio la Arusha sbb lilikuwa ni moto kwao na viti vilikuwa havikaliki
 
Msafiri toka DUCE:

Ukitaka mtu asikae kwenye kiti lazima ukipashe moto, ili watu wafanye kazi lazima watu wasikae chini.

Mwalimu akapasha kiti moto akapasha kiti moto akaleta azimio la Arusha.
Sisi wananchi ndio wenye nchi, Rais ni mkurugenzi mtendaji, na sisi ndio wenye mali.
 
Anasema kuwa katk katiba mpya kuna umuhimu wa kuingizwa kwa azimio la Arusha kama msingi wa uwajibikaji kwa viongozi
 
Mchangiaji wa pili ni mwanachuo wa UDSM anasema kuwa lengo la mwalimu ilikuwa ni kupingana na unyonyaji.

Anauliza wako wapi viongozi wa sasa ambao wangeweza kukemea haya yanayoendelea kama vile Mwalimu alivyonuia wakati wa Azimio?
 
Huyu mchangiaji wa pili anasema viongozi wataakari kama yale yaliyokuwemo kwenye azimio wa Arusha
 
Huyu mchangiaji wa tatu anaonyesha kushangazwa na wale viongozi wa umma wasiotaka kutangaza mali zao.

Anashauri kuwa wakati wa kuandikwa kwa katiba haya mambo ya kutenganisha mali na utawala na mishahara miwili miwili iwe ni sheria.
 
Mchangiaji wa nne nime mis jina lake ni Profesor some body anasema inapaswa tuangalie yale ambayo bado tunayaamini kwenye Azimio ili yaingie kwenye katiba.

Anasema wakati ule mambo yalikuwa na nguvu kwa sababu yalikuwa yanalindwa na chama, baada ya upinzani wa vyama vingi yale mambo yaliyoukua kwenye chama yaliachwa na serikali.
 
Mwenyekiti wa CCK anasema kuwa wakati huu wa mchakato wa katiba ni wakati sasa wa kuweka vipaombele vya taifa, kwa sababu hapa tulipofika ni kama nchi/taifa halina vipaumbele.

Anasema viongozi wanaogopa kufika hata kwenye makongamano kwa sababu wanaogopa kuwa critisized.
 
Anasema kuwa ni bora bepari mwenye roho ya kijamaa kuliko mjamaa mwenye roho ya kibepari....na viongozi wengi wetu ndio walivyo
 
Kuna kitu wachangiaji bado hawajagusa nacho ni tofauti ya vipato, tukianzia mishahara wa mtu mmoja unaweza kuwa wa watu kumi wenye elimu sawa na yeye je katiba mpya haiwezi kukopa kwenye AA?
 
Mchangiaji mwanafunzi wa Engineering UDSM anasema kuwa nyingi ya sera na maazimio ynayosemwa yanakuwa ni maneno tu hakuna utekelezaji
 
Steven Owawa ex-student UDSM anasema kuwa enzi za Azimio kulikuwa na mwelekeo wa nchi...baada ya azimio kufa nchi ikakosa mwelekeo.
Anawakumbusha CCM kabla hawajafukuzana warudi kwanza kwenye misingi ya kuanzushwa kwa chama chao....anasisitiza chama chochote chenye maono ya kushika Dola ni lazima kirudi kwenye misingi ya Azimio
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom