Wajua japo Rais ni sehemu ya Bunge, bado hana mamlaka ya kuliingilia Bunge? Ili kufuta IGA ya DPW, Rais anapaswa kulivunja Bunge?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,604
Wanabodi,

Kama kawaida yangu, kila nikipata fursa, huja na makala zangu za kwa maslahi ya taifa, makala ya leo ni kuhusu Ijue Katiba: Japo Rais ni Sehemu ya Bunge, kwa kuliunda, kulivunja na kuridhia miswada kuwa sheria, lakini Rais Hana Mamlaka ya Kuliingilia Bunge?. Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania limemtaka Rais Samia kuifuta IGA ya DPW, iliyoridhiwa na Bunge, ili Rais Samia aifute hiyo IGA, ambayo baada ya kuridhiwa ni Azimio la Bunge, inambidi Rais kwanza kulivunja Bunge, ndipo alivunje Azimio la Bunge.

Katiba ni kakitabu kadogo tuu ka ukurasa, lakini kuielewa katiba, kunahitaji uwezo wa ziada, kama ilivyo kuielewa Biblia Takatifu au Quran Tukufu, kila mtu anayejua kusoma na kuandika, anaweza kusoma Biblia na Quran, lakini kuielewa unahitaji kupata ufunuo.

Vivyo hivyo kwa katiba ya JMT, kila mtu yoyote mwenye uwezo wa kusoma na kuandika, anaweza kuisoma katiba ila kuielewa kunahitaji ujaaliwe ufunuo.

Kwa mujibu wa katiba, mamlaka rasmi ya kuitafsiri katiba ni mhimili wa Mahakama Kuu, lakini it's very unfortunately mhimili wa serikali hawaijui katiba ndio maana wanatunga miswada kinyume cha katiba.

Mhimili wa Bunge, nao it's very unfortunately wanatunga sheria batili zinazokwenda kinyume cha katiba, na juzi kati hapa Bunge letu Tukufu, limeridhia IGA ya DPW na Bandari zetu ambayo iko kinyume cha katiba na sheria zetu.

Mhimili wa Mahakama wenye jukumu la kutafsiri katiba na sheria, nao it's very unfortunately hautimizi wajibu wake kikamilifu kwa kubariki uvunjifu wa katiba unaofanywa na mhimili wa serikali na mhimili wa Bunge!.

Mimi ni Mwanafunzi wa sheria wa Prof. Shivji, kiukweli niko very proud kuwa miongoni mwa wanafunzi tulio mwelewa vizuri Prof. Shivji alipokuwa akitufundisha somo la katiba, na ndio maana somo lake, mimi nimejenga kibanda, kwa kupata A, hivyo sasa najihesabu ni mwalimu wa kujitolea wa somo la Ijue Katiba, na nimeendesha mihadhara mbalimbali ya katiba ambayo imesaidia sana Bunge letu na serikali yetu, na sasa naanzisha vipindi vya Televisheni weekly kuelimisha umma kuhusu katiba, sheria na haki ambayo vitausaidia sana mhimili wa Mahakama kutenda haki.

Miongoni mwa wasioijua katiba ya JMT, ni Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, wametoa waraka wa kuipinga DPW, na kumtaka rais Samia asitishe ile IGA ya DPW na Bandari zetu, bila kujua kwa mujibu wa katiba, rais Samia hana uwezo huo!.

Ila hawa Maaskofu Katoliki, ni kiboko!.
Juzi baada ya kuutoa waraka wao, leo asubuhi katika makanisa yote ya Katoliki Tanzania, waraka huo umesomwa kanisani, mimbarini na madhabahuni!.

Baada ya kuusoma waraka wa TEC humu JF, Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC): Hatuungi mkono Mkataba wa Bandari. Sauti ya Watu ni sauti ya Mungu niliuliza Mpeni Mungu yaliyo ya Kimungu na Kaisari yaliyo ya Kaisari! Hiki kinachofanywa na Baraza la Maaskofu Katoliki, sio kuchanganya dini na siasa? na baada ya kitendo cha kusoma tamko la kisiasa Mimbarini na Madhabahuni, nauliza tena, huku sio kuchanganya dini na siasa?.

Lile tamko la Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania kuipinga DPW na Bandari zetu, leo limesomwa mimbarini na madhabahuni na maparoko wa makanisa yote ya Katoliki Tanzania nzima kwenye kila ibada ya kila misa!.

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania kama taasisi huru, iko huru kutoa maoni yake yoyote kuhusu jambo lolote, yakiwemo maoni ya kisiasa, kiuchumi na kijamii, lakini kitendo cha Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, TEC, kutoa maoni ya kisiasa kuipinga DPW na Bandari zetu, kitendo cha kanisa Katoliki Tanzania kusoma maoni hayo ya kisiasa ya TEC, mimbarini na madhabahuni, sio kuchanganya dini na siasa?.

Madhabahuni na mimbarini ni mahala pa kuabudia, kitendo cha kanisa Katoliki Tanzania, kuusoma waraka huu mimbarini madhabahuni, ni **** kuwaaminisha Wakatoliki kuwa kuipinga DPW na Bandari zetu ni sehemu ya ibada, hivyo Wakatoliki wote sasa wanatakiwa kuipinga DPW. Wale Wakatoliki wanaiunga mkono DPW wakioongozwa na Makamo wetu wa Rais, Dr. Philip Mpango, tunawaweka kwenye hali gani?. Huku sio kuwakwaza Wakatoliki wote tunaounga mkono DPW na Bandari zetu?.

Waraka huo unasisitiza Vox Populi is Vox Dei, kumaanisha sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, Tangu issue ya DPW ilipoibuka, kanisa Katoliki limewahi kukusanya maoni ya waumimi wake kuhusu jambo hili, hivyo kufikia hii conclusion kuwa Watanzania wengi hawaitaki DPW?.

Mimi ni Mkristo Mkatoliki, na toka issue ya DPW iibuke, sijawahi kukosa kanisani hata mara moja, sikumbuki kuwahi kuulizwa maoni yetu kuhusu DPW!, kama kuna Mkatoliki yoyote aliwahi kuombwa maoni yake na kanisa Katoliki, naomba ajitokeze.

Kama kanisa Katoliki halijakusanya maoni ya waumini wake kuhusu DPW, hii hoja ya TEC kuwa Watanzania wengi hawaitaki DPW, wameyatoa wapi?.

Kitendo cha Kanisa Katoliki Tanzania, kukusanya maoni ya Maaskofu wa Katoliki Tanzania, na kuyageuza ndio maoni ya Watanzania, huku sio kusema uongo?.

Na kitendo cha kuusoma uongo huo wa TEC kuwa Watanzania wengi hawaitaki DPW, na kuusomea mimbarini na madhabahuni, huku sio kumkosea Mungu, kuitumia mimbari yake na madhabahu yake vibaya, badala ya kuitumia mimbari na madhabahu, kwa kuabudia, kanisa Katoliki Tanzania linaitumia mimbari na madhabahu kupigia siasa za uoga za kuipinga DPW kwasababu tuu ni ya Waarabu, hivyo kudhani DPW ikija inakuja kueneza Uislam!, na kwa kuzingatia, hivi tuu DPW bado haijapewa mkataba, imetoa misaada ya kujenga misikiti kadhaa, ikipewa Bandari, kazi ya kwanza si ni itakuwa ni kujenga masjid?.

Bunge letu Tukufu limepitisha Azimio la Bunge kuiridhia IGA ya DPW, hawa Maaskofu wa Katoliki Tanzania, wamemtaka Rais Samia alifute Azimio la Bunge kuridhia IGA ya DPW,
12. Hivyo, sisi Maaskofu Katoliki Tanzania wenye jukumu la kusimamia ustawi wa kila mwanadamu tunamwomba Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mamlaka aliyo nayo asitishe wasilisho la ridhio hili kwa upande wa pili,na vile vile Bunge nalo lifute ridhio la Mkataba huu unaolalamikiwa.
Kumbe maaskofu wetu hawaijui katiba!, hawajui kuwa kwa mujibu wa katiba yetu, Rais wa JMT hana mamlaka ya kufuta Azimio la Bunge!, ili Rais Samia alifute Azimio la Bunge, inambidi Rais Samia alivunje Bunge!.

Rais wa JMT ni sehemu ya Bunge kwa mambo matatu tuu, 1. Kuliunda Bunge, kuridhia muswada kuwa sheria na kulivunja Bunge.

Kwa upande wa miswada ya sheria, Bunge likitunga sheria, rais anaweza kukataa kuisaini, anatakiwa kurejesha Bungeni kurekebishwa, Bunge likigoma kurekebisha, rais anakuwa hana jinsi bali ni kulivunja Bunge!.

Lakini kwa upande wa Azimio la Bunge, Bunge likiisha pitisha Azimio la Bunge, rais wa JMT hana mamlaka ya kuingilia chochote bali ni kuteleleza tuu Azimio la Bunge, vinginevyo ni alivunje Bunge!.

Hawa Maaskofu wa Katoliki Tanzania sio mchezo!, wanampangia hadi rais wa JMT na kumlazimisha apindue jambo lililoridhiwa na Bunge!.

Kwa mujibu wa katiba ya JMT, rais wa JMT halazimiki kufuata ushauri wa yoyote kwenye kufikia maamuzi, isipokuwa katika mambo mawili tuu, ambayo rais wa JMT analazimika kuamrishwa kufuata.

Mambo hayo ni 1.Kuiwasilisha Bungeni ndani ya siku 7, ripoti ya CAG, baada ya kuipokea, na asipoiwasilisha ripoti hiyo ndani ya siku 7, inapofika siku ya 6, then CAG anatakiwa am bypass rais na kuwasilisha ripoti hiyo Bungeni. Hapa ni rais wa JMT anapangiwa na analazimishwa atake asitake!.

Ila Bunge letu lilivyo la mazuzu, likapitisha Azimio batili la Bunge kuwa halipokei ripoti ya CAG! Je, Wajua Bunge linaweza kutoa azimio batili? CAG yuko kikatiba. Je, Bunge lina uwezo kutopokea ripoti ya CAG?

Kiukweli Bunge lile lilipaswa kunishukuru sana mimi, kwasababu ni mimi ndiye niliyewaambia Azimio lao hilo ni Azimio batili, na nikawaambia kitu kitakachowatokea iwapo Bunge halitapokea ripoti ya CAG Je, Wajua Bunge linaweza kuvunjwa Siku 7 Zijazo?. lisipopokea ripoti ya CAG, Bunge linavunjwa kwa mujibu wa Katiba

Kitu kilichofanyika ni kwanza rais aliwasilisha ripoti ya CAG Bungeni kabla hajawa by passed na CAG, pili Bunge likaondoa Azimio lao batili kimya kimya, likaipokea ripoti ya CAG.

Jambo la pili ambalo rais wa JMT anaamrishwa ni kutekeleza Azimio la Bunge.

Baada ya Bunge letu Tukufu kuridhia IGA ya DPW na Bandari zetu, pamoja na mapungufu yake yote ya kisheria, IGA sio mkataba ni makubaliano tuu, mkataba ni HGA, hivyo tunaweza kabisa kuwa na HGA nzuri.

Paskali
 
Nitarudi kusoma japo nimetanzika kidogo maana ata Rais mle kuna Saini yake! Kwamba aligiza kikasainiwe kitu ambacho yeye hakijui? na kwanini atoe power hiyo ikiwa yeye hajakisoma na kujilidhisha kama kitu hicho ni kizuri au kibaya kwa Taifa lake?

Kuwepo kwa sahihi ya Rais mle ndanihakufanyi ionekana Rais aliwashinikiza wengine wakubaliane na Mkataba? Rais hapaswi kuwajibika kwa kuubali vitu ambavyo vinaumiza Taifa lake? Rais hapaswi kuwajibika kwa kwenda kinyume na kiapo chake?

binafsi naona kuleta uwajibikaji lazima Rais ajiuzulu tu sababu ametuonesha wazi kuwa hayupo makini.

2. 2018 Baraza la Maaskofu lilipinga kuminywa kwa Demokrasia na Uhuru wa vyobo vya Habari nchini.
Hapa napo tusemaje? wakiona kuna shida kwaajii ya wananchi wasiwasemee?
 
Rais Yuko kwenye corner ambayo hachomoki ni either afute Mkataba kwa kuivunja azimio la Bunge au akubali kuishia Sasa kwa urais wake kabla ya 2025

Pia ategemee vita Kali ya kidini ambayo haijawahi tokea

NB: Siku 5 kabla ya IGA kwenda Bungeni , Serikali ilikaa kikao na Viongozi wa Kiislam (BAKWATA) including Mufti ili waiunge mkono Serikali katika suala la Bandari, hii inadhihirisha Serikali ilishasoma upepo na ni ngumu kuikataa IGA kutokana na Makubaliano ya Rais na Waarabu

Kiufupi huu mkataba wa Bandari tunakoelekea Kuna uwezekano CCM wakamtosa Samia , mambo yameshaharibika sana (In JK Voice)
 
Wanabodi,
Kama kawaida yangu, kila nikipata fursa, huja na makala zangu za kwa maslahi ya taifa, makala ya leo ni kuhusu Ijue Katiba: Japo Rais ni Sehemu ya Bunge, kwa kuliunda, kulivunja na kuridhia miswada kuwa sheria, lakini Rais Hana Mamlaka
"hivyo kudhani DPW ikija inakuja kueneza Uislam!, na kwa kuzingatia, hivi tuu DPW bado haijapewa mkataba, imetoa misaada ya kujenga misikiti kadhaa, ikipewa Bandari, kazi ya kwanza si ni itakuwa ni kujenga masjid?".

Sasa hapo unaona kuna uwekezaji wenye tija au ni kueneza dini tu. Wakati ukoloni unaingia barani Africa, waliotangulizwa walikuwa hawa hawa watu wa dini na matokeo yake tujikuta tupo utumwani.

Yaani leo hii tukubali kuuza bandari zetu zote chini ya mtu mmoja tena kwa mkataba usiyo na ukomo.

Tunakuheshimu sana, usitake na wewe tukuone poyoyo tu.
 
Serikali imeingia mkataba wa kimataifa, imepewa baraka na Bunge kupitia azimio la Bunge. Serikali inaweza kujitoa kwenye huo mkataba wa kimataifa na ikaomba tena baraka za Bunge.
Tumeshawahi kufanya hivyo huko nyuma.

Azimio linaloanzia bungeni na kupitishwa na bunge ndio haliwezi kufutwa na serikali pasipo kulivunja bunge, au Bunge lenyewe liamue kulifuta azimio hilo. Mfano mzuri ni lile azimio la wabunge wa G55 kudai serikali ya Tanganyika wakati wa Mwinyi, liletwa na Bunge na likafutwa na Bunge.

Mkataba wa DPW haujaanzia bungeni wala haujaletwa kwa azimio la Bunge. Bunge limeazimia kuubariki baada ya serikali kuomba baraka hizo, ni mkataba wa serikali. Na serikali inaweza kuachana nao.

Kuhusu waraka wa TEC tusiwe wanafiki, serikali inazitumia sana taasisi za dini kufanya siasa, sasa siku taasisi hizo zikiwa na mawazo tofauti ya kisiasa tusihamaki. Hilo tumelitaka wenyewe.
 
Wanabodi,
Kama kawaida yangu, kila nikipata fursa, huja na makala zangu za kwa maslahi ya taifa, makala ya leo ni kuhusu Ijue Katiba: Japo Rais ni Sehemu ya Bunge, kwa kuliunda, kulivunja na kuridhia miswada kuwa sheria, lakini Rais Hana Mamlaka ya Kuliingilia Bunge?. Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania limemtaka Rais Samia kuifuta IGA ya DPW, iliyoridhiwa na Bunge, ili Rais Samia aifute hiyo IGA, ambayo baada ya kuridhiwa ni Azimio la Bunge, inambidi Rais kwanza kulivunja Bunge, ndipo alivunje Azimio la Bunge.

Katiba ni kakitabu kadogo tuu ka ukurasa, lakini kuielewa katiba, kunahitaji uwezo wa ziada, kama ilivyo kuielewa Biblia Takatifu au Quran Tukufu, kila mtu anayejua kusoma na kuandika, anaweza kusoma Biblia na Quran, lakini kuielewa unahitaji kupata ufunuo.

Vivyo hivyo kwa katiba ya JMT, kila mtu yoyote mwenye uwezo wa kusoma na kuandika, anaweza kuisoma katiba ila kuielewa kunahitaji ujaaliwe ufunuo.

Kwa mujibu wa katiba, mamlaka rasmi ya kuitafsiri katiba ni mhimili wa Mahakama Kuu, lakini it's very unfortunately mhimili wa serikali hawaijui katiba ndio maana wanatunga miswada kinyume cha katiba.

Mhimili wa Bunge, nao it's very unfortunately wanatunga sheria batili zinazokwenda kinyume cha katiba, na juzi kati hapa Bunge letu Tukufu, limeridhia IGA ya DPW na Bandari zetu ambayo iko kinyume cha katiba na sheria zetu.

Mhimili wa Mahakama wenye jukumu la kutafsiri katiba na sheria, nao it's very unfortunately hautimizi wajibu wake kikamilifu kwa kubariki uvunjifu wa katiba unaofanywa na mhimili wa serikali na mhimili wa Bunge!.

Mimi ni Mwanafunzi wa sheria wa Prof. Shivji, kiukweli niko very proud kuwa miongoni mwa wanafunzi tulio mwelewa vizuri Prof. Shivji alipokuwa akitufundisha somo la katiba, na ndio maana somo lake, mimi nimejenga kibanda, kwa kupata A, hivyo sasa najihesabu ni mwalimu wa kujitolea wa somo la Ijue Katiba, na nimeendesha mihadhara mbalimbali ya katiba ambayo imesaidia sana Bunge letu na serikali yetu, na sasa naanzisha vipindi vya Televisheni weekly kuelimisha umma kuhusu katiba, sheria na haki ambayo vitausaidia sana mhimili wa Mahakama kutenda haki.

Miongoni mwa wasioijua katiba ya JMT, ni Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, wametoa waraka wa kuipinga DPW, na kumtaka rais Samia asitishe ile IGA ya DPW na Bandari zetu, bila kujua kwa mujibu wa katiba, rais Samia hana uwezo huo!.

Ila hawa Maaskofu Katoliki, ni kiboko!.
Juzi baada ya kuutoa waraka wao, leo asubuhi katika makanisa yote ya Katoliki Tanzania, waraka huo umesomwa kanisani, mimbarini na madhabahuni!.

Baada ya kuusoma waraka wa TEC humu JF, Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC): Hatuungi mkono Mkataba wa Bandari. Sauti ya Watu ni sauti ya Mungu niliuliza Mpeni Mungu yaliyo ya Kimungu na Kaisari yaliyo ya Kaisari! Hiki kinachofanywa na Baraza la Maaskofu Katoliki, sio kuchanganya dini na siasa? na baada ya kitendo cha kusoma tamko la kisiasa Mimbarini na Madhabahuni, nauliza tena, huku sio kuchanganya dini na siasa?.

Lile tamko la Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania kuipinga DPW na Bandari zetu, leo limesomwa mimbarini na madhabahuni na maparoko wa makanisa yote ya Katoliki Tanzania nzima kwenye kila ibada ya kila misa!.

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania kama taasisi huru, iko huru kutoa maoni yake yoyote kuhusu jambo lolote, yakiwemo maoni ya kisiasa, kiuchumi na kijamii, lakini kitendo cha Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, TEC, kutoa maoni ya kisiasa kuipinga DPW na Bandari zetu, kitendo cha kanisa Katoliki Tanzania kusoma maoni hayo ya kisiasa ya TEC, mimbarini na madhabahuni, sio kuchanganya dini na siasa?.

Madhabahuni na mimbarini ni mahala pa kuabudia, kitendo cha kanisa Katoliki Tanzania, kuusoma waraka huu mimbarini madhabahuni, ni **** kuwaaminisha Wakatoliki kuwa kuipinga DPW na Bandari zetu ni sehemu ya ibada, hivyo Wakatoliki wote sasa wanatakiwa kuipinga DPW. Wale Wakatoliki wanaiunga mkono DPW wakioongozwa na Makamo wetu wa Rais, Dr. Philip Mpango, tunawaweka kwenye hali gani?. Huku sio kuwakwaza Wakatoliki wote tunaounga mkono DPW na Bandari zetu?.

Waraka huo unasisitiza Vox Populi is Vox Dei, kumaanisha sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, Tangu issue ya DPW ilipoibuka, kanisa Katoliki limewahi kukusanya maoni ya waumimi wake kuhusu jambo hili, hivyo kufikia hii conclusion kuwa Watanzania wengi hawaitaki DPW?.

Mimi ni Mkristo Mkatoliki, na toka issue ya DPW iibuke, sijawahi kukosa kanisani hata mara moja, sikumbuki kuwahi kuulizwa maoni yetu kuhusu DPW!, kama kuna Mkatoliki yoyote aliwahi kuombwa maoni yake na kanisa Katoliki, naomba ajitokeze.

Kama kanisa Katoliki halijakusanya maoni ya waumini wake kuhusu DPW, hii hoja ya TEC kuwa Watanzania wengi hawaitaki DPW, wameyatoa wapi?.

Kitendo cha Kanisa Katoliki Tanzania, kukusanya maoni ya Maaskofu wa Katoliki Tanzania, na kuyageuza ndio maoni ya Watanzania, huku sio kusema uongo?.

Na kitendo cha kuusoma uongo huo wa TEC kuwa Watanzania wengi hawaitaki DPW, na kuusomea mimbarini na madhabahuni, huku sio kumkosea Mungu, kuitumia mimbari yake na madhabahu yake vibaya, badala ya kuitumia mimbari na madhabahu, kwa kuabudia, kanisa Katoliki Tanzania linaitumia mimbari na madhabahu kupigia siasa za uoga za kuipinga DPW kwasababu tuu ni ya Waarabu, hivyo kudhani DPW ikija inakuja kueneza Uislam!, na kwa kuzingatia, hivi tuu DPW bado haijapewa mkataba, imetoa misaada ya kujenga misikiti kadhaa, ikipewa Bandari, kazi ya kwanza si ni itakuwa ni kujenga masjid?.

Bunge letu Tukufu limepitisha Azimio la Bunge kuiridhia IGA ya DPW, hawa Maaskofu wa Katoliki Tanzania, wamemtaka Rais Samia alifute Azimio la Bunge kuridhia IGA ya DPW,

Kumbe maaskofu wetu hawaijui katiba!, hawajui kuwa kwa mujibu wa katiba yetu, Rais wa JMT hana mamlaka ya kufuta Azimio la Bunge!, ili Rais Samia alifute Azimio la Bunge, inambidi Rais Samia alivunje Bunge!.

Rais wa JMT ni sehemu ya Bunge kwa mambo matatu tuu, 1. Kuliunda Bunge, kuridhia muswada kuwa sheria na kulivunja Bunge.

Kwa upande wa miswada ya sheria, Bunge likitunga sheria, rais anaweza kukataa kuisaini, anatakiwa kurejesha Bungeni kurekebishwa, Bunge likigoma kurekebisha, rais anakuwa hana jinsi bali ni kulivunja Bunge!.

Lakini kwa upande wa Azimio la Bunge, Bunge likiisha pitisha Azimio la Bunge, rais wa JMT hana mamlaka ya kuingilia chochote bali ni kuteleleza tuu Azimio la Bunge, vinginevyo ni alivunje Bunge!.

Hawa Maaskofu wa Katoliki Tanzania sio mchezo!, wanampangia hadi rais wa JMT na kumlazimisha apindue jambo lililoridhiwa na Bunge!.

Kwa mujibu wa katiba ya JMT, rais wa JMT halazimiki kufuata ushauri wa yoyote kwenye kufikia maamuzi, isipokuwa katika mambo mawili tuu, ambayo rais wa JMT analazimika kuamrishwa kufuata.

Mambo hayo ni 1.Kuiwasilisha Bungeni ndani ya siku 7, taarifa ya CAG, baada ya kuipokea, na asipoiwasilisha taarifa hiyo ndani ya siku 7, inapofika siku ya 6, then CAG anatakiwa am bypass rais na kuwasilisha taarifa hiyo Bungeni. Hapa ni rais wa JMT anapangiwa na analazimishwa atake asitake!.

Ila Bunge letu lilivyo la mazuzu, likapitisha Azimio batili la Bunge kuwa halipokei ripoti ya CAG! Je, Wajua Bunge linaweza kutoa azimio batili? CAG yuko kikatiba. Je, Bunge lina uwezo kutopokea ripoti ya CAG?

Kiukweli Bunge lile lilipaswa kunishukuru sana mimi, kwasababu ni mimi ndiye niliyewaambia Azimio lao hilo ni Azimio batili, na nikawaambia kitu kitakachowatokea iwapo Bunge halitapokea ripoti ya CAG

Kitu kilichofanyika ni kwanza rais aliwasilisha ripoti ya CAG Bungeni kabla hajawa by passed na CAG, pili Bunge likaondoa Azimio lao batili kimya kimya, likaipokea ripoti ya CAG.

Jambo la pili ambalo rais wa JMT anaamrishwa ni kutekeleza Azimio la Bunge.

Baada ya Bunge letu Tukufu kuridhia IGA ya DPW na Bandari zetu, pamoja na mapungufu yake yote ya kisheria, IGA sio mkataba ni makubaliano tuu, mkataba ni HGA, hivyo tunaweza kabisa kuwa na HGA nzuri.

Paskali

Umeupitia huu uzi?
 
Rais Yuko kwenye corner ambayo hachomoki ni either afute Mkataba kwa kuivunja azimio la Bunge au akubali kuishia Sasa kwa urais wake kabla ya 2025

Pia ategemee vita Kali ya kidini ambayo haijawahi tokea

NB: Siku 5 kabla ya IGA kwenda Bungeni , Serikali ilikaa kikao na Viongozi wa Kiislam (BAKWATA) including Mufti ili waiunge mkono Serikali katika suala la Bandari, hii inadhihirisha Serikali ilishasoma upepo na ni ngumu kuikataa IGA kutokana na Makubaliano ya Rais na Waarabu

Kiufupi huu mkataba wa Bandari tunakoelekea Kuna uwezekano CCM wakamtosa Samia , mambo yameshaharibika sana (In JK Voice)
Mpuuzi ww x
 
Tulii ni kiongozi wa mhimili, Leo amepewa na kusomewa azimio la Tech!!

Wewe ulisali parokia ipi Leo?

Usijifanye hujui Rais ndo Bungez na mahakamar,

Akiamua kufuta anarudisha IGA bungeni, inafutwa, wabunge wanapiga makofi kupongezwa,

Akiamua, mahakama ya Rufaa itaipa ushindi timu Wazalendo under Mwambukusi, Bunge linamalizia kufuta.

Mjadala uliisha Padri Slaa alipoachiwa na Kutolewa waraka wa tech!!
 
Back
Top Bottom