Kongamano la Azimio la Arusha

PMNBuko

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
967
154
Ndugu wana JF,

Salaam.

Taarifa ya habari ya jana ITV saa 2.00 usiku, ilitangazwa kuwa leo kutakuwepo na mjadala juu ya Mapitio ya Azimio la Arusha na Katiba Mpya.

Namna ambavyo Azimio hilo linaweza kuhuishwa katika katiba mpya ijayo.
Mjadala upo ukumbi wa Nkrumah UDSM, utaoneshwa live na ITV na kutangazwa na Radio One.

Tafadhali, aliyeko hapo au uko na TV yako tujulisheni sie huku tuko field tunahudumia jamii japo tuna Generator na Laptop zetu.

Asanteni.
 
Prof. Shivji ndiye atakuwa mzungumzaji leo katika mjadala huo wa Azimio la Arusha. Kipindi hicho kitarushwa saa nne asubuhi hii. Fuatilia tafadhali na mtujuze.
 
Anasema sehemu kubwa ya watu wlaioshiriki mjadala ule na watanzania wanaoishi leo wengi wao ni vijana ambapo wengi hawakuliona Azimio la Arusha likizaliwa.

Wengi walisimuliwa, inawezekana pia kulikuwa na propaganda za kupotosha AA. Lakini anasema kukusanyika kwa vijana hao kunaonyesha kuwa Vijana wameanza kugundua kuwa kulikuwa na kitu ndani ya AA.
 
Kongamano la azimio la arusha linalofanyika udsm na kuoneshwa na itv limeshaanza na mwenyekiti ni Bashiru Ally na sasa anaongea Prof Issa Shivji
 
SHIVJI ANASEMA;

Baada ya miaka 10, baada ya Kifo cha Mwalimu wananchi wa kawaida walipo hojiwa jinsi walivyomkumbuka Mwalimu walisema, wakimkumbuka mwalimu wanakumbuka AA.

Hii inaonyesha kuwa AA lilitujali, mwaka jana kwenye Kongamano la AA vijana wengi waliomba nakala ya AA. Na nakala chache zilizokuwepo ziligombewa.

Ushahidi wa kimazingira, mazingira yaliyopo leo, wananchi wamepoteza tumaini, hawajui ya kesho wala hawataki kujua ya kesho. Wamepoteza matumaini katika fikra za taifa lao, na baya zaiadi na hatari wameeanza kupoteza imani katika taasisi za vyombo vya..... (Sijasikia).

Katika hali kama hii ama unaangukia katika ushirikina au jambo mbadala litakalo toa matumaini. AA linatoa matumaini ndio maana wananchi walisema AA lilitujali na ndio maana vijana walitaka nakala za AA.
 
Shivji anawakilisha chimbuko la AA sababu;

Ni mwalimu mwenyewe, anasema baada ya uhuru viongozi walio iningia katika madaraka ya kiserikali baada ya uhuru walianza kujilimbikiza mali na kuishi maisha ya anasa.

Na makampuni ya kimataifa ya kibepari wakaanza kuwavutia wanasiasa kwa kutoa hisa katika makampuni yao na vyeo vya ukurugenzi ili waje wapate tenda, hiyo ilikuwa ni hongo.
wakati huo tulikuwa tunawaita Wabenzi.
 
Shivji dzaini fluni ni mhindi inakuaje anaijua TZ kiasi hicho, maanake yupo fit katika kila jambo
 
Matatizo ya ufisadi na uwajibikaji usioridhisha yasinge tufika kama tungefuata misingi ya azimio la Arusha. Wakati tukijadiri katiba mpya tufikiri pia juu ya azimio la Arusha
 
Matatizo ya ufisadi na uwajibikaji usioridhisha yasinge tufika kama tungefuata misingi ya azimio la Arusha. Wakati tukijadiri katiba mpya tufikiri pia juu ya azimio la Arusha
 
Wanafunzi wa UDSM wali lalamikia mishahara minono ya tabaka la viongozi wa serikali.
Pale pale Mwalimu alitangaza kupunguza mshahara wake na mawaziri wake kwa asilimia 20.
Baada ya hapo AA lilizaliwa huko Arusha
 
Ngoja nifanye order ya mbuzi katoliki kwanza...i have no appetite na popcorn leo! hii mijamaa inaitwa Dowans haichelewi kunikatia umeme..
 
Anasema AA lilijikita katika Imani ya TANU. Nguzo kuu ya Imani ya Tanu ilikuwa imani ya kwanza Binadamu wote ni sawa, maneno hayo manne ni falsafa ya azimio la Arusha.

Unaposema Binadamu wote ni sawa unamanisha nini?

1. Huwezi kukubali kuwa na ubaguzi kati ya binadamu na bindamu, iwe rangi, jinsia, dini au mahali wapotokea.

2. Kam binadamu wote ni sawa huwezi kuwa na binadamu mmoja anamnyonya binadamu mwenzake na huwezi kuwa na matabaka, tabaka moja linalinyonya tabaka lingine na huwezi kuwa na jamii ya wavuja jasho na wachuma jasho.

3. Kila binadamu ana uhuru w akujiamulia mambo yake mwenyewe, huwezi kuwa na jamii kikundi kimoja kinfanya maamusi na kikundi kingine kinatekeleza maamuzi.
 
Anasema turudi kwenye imani ya mwana Tanu.
1) Binadamu wote ni sawa
 
Matabaka ya wakulima na wafanyakazi ndio msingi wa maendeleo, sio wawekezaji HAPANA; na maendeleo yawe kwa ajili ya wao kwa manufaa yao.

So development is for them and for their development. Chama chenye itikadi ya kijamaa kiwe chama cha wakulima na wafanyakazi hivyo wanachama wake wawe wakulima na wafanyakazi na viongozi wake wawe wakulima na wafanyakazi.

My Take: Wafanyabiashara hawaingii katika chama cha kijamaa?
 
Back
Top Bottom