Kongamano la Azimio la Arusha

Hivi Mdahalo huu na ile miwili ya katiba imeratibiwa na taasisimoja? maana wadau wachangiaji waliokuwepo kwenye ile midahalo iliyopita sijawaona hususan wale wa vyama pinzani na CCM. lakini ajabu leo hata Nape amekuwepo japo kulingana na kijana kiongozi wa mdahalo anasema hakuna mtu aliyepewa mwaliko rasmi. kweli wazee wote akina Butiku wamekuja hapo bila mwaliko rasmi! tena wakawa wachangiaji wazuri vile! this is so interesting. Lisije likawa ni Gamba linajaribu kufunika nguvu ya midahalo iliyopita.

Achana na issue za gamba is not logic

Ni kweli kwanza liliandaliwa ka haraka na chanzo au sababu ni ubishani kwenye panel moja ikapelekea hili kongamano.

makongamano yajayo tutajitahidi yawe na mialiko ya watu wote, lakini lengo ilikuwa kupata data fulani na mawazo ya watu wasiosikika sana

Prof Shivji anaamini kwenye AA

Personally siamini kwenye AA naamini kwenye sheria, na hoja kubwa ni kuwa hata kama AA itakuja tena, kama kuna viongozi dhaifu
wa kutosimamia litakuwa halina maana.

There willbe about 4 makomgamano ni mjadala wa kitaifa zaidi na unaoeleka kwenye capacity building hata ya vyama vya siasa ambavyo , vinaonekana havina think tanker wa kukaa chini na kudadavua mifumo yetu na matatizo yake, nadhani kwa mfano kuna sehemu prof kagusia ufisadi ni mfumo.. nakubaliana naye kwa asilimia 100! bila kujua na kutoa solutiona tutajaza majina kila siku ya wezi wa nchi hii na mwisho tutajistukia tunajitaja! though in politics anything is allowed! sasa tutofautishe siasa na hali halisi

Kudhihirisha kuwa tunajisahau sana kuwaza juu ya taifa letu, sisi wote regardless uko wapi na unafanya nini, kujadili AA na bila mbadala kwa zaidi ya miaka 25 ndiyo indicator kuwa taifa limelala. Nyerere aliwaza na akafanya kwa taifa lake , awe alifail au kufaulu he played is remarkable role...je sisi tunafanya nini??
 
nakubaliana na wewe shvji,lwaitama,na hayat prof haroub wao waumin wa AA,pia walimu wa idara ya historia pale udsm.......
Lakin yote kwa yote tunahitaji kuwa na taifa lenye viongozi wenye utashi wa kuongoza
 
Azimio la Arusha, lilikuwa ni azimio la misingi ya utu. Pamoja na mambo mengine, lilikuwa linasema hivi: ukitaka kulinda utu wako, heshima yako kama binadamu, jitegemee, ndio kusema, tumia raslimali zako na nguvu zako, na akili zako kujiendeleza. Usiwe kupe. Omba msaada pale tu unapoona huwezi kabisa. Lakini kwenye thread nyingine kuhusu AA nimeshangazwa kuona baadhi ya wana JF wakilikejeli Azimio hilo, wengine wakimlaumu Mwalimu eti kalilazimisha, na wengine wakilalamikia jitihada za Prof. Shivji kuzua mjadala huo ili yale mazuri yake tuyaweke kwenye katiba mpya. Ndugu zangu, mtu ni utu, ndivyo tulisema wakati wa AA, na sidhani maana hiyo imebadilika sasa eti kwa kuwa tuna wafadhili. Tunajidanganya.
 
I have problem na wananchi kujadili vitu visivyo relevant na major challenges za Taifa. What's Azimio la Arusha? What's benefit Azimio la Arusha to regular Tanzanians? The problem of discussing ccm failed policies and force people to discuss their issues we never take the country anywhere. Constitution of Tanzania has nothing to do with Azimio la Arusha and please people focus on Stronger Constitution to benefit all not ccm. Tuna matatizo mengi yanatokana na hizi siasa na sera za ccm na hakuna mtanzania asiejua loop holes za hii serikali na jinsi wanavyotaka kuzilinda ili watutawala na vijikuu vyao. I am not going to stand for that.
 
Azimio la Arusha, lilikuwa ni azimio la misingi ya utu. Pamoja na mambo mengine, lilikuwa linasema hivi: ukitaka kulinda utu wako, heshima yako kama binadamu, jitegemee, ndio kusema, tumia raslimali zako na nguvu zako, na akili zako kujiendeleza. Usiwe kupe. Omba msaada pale tu unapoona huwezi kabisa. Lakini kwenye thread nyingine kuhusu AA nimeshangazwa kuona baadhi ya wana JF wakilikejeli Azimio hilo, wengine wakimlaumu Mwalimu eti kalilazimisha, na wengine wakilalamikia jitihada za Prof. Shivji kuzua mjadala huo ili yale mazuri yake tuyaweke kwenye katiba mpya. Ndugu zangu, mtu ni utu, ndivyo tulisema wakati wa AA, na sidhani maana hiyo imebadilika sasa eti kwa kuwa tuna wafadhili. Tunajidanganya.

Mtandu;

Uasili wa mwanadamu hatabadilika milele!

Mtu anayepinga Utu wake anataka uasili wake uwe ni upi? Mnyama?

Uasili wa Mtu ni Utu ..unaomtofautisha na viumbe wengine wote ulimwenguni. Kuusaliti utu kunamfanya mwandamu awe kiumbe chenye mahangaiko kuliko kimbe kingine ulimwenguni... Kwa kuwa wanyama na mimea ni viumbe ambavyo havina fursa ya kuukana uasali wake ..mara zote vimekuwa kwnye mafanikio na maisha bora.

Mwanadamu peke yake ndiye mwenye uwezo wa kuukana na kuutilishaka uasili wake ambao ndio utu wake ...Its a shame!!

Kwa mtizamo huo basi ndio maana kuna haja ya Kuwa na maazimio ya kuulinda, kuurutubisha na kuujenga utu wa mtu kwenye kila mfumo wa jamii huru...

Utu kwenye tiba ..

Utu kwnye siasa...

Utu kwneye uazalishaji...

utu kwenye kilimo...

utu kwnye malezi... nk

Huu ndio msingi wa azimio la arusha...

Utu haupitwi na wakati... Nani amekumabia UN, World Bank nk wanahaki ya kuupangia uasili wako... Utu wa Taifa la tanzania hauna uhusiano wowote na vyombo vya kimataifa..utu ni utu ..ni kitu huru!!

Bila utu ..Rasilimali zote zinageuka kuwa misingi ya vita, magonjwa, umasikini , ufisadi nk nani bado haoni umuhimu wa Maazimio na misingi ya utu kwenye taifa letu?

Hata ukiwa na Mitaji na fedha kiasi gani bila kuwa na utu Faida zote hizo ni sawa na silaha za maangamizi ..wakati wowote zitasababisha vita, majanga, vifo nk...Msingi wa maendeleo ni utu wa mtu kusimamamia mitaji na rasilimali zote za Tiafa ...TUAMKE!!
 
Achana na issue za gamba is not logic

Ni kweli kwanza liliandaliwa ka haraka na chanzo au sababu ni ubishani kwenye panel moja ikapelekea hili kongamano.

makongamano yajayo tutajitahidi yawe na mialiko ya watu wote, lakini lengo ilikuwa kupata data fulani na mawazo ya watu wasiosikika sana

Prof Shivji anaamini kwenye AA

Personally siamini kwenye AA naamini kwenye sheria, na hoja kubwa ni kuwa hata kama AA itakuja tena, kama kuna viongozi dhaifu
wa kutosimamia litakuwa halina maana
.

There willbe about 4 makomgamano ni mjadala wa kitaifa zaidi na unaoeleka kwenye capacity building hata ya vyama vya siasa ambavyo , vinaonekana havina think tanker wa kukaa chini na kudadavua mifumo yetu na matatizo yake, nadhani kwa mfano kuna sehemu prof kagusia ufisadi ni mfumo.. nakubaliana naye kwa asilimia 100! bila kujua na kutoa solutiona tutajaza majina kila siku ya wezi wa nchi hii na mwisho tutajistukia tunajitaja! though in politics anything is allowed! sasa tutofautishe siasa na hali halisi

Kudhihirisha kuwa tunajisahau sana kuwaza juu ya taifa letu, sisi wote regardless uko wapi na unafanya nini, kujadili AA na bila mbadala kwa zaidi ya miaka 25 ndiyo indicator kuwa taifa limelala. Nyerere aliwaza na akafanya kwa taifa lake , awe alifail au kufaulu he played is remarkable role...je sisi tunafanya nini??
Hapo kwenye nyekundu,sheria za nchi hutokana na katiba ya nchi.AA haikuwa incorporated kwenye katiba yetu kama watu wengi walivyotaka,especially when it comes to government leaders/workers.Hii ndiyo tunatakiwa kuifanyia kazi!!
 
Nilichojifunza kutokana na mdahalo wa jana ni kuwa Azimio la Arusha lilikuwa icorporated kweny katiba/sheria za chama,CCM na ni kweli sio kwenye katiba. Ndio maana hasa baada ya mabadiliko kutokea AA likawa halina nguvu kuwaguide wafanyakazi wa serikali, likawa linawabind wale wa chamani tu
 
Niweze,
Sir/madame
The discussion about the AD, initiated by Prof Shivji and the University of Dar-es-Salaam, is relevant to the challenges we face as a people and as a nation. If you are a careful observer of the Tanzanian scene and have spent some time educating yourself about the policies enshrined in the AD, you will no doubt realize that almost all the problems you want the new constitution to address, are partly due to the abandonment of the AD, which by extension, is the abandonment of our humanity as Tanzanians, and as Africans. Hayo matatizo mengi tuliyo nayo, yanatokana na sisi watanzania, na CCM hasa, kutuaminisha kwamba tutakuwa watu bora zaidi kama tutadharau misingi ya utu! Kwa karibu miongo mitatu tumedharau utu wetu, sasa tunavuna matunda yake...
 
Azimio Jipya, sir,
ukizaliwa binadamu utaendelea tu kuwa binadamu hata kama ukichinja watu milioni sita kama Hitler alivyofanya wakati wa vita kuu ya pili ya dunia. Lakini tulio wengi tunapata shida kuamini kwamba matendo ya Hitler, au wengine ambao matendo yao yanawatesa binadamu wengine, ni matendo ya ki-utu. Na kwa kweli nakubaliana na wewe kabisa kwamba tunahitaji matendo ya utu kwenye nyanja nyingi za maisha yetu kama taifa. Tunataka ukiugua, wauguzi hospitali watujali. Tunataka utu kwenye maeneo mengine hayo uliyo yataja. Azimio la Arusha, lilikuwa ni jitihada za makusudi kabisa kujenga tunu za utu. Kwa hiyo sijui tunatofautiana wapi.
 
It was a good post! Labda tu sikuanza hivyo!!

Niliandika kungana na wewe!!
 
Nilichojifunza kutokana na mdahalo wa jana ni kuwa Azimio la Arusha lilikuwa icorporated kweny katiba/sheria za chama,CCM na ni kweli sio kwenye katiba. Ndio maana hasa baada ya mabadiliko kutokea AA likawa halina nguvu kuwaguide wafanyakazi wa serikali, likawa linawabind wale wa chamani tu

Ndio Maana mdahalo huo ukawa na wachangiaji wana CCM, Pamoja na mdau kujitetea hapo juu kuwa uliandaliwa shaa shaa ndio maana hawakualika watu mimi naona kama ni kujitetea kusiko mantiki. huwezi kuandaa kitu kikubwa kama hicho kwa mtindo wa kukurupuka. Tunaomba hata hiyo mingine ijayo msifanye makosa kama hayo tena. Kwa sababu hilo AA lilikuwa kichama zaidi ndio maana kulikuwa hakuna haja ya wasikokuwa wana CCM au wenye mrengo wa CCM kulishabikia.

Leo wanataka kuleta ushawishi liingizwe kwenye katiba wakati likiwa kwenye chama walishindwa kulisimamia. Likija kwenye taifa je?

To hell with AA we dont need it.
 
Wakuu zangu,
Swala la Azimio la Arusha ni hoja ya chama CCM na wao ndio wanatakiwa kuijadili, labda tu ikiwa kongamano hili halihusiani na itikadi..Na maadam sasa hivi nchi yetu tunafuata mfumo wa vyama vingi kongamano hili linatakiwa liwe ktk kutazama Azimio la Arusha kama ni itikadi inayokubaliwa kutokubaliwa kwa maana kwamba ni siasa ya Kijamaa yenye mtazamo wa kushoto. Hivyo tunabishana ktk kujenga hoja za mazuri na mabaya ya itikadi hii.

Lakini kujadili Azimio la Arusha kwa matakwa ya kurudisha Miiko na maadili ya Viongozi, huu ni upotoshaji kwa sababu miiko na maadili sii swala la kiitikadi bali ni swala la kikatiba lenye lengo la kuimarisha uongozi bora na halina upande wowote wa kisiasa..Hivyo ni makosa makubwa ktk dunia hii ya leo kuhusisha Azimio la Arusha au Ujamaa na Kujitegemea kama ndio dira ya Kitaifa na inajadiliwa kwa malengo ya kulirudishwa Kikatiba.

Kama huu ndio msimamo wa chama CCM na waumini wake itaeleweka, sii watu wote wanaokubaliana na itikadi hii pamoja na kwamba yapo mazuri yake ambayo yaliondolewa na Azimio la Zanzibar ktk mazingira ya kutatanisha kwani maswala ya Ubaninafsishaji au maadili ya viongozi hayahusiani kabisa na itikadi wala mrengo wa chama chochote..

Kwa hiyo wakuu zangu, mimi nadhani ni muhimu zaidi kulizungumzia Azimio la Zanzibar ambalo lilingizwa kikatiba na limetuletea athari nyingi sana hasa ktk uzalendo wa viongozi na wananchi kwa ujumla. Marekebisho yafanyike ndani ya katiba kuziba nyufa zote za mirija inayotokana na Azimio la Zanzibar..hili ndio tatizo la nchi yetu na ndio mbegu iliyopandikizwa na wanaCCM ili tupate Mafisadi.

Kinyume cha hapo vyama vya kisiasa ndivyo vyenye jukumu la kuyakubali baadhi ya mambo mazuri ya Azimio la Arusha (itikadi)hivyo kuunda sera zinazozingatia mwongozo huu. Hivyo basi Azimio la Arusha ni mtazamo wa kifkra wa kiCCM na wafuasi wake ndio wanaotakiwa kujadili ktk kujivua magamba, lakini kama swala zito hasa linalopelekea kujadili Azimio la Arusha ni miiko na Maadili basi hatuna sababu kabisa ya kujadili Azimio la Arusha lililounda siasa ya Ujamaa na Kujitegemea. Nina hakika kabisa sehemu kubwa ya Watanzania hawakubaliani na Azimio la Arusha kama mrengo wa kushoto, ingawa yapo mazuri ambayo yanakubalika kwa sababu hayahusiani kabisa na itikadi.
 
Mkandara;

Kama nakupta vizuri , umetenganisha kati ya Itikadi ya azimio la arusha na kanuni ya MIIKO NA MAADILI!

Umesema Itikadi tuwaachie CCM

na

Miiko na Maadili liwe swala la kitaifa!

Naona ni mtizamo ambao unao weza kuwa mzuri ... kwenye mijadala inayoendelea sasa nchini.

Lakini kimsingi nini haswa ni tofauti kati ya hali hizo mbili ...? Itikadi na Miiko/maadili
 
Back
Top Bottom