Bernadi James mwanafunzi wa UDSM,anasema kabla ya kurudisha azimio la Arusha ni lazima kwanza tuvunje azimio la Zanzibar.....anakumbusha ubinafsishaji wa nyumba za serikali ambao ni matokeo ya azimio za Zanzbr
Shifji anaanza kuchambua tofauti ya viongozi na watawala....anasema Azimio halikuzungumzia kuhusu utawala bora, dhana hii ilitolewa na World bnk, anasema azimio linazungumzia uongozi bora na liloiweka muongozo ili viongozi wasijegeuka watawala
Shivji: katiba ya mwaka 77 bado inataja ujamaa na kujitegemea na uliweka miiko ya uongozi, baada ya kukubali uliberali neno ujamaa na kujitemgemea halikuondolewa ila neno ujamaa na kujitegemea lilikuwa defined
Defn ya sasa mbona haijinyambulishi, na huwezi elewa maana halisi?
Nimeshaisoma, haieleweki, huwezi kuona mjamaa na mbepari. Almost wote ni Wajamaa....
Shivji;
Mwalimu alisema alikuwa anaomba Mungu kusiwe na vyama vingi kwa idadi bali viwe viwili kama Marekani, na vyote viwe na msingi wa ujamaa, ila viwe vinatofautiana kwa namna ya kuitekeleza
Shivji:
Vyama vyote vya siasa lengo lao ni kuingia madarakani, na kwa njia hii wanaweza kutumia njia yoyote ili kuingia madarakani. Kwa hiyo tusitegemee kama vinaweza kubadilisha mfumo wa jamii iliyo kubwa.
Ibrahim Kaduma;
Lengo la miiko lilikuwa ni kujenga maadili ya kijamaa, kwa hiyo maadili yanafundishika.
Anachallenge point ya Shivji kuwa maadili hayafundishiki.
Kaduma;
Kulipokuwa na tatizo kama la Shinyanga wafungwa kufa mawaziri waliwajibika, wafungwa walipotoroka Ukonga mawaziri na makamishna wa magereza walijiuzuru.
MY take: Mbona Mbagala na Gongo la Mboto hakuna aliyewajibika?
Kaduma:
Maadili yanaanzia mahali, unatekeleza kitu fulani then ndo inakuwa tabia ya taifa. Anakumbusha jinsi Mwinyi alipojiuzulu wakati ule wafungwa walivyokufa na pia yule waziri aliyejiuzulu wakati wafungwa walipotoroka gereza la ukonga.
Shivji: Ngombaremwilu ndiye ayetoa hoja kuwa wafanyabiashara wanaweza kuwa wanachama wa CCM hii ilikuwa ni enzi ya kipindi cha mzee ruksa, kabla ya hapo CCM ilikuwa ikifahamika kwa ajii ya wakulima na wafanyakazi
AA halikuuliwa pale Zanziba na Azimio la Zanzibar, bali na hotuba ya Kingunge Ngombale Mwiru pale Chimwaga pale Dodoma. Na huo ukawa ndio mwanzo wa mafisadi kuingia katika chama na ndio mwanzo wa Kingunge mwenyewe kubadilika kuwa fisadi naye na kusahau misingi ya AA.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.