Komodo dragon ndio mnyama hatari zaidi kuliko Black mamba (koboko), Simba, Mamba, Tiger na wanyama wengine wa aina hiyo

Ni mnyama coward na mviziaji. Anachofanya anavizia ukiwa huna hili wala lile, anakung'ata halafu anakimbia kama kafumaniwa usije mdhuru, anakuacha akisubiri sumu isambae mwilini udondoke aanze kunusa nusa ulipopita ndo ale nyama ya mwili wako. Hata hivyo huwa anamuavoid binadamu.
View attachment 2321528
Mkuu Tsh , kila mnyama hapa duniani hukamata windo lake kwa timing. Hata Tiger, Simba, Mamba, Chatu na wengine wa aina hiyo huvizia pale muwindwa anapokuwa hana hili wala lile na kumvamia ghafla (ambush) kisha kuanza kumshambulia na hatimae kummaliza.

Kuhusu kuavoid binadamu huu ni uwezo tuliopewa binadam dhidi ya wanyama wote wakali na wapole kama tunavyoona pichani.
 

Attachments

  • images (15).jpeg
    images (15).jpeg
    27 KB · Views: 8
  • images (21).jpeg
    images (21).jpeg
    52.9 KB · Views: 8
Habari zenu wana JF wenzangu.

Leo nimekuja na mada inayohusu mnyama hatari kuliko wanyama wote duniani anaitwa Komodo dragon.

Mnyama huyu ana uwezo wa kuua wanyama wengine hatari kama vile
1) Tiger
2) Simba
3) Leopard, Cheetah (chui)
4) Mamba
5) King cobra, Black mamba nk.
6) Honey badger pamoja na uwezo wa kuishi karibu na wanyama wakali, lakini hawezi kufanya mzaha huo mbele ya Komodo dragon aisee atamezwa yeye na manyoa yake. Jamaa hana masihara na mnyama mwingine yoyote.

Komodo dragon ana venom (sumu kali) kuliko mnyama yoyote hapa duniani. Akiuma mara moja tu inatosha kumaliza mchezo. Hata iwe Tembo, kifaru, kiboko, simba nk hawawezi kufikisha dakika 5 bila kuanguka chini na kupararaizi, kisha Komodo anajivuta taratibu kuja kula nyama.

Haijalishi hapo mnyama atakuwa ameshakufa au bado anapumua, Komodo atachofanya ni kuanza kumtafuna mzima mzima huku anayetafunwa anamuona. Kwa vile atakuwa ameshapararaizi basi mshambuliwa hatokuwa na nguvu ya kumfanya chochote Komodo.

Mnyama huyu hata sumu ya koboko haimdhuru kutokana na aina ya uumbwaji wake ulivyo, ila yeye ya kwake inamdhuru koboko kwa sekunde tu, kwanza anaweza kummeza kwa sekundi 10 bila hata kutumia venom (sumu) yake.

Kwa upande wa binadam sometimes unaweza kuumwa na Simba, Tiger, Leopard, Mamba nk ila ukawa jasiri na kufanikiwa kujiokoa na kutoka nduki kuokoa maisha yako.

Ila mzee Komodo yeye akishakupiga jino basi ujue ni bye bye maana kama ukibahatika sana itachukua ni dakika 3 au 5 kuiaga dunia na pengine mzee wa kazi atakuja akutafune ukiwa bado hujafa hadi atakumaliza na kukumeza wewe wote.

Huyu mnyama akishakupiga jino hukaa pembeni umbali kidogo wa ulipo halafu anakusikilizia. So unaweza kutoka nduki ukidhani umepona kumbe dakika mbili au tatu za mbele utaanguka na kuanza kuishiwa nguvu, hapo ndo mzee wa kazi ataanza kukufuata huku akitumia pua yake kunusa kila sehemu uliyokanyaga hadi atakukuta ukiwa hoi na yeye au wao wakumalizie kabisa.

Huyo ndio Komodo dragon mbabe wa wababe wote duniani. Japo wengi huku Afrika hawamjui kutokana na wanyama hao kupatikana zaidi katika bara la Asia.

View attachment 2321342View attachment 2321345
Akijitokeza kwa Hadzabe huku Lake Eyasi analiwa na sumu yake tena msosi fresh kabisa
 
Blank mamba ndio hatari ndani ya dakika umeshapotea
Black mamba ni hatari kwa binadam tu, ila kuna baadhi ya viumbe mfano wale aina ya nguchiro huwa wanamtafuna black mamba vizuri, ila hili dubwasha linaweza kumtafuna huyo nguchiro na black mamba wake kwa pamoj na hakuna madhara yoyote linalalopata zaidi ya kushiba na kutafuta mahali pa kujipumzisha tu.
 
Kuna documentary Moja nilisoma,

Kwamba sehemu nzur na salama ya kukimbilia endapo zile movie hollywood za mazombie zitakuja kua kweli

Kua Ni comodo island,
Kisiwa wanakolatikana comodo dragons

Kwamba wao mizoga kama mazobi ndo sukari yao, mazombi yote yataliwa na Dunia itabaki salama
 
Huyu mnyama akihakikisha amekuchubua na meno yake, basi anakuacha na kusepa. Anajua tu muda si mrefu utapoteza fahamu au kufa kabisa then anakurudia kukumaliza kabisa.
Na anaweza kula windo lake likiwa hai kabisa (alive)
 
Kuna documentary Moja nilisoma,

Kwamba sehemu nzur na salama ya kukimbilia endapo zile movie hollywood za mazombie zitakuja kua kweli

Kua Ni comodo island,
Kisiwa wanakolatikana comodo dragons

Kwamba wao mizoga kama mazobi ndo sukari yao, mazombi yote yataliwa na Dunia itabaki salama
Aisee hiyo documentary ni nzuri sana mkuu 😂😂😂🤣🤣
 
Huyu mnyama akihakikisha amekuchubua na meno yake, basi anakuacha na kusepa. Anajua tu muda si mrefu utapoteza fahamu au kufa kabisa then anakurudia kukumaliza kabisa.
Na anaweza kula windo lake likiwa hai kabisa (alive)
Hivyo hivyo wala hujakosea mkuu. Ubarikiwe sana kwa ufafanuzi wako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom