Komodo dragon ndio mnyama hatari zaidi kuliko Black mamba (koboko), Simba, Mamba, Tiger na wanyama wengine wa aina hiyo

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
6,860
12,293
Habari zenu wana JF wenzangu.

Leo nimekuja na mada inayohusu mnyama hatari kuliko wanyama wote duniani anaitwa Komodo dragon.

Mnyama huyu ana uwezo wa kuua wanyama wengine hatari kama vile
1) Tiger
2) Simba
3) Leopard, Cheetah (chui)
4) Mamba
5) King cobra, Black mamba nk.
6) Honey badger pamoja na kuwa na uwezo wa kuishi karibu na wanyama wakali, lakini hawezi kufanya mzaha huo mbele ya Komodo dragon, aisee atamezwa yeye na manyoa yake yote 😂🤣🤣🤣. Jamaa hana masihara, huruma, wala mzaha na mnyama mwingine yoyote.

Komodo dragon ana venom (sumu kali) kuliko mnyama yoyote hapa duniani. Akiuma mara moja tu inatosha kumaliza mchezo. Hata iwe Tembo, kifaru, kiboko, simba nk hawawezi kusavaivu bila kuanguka chini na kupararaizi, kisha Komodo anajivuta taratibu kuja kula nyama.

Haijalishi hapo mnyama atakuwa ameshakufa au bado anapumua, Komodo atachofanya ni kuanza kumtafuna mzima mzima huku anayetafunwa anamuona. Kwa vile atakuwa ameshapararaizi basi mshambuliwa hatokuwa na nguvu ya kumfanya chochote Komodo.

Mnyama huyu hata sumu ya koboko haimdhuru kutokana na aina ya uumbwaji wake ulivyo, ila yeye ya kwake inamdhuru koboko kwa sekunde tu, kwanza anaweza kummeza kwa sekundi 10 bila hata kutumia venom (sumu) yake. Anamtafuna black mamba kama mtu anavyotafuna tambi.

Kwa upande wa binadam sometimes unaweza kuumwa na Simba, Tiger, Leopard, Mamba nk ila ukawa jasiri na kufanikiwa kujiokoa na kutoka nduki kuokoa maisha yako.

Ila mzee Komodo yeye akishakupiga jino basi ujue ni bye bye maana kama ukibahatika sana itachukua ni dakika 3 au 5 kuiaga dunia na pengine mzee wa kazi atakuja akutafune ukiwa bado hujafa hadi atakumaliza na kukumeza wewe wote.

Huyu mnyama akishakupiga jino hukaa pembeni umbali kidogo wa ulipo halafu anakusikilizia. So unaweza kutoka nduki ukidhani umepona kumbe dakika mbili au tatu za mbele utaanguka na kuanza kuishiwa nguvu, hapo ndo mzee wa kazi ataanza kukufuata huku akitumia ulimi wake kunusa kila sehemu uliyokanyaga hadi atakukuta ukiwa hoi na yeye au wao wakumalizie kabisa.

Huyo ndio Komodo dragon mbabe wa wababe wote duniani. Japo wengi huku Afrika hawamjui kutokana na wanyama hao kupatikana zaidi katika bara la Asia.

Wataalam wa wanyama washakiri wazi kuwa hata king of the jungle Simba mwenyewe hawezi kuweka mguu maeneo ya hawa viumbe.

images (14).jpeg
Screenshot_20220811-232426.jpg
 

Attachments

  • Screenshot_20220816-095112.jpg
    Screenshot_20220816-095112.jpg
    37.1 KB · Views: 39
Kuna video 1(Nat Geo) nilimuonaga huyo jamaa,alimng'ata kidogo tu yule ng'ombe wa porini na ng'ombe akafanikiwa kukimbia Ila hakufika mbali akadondoka, nyingine alimng'ata swala nae hakuchukua round.
Yani huyu akishang'ata tu kazi imekwisha. Unaweza kusavaivu tu zile dakika 2 za mwanzo. Baada ya hapo wewe ni kitoweo chake. Haijalishi umeshakufa au bado, utaliwa tu kiubabe. Farasi na ukubwa wake wote, alipigwa jino moja tu. Baada ya dakika tatu akaanza kuliwa nyama huku anajiona.
 
Venom yake ni fatal! Japo haiui kwa haraka kama usemavyo
Bora umemrekebisha mkuu. It takes time kuweza kuua,na inachofanya inazuia pia damu kuganda hivyo mnyama atableed sana.

Yeye akishauma tu, na mate kuingia kwenye kidonda cha muhusika basi humfuatilia huyo mnyama mpaka atakapopata nafasi ya kuanza kumla. Zipo documentary Nat Geo zinazo muhusu.
 
Bora umemrekebisha mkuu. It takes time kuweza kuua,na inachofanya inazuia pia damu kuganda hivyo mnyama atableed sana.

Yeye akishauma tu, na mate kuingia kwenye kidonda cha muhusika basi humfuatilia huyo mnyama mpaka atakapopata nafasi ya kuanza kumla. Zipo documentary Nat Geo zinazo muhusu.
Bora ukimbilie ndani ya chombo 😂😂😂 sio kuliwa huku unajiona
 
Huyu mdusu haangaiki kukupiga jino kwanza ana kupa kia lake 1 tu unakuwa FINYANGO FINYANGO,halafu anaweza akakuacha na hutoboi lazima uondoke si kiumbe mzuri
Hahahaha ya huyu ni mnyama hatari zaidi kuliko uhatari wa mnyama yeyote. Kwanz mnyama yoyote akijaribu tu kumjeruhi kwa mdomo basi ataanza kwanz kufa yeye kwa sumu ya hili dubwasha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom