Jamani tulishawahi kuujadili vyakutosha huko nyuma kuhusiana na waraka huu. Huyu mzee anajua tofauti kati ya waraka na ilani. Lakini kwa makusudi kabisa anaamua kutumia neno "ILANI" mahali pa "WARAKA" ili kuwapumbaza watu kuwa kanisa linaandaa ilani (manifesto) itakayofuatwa na vyama vya siasa kwenye uchaguzi ujao. Huu ni opotoshaji mkubwa ambao watu wenye mawazo na mtizamo chanya wanapaswa kumkemea huyu babu. Iweje watu waelekezwe namna ya kuchagua miongoni mwetu viongozi waadilifu iwe ni kuchochea udini? Au ni kwa namna gani watu wakumbushwe jinsi ya kujali utu na rasilimali za taifa iwe ni ubaguzi? Ni kwanini huyu mzee hataki kuonyesha kwenye huo waraka mahali ama vipengele vinavyohashiria udini ama machafuko katika jamii? Nafikiri kuna sababu ya kumpuuza kwa kukaa kimya kwani pia hiyo ni adhabu tosha.
Mkuu, binafsi sihangaiki sana na title ya waraka - Manifesto au Ilani - bali content. Swali: Je, ni kweli hakuna hata kipaumbele kimoja katika waraka huo kinachotufaa Watanzania? Swali hili limekuwa lininisumbua sana! Pili, Prof Lipumba aliulaani sana huo waraka lakini Rev Mtikila alipowahamasisha wanakanisa wake wasipige kura 2010 aliunga mkono! Je, kweli akili zinatutosha sisi Watz?