Waraka unaelezea sifa za kiongozi,na kwa kuwa imani za dini husaidia watu kuwa na hofu ya Mungu itasaidia kupata watu wenye busara kutuongoza.Vyama vya siasa CCM ikiwa ni moja ya vyama vimekwenda nje ya utaratibu wa kupata viongozi,zamani afadhali sifa za kiongozi zilikuwa zikitazamwa ili kupata viongozi waadilifu,pia Mwalimu alikuwa anajitahidi kuwa mkali na wizi na ubadhirifu japokuwa nae alikuwa na mapungufu yake.Ni lazima viongozi wa dini waelimisha waumini sifa za viongozi kulingana na vitabu vitakatifu vinavyoeleza.Mzee Kingunge amalizane na suala la ubungo na atoe maelezo ya kuridhisha iweje yeye anayejiita mtu safi familia yake ihusishwe na madudu ya parking za magari na menejimenti ya ubungo bus terminal,pia mwanae anayejisifia anaishi kwenye nyumba ya dola milioni moja za kimarekani,je yeye kama mzazi hausiki na kuhusishwa na ufisadi huo?Tatizo la viongozi waliozoea kuishi kama miungu watu wakiambiwa ukweli wanakuwa wakali........