Kingunge amechanganyikiwa?

Amechanganyikiwa haswa! Nilidhani atazungumzia mapungufu wa Waraka, kitu ambacho hakukufanya kabisa. Haitoshi kusema dini isichanganywe na siasa. Mbona mara nyingi katika matukio mbalimbali wanasiasa hukaribisha viongozi wa dini wawaombee?
 
TUNACHOTAKIWA Watanzania wote kwa pamoja ni kuamua je, tunachotaka kuweka mbele ni UTANZANIA na UAFRIKA wetu au kabila, dini, rangi, jinsia, usomi, vyeo, kazi, mali au ukoo wetu ?

Kama tumeamua kumpa MUNGU kilicho cha Kaizari sawa!!!

Kama tumeamua kwamba mpanda fahali wawili hawezi kupasuka msamba basi tuendelee na kupanda fahali wawili!

Kama tumeamua kwamba kujenga ufa ni kwa kuongeza ufa mwingine tufanye hivyo!

Kama tumeamua kwamba gauni au suruali mpya hupatikana kwa kushona kiraka juu ya kraka tuendelee vivyo hivyo!

Kama tumeamua kwamba akumulikaye mchana usiku hatakuchoma bali atakumwagia maji ya baridi kwanini tuogope maji ya baridi?

Kama akili ni nywele na kila askofu na sheikh ana mvi na sio nywele nyeusi na tumezipenda mvi zisizo na hekima wala busara kwanini tusizipende!!!

Kama tunadhani fataki hawezi kuwepo kwenye majengo ya makanisa na misikiti tuendelee kuruhusu hata wenda nusu uchi kuja kuswali.

Kama hatujui asiyekutaka au anayekutakia baya hawezi kukwambia toka au hawezi bayana bin bayana kukulaani ngoja asubihi ipishe mchana na jioni ipishe usiku.
Duh! Mbunge kwa mistari umenikuna. Nakufananisha na wabunge wenzako akina Shibuda na Mudhihiri! Ni hayo tu!
 
Niliwahi kuwaambia mkasome kitabu kinaitwa the root of all evil. Kama hamjui vita vingi vya wenyewe kwa wenyewe vina mkono wa Roman Catholic Church na sasa Tanzania ndipo inapolekea nyie subirini. Kingunge analosema ni kweli na hajakosea hata kidogo tunahitaji watu wenye ushupavu kama huo kunyooshea kidole Tabia kama hii.

Na tukiiachie Tanzania inaelekea katika vita vya wenyewe kwa wenyewe

Nadhani unataka kumaanisha vita vingi vilivyowahi kutokea karne nyingi zilizopita, vilisababishwa na uenezaji wa dini. Maana tunajua pia kuwa dini nyingi zilienezwa kwa nguvu sana, si ukristo peke yake.

Hakuna vita yoyote inaloweza kusababishwa na Catholic church kutikana na waraka wao huo. Wasiwasi unaowakumba wanasiasa unatokana na uzito wa hoja zilizomo kwenye waraka inayozungumziwa. Wanasiasa wanajua kuwa watanzania ni waoga wa machafuko na pia, waraka huo unawaumbua sana. Wametumia woga huo kushinda chaguzi nyingi za miaka ya nyuma zilizohusisha vyama vingi vya siasa. Wanataka tuamini pia kuwa, waraka huo unaoainisha mapungufu ya kiuongozi nchini ni ya kidini, ya kundi dogo la watu na yenye nia ya machafuko. Mbona hawasemi ni kwa jinsi gani machafuko yanaweza kutokea endapo watu watatii yaliyoandikwa kwenye waraka huo?

Nadhani umefika wakati wa kuchambua content zaidi ya mtoaji wa content hizo.
 
Mimi nadhani tumsaidie mzee wetu huyu kwa kumshauri astaafu; kwa kweli hali aliyofikia sasa ni ile ya kukaa nursing home au kupata palliative care tu!!!

Lazima akubali kwamba kila jambo na wakati wake, na kila binadamu ana life span... is has already passed the productive stage na sasa anaelekea destructive stage

I still dont know why media inaendelea kumpa nafasi wakati wakijua wazi kwamba inaweza kuwa counter-productive kwa kingunge na CCM


Kazee haka hakawezi kukubali. Sasa hivi hakana hoja kabisa, kama mtu anapinga waraka wa katoliki maana yake anatetea mafisadi. Naona Kingunge baada ya Nyerere kufa anaonesha sura yake halisi.

Nashangaa sana wenzake wote rika yake wanaogopa kujitokeza mbele ya waandishi wa habari, sio kwa kuwa wanaogopa bali kwa kuwa wanataka wengine wenye nguvu wafanye kazi. Ni vema akitulia tukimhitaji tutamuomba atusaidie.
 
Kwa wale waliomsikiliza na kumuona Kingunge akiongea na waandishi wa habari jana bila shaka watakuwa na maoni tofauti kuhusu kikongwe huyu. Binafsi namuona kama mtu aliyeanza kuchanganyikiwa. Alikuwa anazungumzia Waraka wa Kanisa Katoliki lakini mpangilio wake wa maneno ni wa kushangaza na hauna mantiki. Mpaka sasa hajasema ni nini hasa anachoona yeye ni kibaya katika waraka huo unaohamasisha wananchi kuchagua viongozi waadilifu, zaidi ya kusisitiza kwamba utaigawa nchi.

Mwaka 1992, Maaskofu wa Kanisa Katoliki Malawi walitoa waraka kama huu wa kwetu - uliolenga kero za watu (kuboresha huduma za jamii, mgawanyo mzuri wa raslimali za nchi, umaskini, uhuru wa kutoa mawazo, haki za binadamu nk) - na kwa vile ilikuwa mara ya kwanza kupinga hadharani upungufu uliokuwepo katika utawala wa Dr Kamuzu Banda, maaskofu hao waliwekwa chini ya ulinzi na kuitwa wajieleze mbele ya Rais.

Hali ilikuwa tete sana na hata printing press iliyochapa waraka huo ilichomwa moto mara moja!

Wakati huohuo chama tawala (Malawi Congress Party - MCP) kilifanya mkutano wa siri namna ya ama kuwafukuza maaskofu hao nchini au kuwafanya wapotee wasionekane tena bila watu kujua wako wapi. Baadhi ya walikuwa viongozi wa Kanisa na wanachama wa MCP walikana dini hadharani kwa kusema maaskofu wamemdhalilisha Rais wao na hivyo wao wenyewe hawana sababu ya kuendelea kusali kwenye Kanisa ovu namna hiyo.

Maaksofu walitungiwa kila aina ya ubaya lakini kwa vile haki na ukweli husimama mpaka mwisho, wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka 1994, chama tawala MCP kilianguka vibaya sana na United Democtatic Front (UDF) kikawa madarakani. Baada ya Dr Banda kuangushwa maaskofu waliombwa wafungue kesi ya kutishiwa kuuawa na Dr Banda lakini walisema wameshamsamehe na hivyo kesi yake kufutwa.

Baada ya Dr Banda kufariki, viongozi waliokana dini hadharani walirudi tena kuomba radhi kanisani kwa kusema walichokisema hakikuwa kimetoka moyoni mwao bali ilikuwa kulinda maslahi yao ya kisiasa tu!

Tanzania tunaelekea kwenye njia ya namna hiyo na hakika haki na ukweli kuhusu waraka huo vitasimama hadi mwisho! Kama kweli nia ya waraka ni kumchagua Rais Mkatoliki au Mkristo au kuleta udini na kinachosemwa dhidi ya Kanisa Katoliki ndiyo kero halisi za Watanzania, basi mwisho wa yote Mungu mwenyewe ataamua ukweli uko wapi!
 
Ni uzee tu jamani unamsumbua . Tuwaombe tu waliyokaribu naye wamshauri apumbuzike sasa mambo ya siasa ili asiendelee kujiabisha. KWA USEMI WA SASA HIVI YEYE KESHAPITWA NA WAKATI
 
Jamani tulishawahi kuujadili vyakutosha huko nyuma kuhusiana na waraka huu. Huyu mzee anajua tofauti kati ya waraka na ilani. Lakini kwa makusudi kabisa anaamua kutumia neno "ILANI" mahali pa "WARAKA" ili kuwapumbaza watu kuwa kanisa linaandaa ilani (manifesto) itakayofuatwa na vyama vya siasa kwenye uchaguzi ujao. Huu ni opotoshaji mkubwa ambao watu wenye mawazo na mtizamo chanya wanapaswa kumkemea huyu babu. Iweje watu waelekezwe namna ya kuchagua miongoni mwetu viongozi waadilifu iwe ni kuchochea udini? Au ni kwa namna gani watu wakumbushwe jinsi ya kujali utu na rasilimali za taifa iwe ni ubaguzi? Ni kwanini huyu mzee hataki kuonyesha kwenye huo waraka mahali ama vipengele vinavyohashiria udini ama machafuko katika jamii? Nafikiri kuna sababu ya kumpuuza kwa kukaa kimya kwani pia hiyo ni adhabu tosha.
 
Kingunge alisema ni vizuri kanisa likaelewa kuwa lenyewe sio chama cha siasa na kwamba, halina uwezo wa kuandaa ilani ya uchaguzi.

Hivi ni kweli kuwa kanisa katoliki limetoa ilani ya uchaguzi? Nijuavyo mimi, ilani ya uchaguzi ni maelezo yanayotumiwa na vyama vya siasa vyenye lengo la kugombea uchaguzi ila kuelezea malengo/mipango/mikakati yao endapo vitapata ridhaa ya wananchi kuongoza na/au kuunda serikali. Siwezi kuhusisha waraka wa kanisa Katoliki na Ilani ya chama chochote. Ninavyojua ni kwamba, kanisa limeoa kitabu/waraka ambao unaelezea matarajio yao kwa uongozi wa nchi ambao ina amini kuwa yakifuatwa, yataleta ustaarabu, utulivu, haki na maisha mema kwa wananchi wote bila kujali imani zao, mahali wanapotokea wala itikadi zao. Hapo nadhani neno ilani limetumiwa ili kudhoofisha malengo ya maoni yaliyotolewa. Na hivyo neno ilani limetumika kurubuni na kudhoofisha jitihada zozote za kijamii kudai hali bora kwa watu wote. Ni kauli za kisiasa sana.

Alifafanua kwamba, wakati anazungumzia waraka huo bungeni hakuwa anataka uhasama na kanisa kwa kuwa anaheshimu imani, ila alikuwa akitoa angalizo kwa kuwa dini haiongozi nchi kama serikali.

Mzee Ngombale anayo haki kama ambavyo tunayo wengine wote ya kupendekeza, kutoa maoni na kuelezea hali halisi ya uongozi wa nchi yetu bila kuwa tumevunja sheria. Haki hii ni ya kikatiba. Hakuna mwenye mamlaka ya kumnyamazisha mtu kutumia haki hii.

Ni kweli kuwa hakuna shirika la kidini lolote linaloongoza nchi kama serikali. Ila mashirika hayo ya dini yanaongoza jamii kwa namna tofauti na ambazo ni kubwa na zisizofaa kudharauliwa. Dini zote nchini zina waumini wengi ambao ni watiifu kwao. Vile vile dini zote zinawajibu wa kutoa mafunzo/maelekezo kwa waumini wao ili waishi katika njia bora. Hayo yote ni maongozi.


Alisisitiza kuwa dini si chombo cha kuunganisha watu, bali kuwatenganisha ndiyo maana kila mtu ana dini yake, lakini serikali ni moja, hivyo nchi yenye dini nyingi haiwezi kuunganishwa na dini bali siasa.

Nadhani kauli yake hapo juu inataka kuanzisha mjadala mpya na mgumu ambao wala sidhani kama anauweza. Kusema kuwa kazi ya dini ni kutenganisha watu na sio kuwaunganisha, ni upotoshaji wa hali ya juu. Sijui shirika lolote la dini ambalo linafundisha waumini wake wasishirikiane na waumini wa mashirika mengine au wawachukulie waumini wa mashirika mengine ya kidini kuwa ni wabaya na wasiofaa katika jamii. Dini zote ninazozijua, zinawataka waumini wake wawe watu wapole, watiifu, wawe na upendo kwa wote na wamtii Muumba wao. Labda kama Mzee Ngombale Mwiru ana maana kuwa, anadhani kama ilivyokuwa kazi ya siasa, dini pia hutenganisha watu na sio kuwaunganisha na ndio maana tuna vyama vingi vya siasa, na chama kimoja chenye haki zaidi ya vingine. Tuna ushahidi wa kihistoria pia wa viongozi wa kisiasa wanaotaka wananchi na hata wafanya biashara wasijiunge na upinzani wakidai kuwa si watu wanaofaa.

Sidhani kama Mzee wetu huyu anataka kuendeza mjadala kama huu. Naamini kuwa hauwezi
kabisa mjadala mgumu na wahatari kama huu.
 
Mwaka 1992, Maaskofu wa Kanisa Katoliki Malawi walitoa waraka kama huu wa kwetu - uliolenga kero za watu (kuboresha huduma za jamii, mgawanyo mzuri wa raslimali za nchi, umaskini, uhuru wa kutoa mawazo, haki za binadamu nk) - na kwa vile ilikuwa mara ya kwanza kupinga hadharani upungufu uliokuwepo katika utawala wa Dr Kamuzu Banda, maaskofu hao waliwekwa chini ya ulinzi na kuitwa wajieleze mbele ya Rais.

Hali ilikuwa tete sana na hata printing press iliyochapa waraka huo ilichomwa moto mara moja!

Wakati huohuo chama tawala (Malawi Congress Party - MCP) kilifanya mkutano wa siri namna ya ama kuwafukuza maaskofu hao nchini au kuwafanya wapotee wasionekane tena bila watu kujua wako wapi. Baadhi ya walikuwa viongozi wa Kanisa na wanachama wa MCP walikana dini hadharani kwa kusema maaskofu wamemdhalilisha Rais wao na hivyo wao wenyewe hawana sababu ya kuendelea kusali kwenye Kanisa ovu namna hiyo.

Maaksofu walitungiwa kila aina ya ubaya lakini kwa vile haki na ukweli husimama mpaka mwisho, wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka 1994, chama tawala MCP kilianguka vibaya sana na United Democtatic Front (UDF) kikawa madarakani. Baada ya Dr Banda kuangushwa maaskofu waliombwa wafungue kesi ya kutishiwa kuuawa na Dr Banda lakini walisema wameshamsamehe na hivyo kesi yake kufutwa.

Baada ya Dr Banda kufariki, viongozi waliokana dini hadharani walirudi tena kuomba radhi kanisani kwa kusema walichokisema hakikuwa kimetoka moyoni mwao bali ilikuwa kulinda maslahi yao ya kisiasa tu!

Tanzania tunaelekea kwenye njia ya namna hiyo na hakika haki na ukweli kuhusu waraka huo vitasimama hadi mwisho! Kama kweli nia ya waraka ni kumchagua Rais Mkatoliki au Mkristo au kuleta udini na kinachosemwa dhidi ya Kanisa Katoliki ndiyo kero halisi za Watanzania, basi mwisho wa yote Mungu mwenyewe ataamua ukweli uko wapi!

Mkuu hapo nilikokoleza umesema maneno mazito sana. Kwangu yamesimama kama sala hivyo sina la kusema zaidi ya "AMEN".
 
Maaskofu wamuombee huyu Mpagani Kingunge ili aongoke. Naona ametawaliwa na nguvu za Shetani.
 
Wengi nadhani hamjamwelewa vyema huyu Kikongwe anamaanisha kuigawa nchi kati ya Mafisadi na Wazalendo. Ndio maana anapiga vita waraka unaopiga vita ufisadi usijeleta mgawanyiko huo.
 
mzee wangu umechoka,fikra zako ni za kichovu huna jipya na usipokuwa mwangalifu utajondolea heshma kubwa uliyo nayo mbele ya umma wa watanzania, kumbuka hizi ni zama za fikra hura kila mtu au taasisi ina haki yakutoa mawazo yake na nijuu ya watanzania kupima na kuamua,pia namshangaa huyu babu kwa kukataa waraka huu, je yeye ni nani hadi atuchagulie kipi chema kwetu? sisi umma ndio wenye maamuzi na sio wao wakio kaa madarakani miaka yote na sas wanaondoka na kuiacha nchi kwenye wimbi la umasikini, na sehemu kumbwa ya urithi wetu ukiwa mikononi mwa wageni na mafisadi wa chache. mimi nadhubutu kusema kuwa viongozi hao watakapo kufa vizazi vijavyo vitachimba makaburi yao na kutoa mabaki yao ili kupima kama walikuwa na akili timamu
 
Mimi nadhani ambaye hajamuelewa ni mbumbumbu aliyoyaeleza ni ukweli mtupu iweje anayeukosoa kitemdo cha Roman Catholic kuandaa waraka anaambiwa fisadi na kubezwa ili kila hali tunajua kuwa Dini isichanganywe na siasa.Hivi kweli Mwenye akili timamu anataka watanzania tuongozwe na Mashikh na Maaskofu nani wa kumchagua.Au hizi fedha chafu zinazotolewa kama njugu kama misaada zinatufanye tupoteze misimamo yetu

Kutoa tu 'sweeping/blanket statement' kuwa wamechangaya dini na siasa hakusaidii. Onyesha ni kipi cha kidini kilichochanganywa na siasa. Otherwise, inaoneysha kuwa hata wewe unafikiri kikongwe kama Kingunge, ambaye licha ya kuambiwa ataje kipengele chochote kwenye waraka kitakacholeta mafarakano au udini badala yake amezidi tu kusema ni waraka hatari bila ya kuoneysha ni kwa namna gani!

Hivi, hata huwezi kuchambua kitu?
 
Nimemuona na kumsikiliza huyu mzee wetu kwa kweli kimawazo/kifikra amekwisha kweli, kama mtu unavyozeeka kasi ya nywele inavyopukutika kichwani iko sawia na kupungua kwa fikra basi mzee wetu tumsamehe kwa kweli, hana HOOJA.
 
Nimemuona na kumsikiliza huyu mzee wetu kwa kweli kimawazo/kifikra amekwisha kweli, kama mtu unavyozeeka kasi ya nywele inavyopukutika kichwani iko sawia na kupungua kwa fikra basi mzee wetu tumsamehe kwa kweli, hana HOOJA.

Rais wetu alisema wazee ni dawa na lazima wapewe nafasi. Ila anashindwa kujua kuwa Kingunge ameishaingia kwenye senescence-The organic process of growing older and showing the effects of increasing age. Hapa mtu anarudi utotoni (Kwenye stage ya maji kuita mma). Sasa tumsamehe huyu babu. Anajua bado tupo kipindi cha mwalimu. Mi toka nimepata fahamu nasikia Kingunge, Kingunge. Mpaka ikafikia wakati viongozi wakawa wanaitwa "Vingunge". Hawa watu hawa ndiyo wanatuharibia nchi kwa kumpa rais ushauri wa kitoto.


6C2CA-senescence.gif


Ila tusipokapuuza haka kababu huenda wakati mwingine akili zinakarudia. Hapa isijekuwa ni moja ya kazi zilizomuweka kwenye ulaji kwa umri wake wote. nayo ni "propaganda" - Kwa kutaka kanisa limwombe radhi huenda anazuungusha usukani wa jahadi la mjadala wa "CCM na mafisadi" na kuupeleka kwa "Kingunge na Kanisa", huku akiwapa CCM muda wa kujiandaa na uchaguzi 2010. Tusimdharau huenda analijua analolifanya, japo hata kwa kufungiwa "chip" kwenye brain.
 
Last edited:
Kwa mtazamo wa kingunge ni kwamba kuna MUNGU wengi. Kila dini na ya kwake. KWAHIYO DINI NI VURUGU.Amesema hajaingilia maudhui KWAHIYO TATIZO SI MAUDHUI YAKE BALI KANISA KATHOLOIKI KULIANDIKA.Anasema ni KIONGOZI wa siku nyingi, MAFANIKIO je, ndo HUU UMASKINI, na UFISADI TELE Tanzania. Nilisoma mahali kwamba seli zinazotunza kumbuku ya zamani na mapya zinazeeka, kufa na hazitengenezwi upya. Kama ni kweli (madaktari kama wapo watuambie) kingunge kuwa mshauri wa Rais katika ulimwengu huu ni productive? kanisa haitenganishwi na siasa kwa sababu maamuzi yenu huko bungeni yanaathiri mfumo wa maisha ya kila mtu. hakuna mipaka. Kingunge Huwezi kutunyamazisha kama ajira, elimu, njaa, magonjwa na UFISADI BADO UPO. wewe ni Fisadi wa UBUNGO BUS TERMINAL
 
of course yes,kachanganyikiwa!!!!!!!!Namshangaa sana huyu mzee kumbe anajua mambo ya dini ni hatari?Mbona ccm wameweka waraka wa waislamu kwenye ilani yao?Ni lini wataweka ilani ya madhehebu mengine kwenye ilani ambayo kingunge ameitunga na kuisimamia.Haya yote ni matoko ya uroho na uanganyifu wa ccm.Bila kutumia ilani kuwahadaa waislamu haya yasingetokea.Baba wa taifa aliona mbele wakati huo kingunge alikuwa akiona karibu,Baba wa taifa asingekubali ccm kiwe hama cha kutetea maslahi ya dini fulani.Huyu mzee kazeeka vibaya.Huu waraka si mara ya kwanza kutolewa na kanisa nadhani mzee kashituka zaidi pale MAFISADI walipoanza kubanwa na waraka.Hajaonesha ni kwa jinsi gani waraka umivuruga nchi na hajaonysha
Kwa wale waliomsikiliza na kumuona Kingunge akiongea na waandishi wa habari jana bila shaka watakuwa na maoni tofauti kuhusu kikongwe huyu. Binafsi namuona kama mtu aliyeanza kuchanganyikiwa. Alikuwa anazungumzia Waraka wa Kanisa Katoliki lakini mpangilio wake wa maneno ni wa kushangaza na hauna mantiki. Mpaka sasa hajasema ni nini hasa anachoona yeye ni kibaya katika waraka huo unaohamasisha wananchi kuchagua viongozi waadilifu, zaidi ya kusisitiza kwamba utaigawa nchi.
 
Mtu wa pwani
Baba wa Taifa mwl Nyerere angekuwepo kingunge asingekuwa anakusanya kusanya vikodi ,kodi pale ubungo, PInda !!..... pinda !!! tusomeeee basi hiyo ripoti ya kituo cha basi cha ubungo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom