Kaa la Moto
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 7,903
- 1,053
Waraka wenyewe huu hapa View attachment 5607Mkuu umesema vizuri sana kwamba wewe HUONI popote penye matatizo.. Mimi naona sehemu nyingi sana kwani siku zote ktk Uongozi wa nchi, taasisi za kidini zinapoingilia kati ndipo utata huanza.
Unajua nchi za kiarabu kuna mengi ya wahubiri wa dini huzitaka serikali zao kufanya mema kwa faida ya wananchi wote lakini utata huja pale sisi tunapotazama nafasi ya dini na uongozi wa nchi hizo pamoja na kwamba population ya nchi hiyo ni 99 waislaam. Kifupi kanisa wala Msikiti hautakiwi kabisa kuingiza hoja zake serikalini unless swala hilo linahusiana na waumini wake.
Ni makanaisa na misikiti ilotuchanganya akili wakati wa uchaguzi wa Mkapa na huyu JK..ni hao hao waliowatukuza na kuwaona viongozi bora, leo hii tunapewa somo jingine tena wakati wa uchaguzi ukikaribia.
Trust me mkuu wangu hakuna mtu hata mmoja asiyefahamu nani kiongozi mzuri hata iwe jangwani au kijijini ndani kabisa Umasai...wote hawa walikuwa na mila za kuchagua viongozi wao na walitoa sifa au kashfa kutokana na kiongozi aliyepo.
Tatizo ni kwamba, kiongozi mzuri hana alama usoni nahata siku moja huwezi kukisia ila kwa ahadi zake..Kinachomtangulia kiongozi ni mfumo bora wa utawala.. Maadili na miiko ya Uongozi ndio road signs za kiongozi yeyote yule..kisha wananchi nao wapate somo la haki za uraia wao na sii somo la kumchagua kiongozi mzuri ambaye hajawahi kuongoza. zaidi ya hapo Mbunge sii kiongozi hata siku moja ila ni mwakilishi wa wananchi..
Hivi kweli unaweza kunipa sifa za kumchagua mtu kati Mwakyembe na Mwakalinga kwa kutumia vigezo hivyo?.. Mwakyembe tunamjua na mapungufu yake, mtu kama Mwakalinga hatumjui hivyo.. somo linatuambia nini kuhusu watu kama hawa?.. Je, linazungumza nini kuhusu wagombea wa vyama vya upinzani..Tunatazama mtu au chama? maanake nashindwa kuelewa inaonyesha kama waraka huu unataka tuishague CCM lakini tuwachuje viongozi wake badala ya kutazama upana na sera za vyama..
Siku zote uchaguzi wa viongozi hutokana na sera za chama sasa tukianza kuweka macho yetu kwa watu na tabia zao sijui nani mbora kuliko mwingine...
Hivyo pamoja na makosa ya mzee Kingunge ktk mtazamo wa wengi bado mzee huyu ana haki sawa ya kuelezea yale anayoyaona yeye kuwa ndio safi na tumkosoe kwa alosema tukizingatia kwamba tupo radhi kupokea maagizo kama haya ya waraka toka dini tofauti..
Binafsi sipo radhi kabisa na itajenga uhasama zaidi inapofikia viongozi wa dini kuitumia serikali kujenga kitu chochote kile..
Tuonyeshe wapi una kasoro badala ya kuja na hoja za kidini dini tu.