Jicho la tatu na Jinsi ya kulifungua (The third Eye)

Rakims

JF-Expert Member
Jun 4, 2014
4,982
4,482

JICHO LA TATU​

Watu wengi huamini kwamba Jicho la tatu ndio mwisho wa maelezo katika Meditation ama ndio moja kati ya mafanikio makubwa katika Meditation lakini kuhusu hili jibu ni HAPANA.

Safari ya Mikao ya Meditation ni kubwa kuliko vile mtu anavyofikiria kwa haraka.



Kuna vituo vingi sana katika Meditation ambavyo mtu anaweza kupitia hadi kufikia Jicho la tatu lakini pia safari haiishii hapo bado itazidi kwenda hadi kufikia Crown chakra na huko ndio kwenye mafanikio ambayo mtu anadhani kuwa anaweza kuyapata katika jicho la tatu.

Vile vile wengi hudhani aliyeifikia Crown Chakra ndiye aliyeyafikia mafanikio ya Meditation hapana waliofikia Crown Chakra ni sawa na maskini aliye tajirika kwa kupata uchumi Size ya kati na kuona yeye ndio Bernard Arnault au Elon Musk mwenyewe.

Hii video ni muendelezo wa video za Chakras katika playlist ya Chakra za Meditation inayopatikana

https://www.youtube.com/@rakimsspiritual/playlists

Ni mapenzi yangu kufundisha hatua kwa hatua katika playlist hiyo isipokuwa nimeandaa kwa maombi mengi ya watu kuomba kufundishwa juu ya jicho la tatu.

Kwanza kabisa tuangalie Jicho la tatu ni nini?​

Jicho la tatu ni Moja kati ya vituo maarufu kama Chakra katika mwili wa mwanadamu.

Zipo Chakra saba ikiwa bado hujazitambua vizuri basi rejea katika videos za chakra nilikuwa naelezea chakra moja moja na faida zake.

https://www.youtube.com/watch?v=xKL62RKzcUA&list=PLCxOn3pv1vHOTrZjUtNkPt3bNtB7sX1hl

Hivyo basi hii ni Chakra ya Sita ambapo tunaita chakra ya Jicho la tatu. iliyojaa mambo mengi na fikirishi kwa watu wengi na kama bado hujaijua inahusu nini basi rejea katika playlist ya chakra utajifunza jambo kuhusiana na chakra hizi.

Hivyo kwa maelezo mafupi Jicho la tatu ni Chakra ya Sita ambayo inahusishwa na MAONO ambayo hufungwa na Illusion yaani imani ya maono potofu.

Hivyo sishangai kwa wale walioona sticker ya video hii na kuona teyari hii video itakuwa inahusu uchawi basi bila hata kusumbuka akili moja kwa moja unajua tu kwamba hawa watu wamepotoka kwa kudhani ama kufananisha jicho la tatu na jicho la Dajjal ama Mpinga Christo unajua ukikosa maarifa kila kitu chenye mtizamo zaidi ya uelewa wako wewe utaona uchawi tu.

Ukweli kuhusu jicho la tatu?​

Ukweli kuhusiana na jicho la tatu. Jicho la tatu ni neno tu la kutambulisha ama idea ya kuweka uhusika wa jambo linalozungumziwa hapo.

Jicho la tatu ni jicho la roho ama mtizamo wa roho katika mambo ya kiroho ambayo si rahisi kuonekana kwa jicho la kawaida.

Jicho la tatu ni sawa na kufunua pazia ulilowekewa katika macho yako kwa ajili ya kutokuona mambo mengine yasiyoonekana kwa macho ya kawaida.

Jicho la tatu

Kama vile roho zilizozagaa, wachawi, majini, malaika, bacteria na mengineyo mengi yasiyoonekana.

Hapa hapa linaweza kupatikana swali kwamba kwa hiyo waganga na wachawi wenye uwezo wa kuona vitu mfano hivyo je wamefungua jicho la tatu?

Jibu ni HAPANA wala hao hawana wanachojua kuhusiana na jicho la tatu.
Jicho la tatu ni zawadi kama zawadi zingine alizokupa Mungu kisiri ili washindane na wenye kushindana basi na atakae lifungua ataona mengi kwa ukweli wake.

Swali lingine linaweza kuja hapa kwamba

Je, aliyefungua jicho la tatu anakuwa kwenye imani fulani ya dini?

Jibu ni HAPANA kwa maana swali hili ni sawa na kuuliza

Je, watu wenye roho ni watu wa dini fulani pekee?

Hivyo ukweli kuhusu jicho la tatu sio Jicho kama vile jicho mtu analo dhani lipo katikati ya nyusi hapana hili sio jicho.
bali ni maono ya kutumia roho yako katika kuangalia UKWELI.

Nadhani hadi hapo shaka na dhana kuhusu Jicho la tatu na Ushetani nitakuwa nimekutoa.

Jicho la tatu lina faida gani?​

Faida za jicho la tatu hutegemea na matumizi ya mtu na mtu baada ya kulifungua. wengine huweza kupata experience zaidi kuliko wengine lakini faida za jicho la tatu kwa ujumla kwa watu wote wenye kufungua ni kama ifuatavyo;

  • Uwazi wa kiakili ambapo hukuongezea fahamu na kumbukumbu.
  • Ukishika ama kufanya chochote hufanikiwa.
  • kuwa na uwezo mzuri wa kuujieleza kwa wazi.
  • Kuwa na machale yalichopitiliza.
  • Kuhisi raha muda mwingi katika roho.
  • Kuwa na maamuzi sahihi.
  • Kuwa na maono makali na Maamuzi sahihi.
Hizi ni faida kuu za awali kabisa ambazo kila mtu huweza kuzipata pale ambapo akiwa amefungua jicho la tatu na pia dalili za jicho la tatu kufunguka kwa mwenye kufungua ni kama ifuatavyo;

Kuna dalili ambazo hutokea kwenye mwili na zingine hutokea kwenye roho ama akili;

Kuhisi mgandamizo kiasi katika jicho la tatu​

Ukiwa unakaa ama kufanya jambo basi utahisi mgandamizo mfano mitekenyo katika jicho hili la tatu yaani eneo katikati ya nyusi.
Mara ya kwanza inaweza kukuchanganya na kukupelekea kutaka kupekecha sehemu hiyo lakini baada ya muda utazoea.

Kuona Sababu ya wewe kuwa hai​

Muda mwingine hutokea wakati unafungua jicho lako la tatu unaona sababu na nini unatakiwa ufanye katika uhai wako maana yake utaona hasa ni nini muongozo wa maisha yako unakutaka ufanye na hapo ndo utapatia sababu ya kwa nini wewe uko hai.

Hii ni moja kati ya faida kubwa sana wanazozipata wenye kufungua jicho la tatu.

Moja kwa moja baada ya kujua hili utaanza kuongezeka kwa hisia zako ama dhana zako kuwa na ukweli ndani yake, utakuwa na uwezo wa kumjua mtu akili na fikra yake inawaza nini, utakuwa na uwezo wa kuona jambo kwa kubashiri kabla halijatokea yaani utakuwa unapata kama maono ya jambo lililopita na linalowezekana kutokea.

Kama haitoshi utaanza kuhisi ukaribu na ulimwengu uliyopo na kuanza kujihisi kufanya heri kwa watu wengine kama kupanda miti kwa ajili ya vizazi vijavyo kutengeneza mazingira ya watu wengine kufurahi na utapata kujua ni msaada gani unaweza kuutoa kwa watu wengine kwa jambo moja unalo lifahamu ama utalijulia huo ambalo litakufanya uwe mmoja ya watu wema wenye kukumbukwa.

Utaanza kupata ndoto za watu ambao unawaheshimu katika Maisha ya kuroho mfano Babu zako, baba zako, Mitume wako na hata malaika wa kweli ikiwa utafungua katika misingi ya kiimani thabiti.

Wengine hupata picha za kurudi nyuma na kumbukumbu zilizozikwa na ubongo kama maisha ya utotoni na uzeeni kwa wale ambao roho zao zimetakata.

Vile vile kwa wenye roho za kizee yaani vijana wenye roho za kiutu uzima kwa maana busara zaidi basi kwao ni rahisi sana kufungua third eye ama Jicho la tatu.

Na sababu kuu ya jicho hili kufunguka utaiona na utaelewa kwa undani zaidi pale ambapo litafunguka moja kati ya wazee waliopita kipindi cha nyuma aliwahi kwenda na kuhiji makka katika usingizi wake na kuhadithia watu waliofika huko jinsi palivyo nao walikili ni kweli enzi hizo Televisheni ni kitendawili kwa watu wengi.

Pia zipo story nyingi za maono ya watu wenye kufungua jicho la tatu na kuona mambo mengi yasiyowezekana kufikiwa kwa akili ya kawaida hasa kwa watu wengi maarufu na wenye hesabu kuu za maumbile ya dunia ajabu ya mambo haya hutakuta yanafundishwa Shule yoyote ama vyuo vyovyote.

Usiangalie nani kafungua na kapata nini angalia wewe ukifungua utapata nini?

Katika kufungua jicho la tatu utapata kujua ni nini wewe unatakiwa kufanya mfano kama wewe ni muandishi mzuri wa vitabu na umefungua jicho la tatu na ukaona unatengeneza gari yako ama ya watu na maono haya yamekujia mara tatu.
Basi moja kwa moja usichelewe achana na hiyo kazi kajifunze ufundi uanze kufurahia maisha yako kwa maana huo ndio wito wako.

Utajikuta ni mwenye mafanikio makubwa kwa muda mfupi sana na utaona ni wito mkubwa wa mafanikio hivyo kupelekea kusaidia hata wengine wasiokuwa na uwezo wa kujikomboa katika maisha.

Maumivu katika mwili​

Pindi unapokuwa mwanzoni katika kufungua jicho la tatu moja kwa moja utaanza kupata maumivu sehemu za mwili ambazo ni ishara kuwa jicho hili linafunguka utaanza kuhisi:

  • maumivu ya kifua,
  • maumivu ya tumbo,
  • kupatwa na hofu,
  • utumbo kuvuruga vuruga,
  • kuota unatapika tapika vitu vya uchawi na ajabu ajabu,
  • juu ya tumbo kunakuwa na vurugu kama mtu mwenye ulcers
  • maumivu yasiyo eleweka
Haitachukua muda utaona hali hiyo imepotea.
Dalili hizi si pekee ambazo humkuta mtu lakini kufupisha maelezo nimeandika ambazo mtu anaweza kuzipata mapema sana.

Kuona mwanga, maumbile ya hesabu na michoro ya ramani ukifumba macho​

Ukifumba macho ukatizama eneo la jicho la tatu utaona mwanga na nuru ambayo itakuwa imejichora maumbile hayo ambayo utaona mwanga mkali unakumulika wengine kufikia hapo unakuta anataka kufumbua macho ili kuona kafumba au kafumbua macho.

Mara nyingi watu wengi rangi ambazo huona ni Blue, indigo na nyeupe.

Hizi rangi zenye mwanga huwatokea na kuhakikisha kwamba muhusika anaekuta anatumia jicho la tatu kwa muda huo anakuwa hapitiwi na usingizi katika mwili wake ili kuzuia akili kuweka maono hayo kama ndoto;

Na vile vile huwa ni rangi za kupendeza sana ambazo kwa hakika hakuna aliyefikia hapo akatamani kupitiwa na usingizi na hii ni kwa maana kwamba ubongo wa mwanadamu huhitaji giza ili kuweza kulala ndio maana katika kufungua jicho la tatu kuna mwanga mkali katika jicho la tatu ambao huhakikisha mwenye kufanya zoezi hili halali.
Fikiria kwa nini mitume walikuwa wakifanya ibada hawapitiwi usingizi na wewe ukifanya ibada kidogo tu unahisi kulala.

Kuongezeka kwa mwanga na hisia za sauti​

Ni kawaida kwa watu ambao jicho la tatu limefunguka kwao kuhisi kero kwenye mwanga mkali na sauti za kelele.

Ulishawaihi kumuona nani kafungua jicho la tatu anapenda makelele au mwanga mkali?

Jibu ni hapana watu hawa hutawakuta Disco wala sehemu zenye makelele au maharusini wengi wao hawahudhurii, utawalaumu bure tu wao ni watu wasiopenda sauti kubwa wala mwanga mkali.

Ukiwakuta maeneo hayo basi ni sawa na kuwatesa kisiri siri na hata wakiigiza ili wasionekane wamepitwa na wakati ama ni wenye kujisikia basi baadae wakikaa peke yao kwenye utulivu huwa na visirani.

Pia utakuwa na macho yenye nguvu sana na hata ukiona mwanga mtizamo wako utakuwa ni tofauti na awali na hutapendezwa na mwanga mkali.

Hii ni kwa sababu akili na ufahamu wako wa ulimwengu unakuwa unatanuka katika ulimwengu wa nyama na wakiroho.

Utaanza kuyaelewa maisha yako​

Hata kama uelewa wa maisha yako siku zote ni sehemu ya maisha yako na ni mwenye kuelewa maisha yako lakini kujua maisha yako kwa mtu ambaye roho yake bado ipo usingizini wale wazee wa thibitisha kisayansi na technolojia kwao ni ngumu sana kuelewa kweli ya maisha yao.

Ndio maana utaona kila siku wanahangaika kujilimbikizia hazina wao binafsi za kuwafaa miaka elfu 1 hali ya kuwa hawajui hata kama miaka 50 tu watafika.

Ni kwamba mtu anapofungua jicho la tatu uelewa wake wa maisha unakuwa ni mkubwa sana na hivyo kufikia hatua ya kufahamu kwamba hakuna kitu kama bahati mbaya katika maisha.

Kwa maana ulimwengu teyari umekwisha kadiriwa mambo yake na hatua zake kwa hesabu zake hivyo kila kitu hutokea kwa njia fulani.

Hivyo ukifungua jicho la tatu utaanza kuona watu fulani wanaanza kuja katika maisha yako na kwa muda sahihi na kuanza kukuongoza maisha yako ya kiroho.

Ukianza safari ya kufungua jicho la tatu na chakra zingine utaelewa matukio mengi ya ulimwengu na imani yako itakomaa vema na mambo yako yatakwenda kwa mipangilio iliyokadiriwa vema na kwa kukutosheleza kuwa na furaha.

Utakuwa ni mwenye kujielewa zaidi kwa kila unachokula​

Vyakula huwa na nguvu ambayo inaweza kukuongezea mitetemo ya mwili wako hivyo jicho lako la tatu linapofunguka moja kwa moja utafahamu ya kwamba

Mwili wako utaanza kudai vyakula ambavyo vinaweza kuhimili mikiki ya jicho la tatu na ambayo inaweza kukupelekea kuanza kuchagua na kubagua vyakula kwa mpangilio sahihi unaotakiwa.

Ili kwenda sawa na maisha ya jicho la tatu na hii inaweza kufikia hatua ya kuanza kuota vyakula unavyokula pia.

Inaweza kukuijia hali ya kuacha kula nyama kwa maana ukitaka kula utakuwa unakumbuka ama kuhisi ni jinsi gani wanyama walikuwa wanaogopa na walikuwa wanaumia wakati wa kuchinjwa.

hii inakuwa katika mitizamo miwili kwa watu wale wanaofanya kwa imani na wale wanaofanya kwa bila ya imani.

Mabadiriko mengine yatakayo kukuta ni utajihisi ni mwenye kutamani sana kula vitu vya asilia zaidi kuliko vitu vilivyoandaliwa yaani utajikuta ni mwenye kutamani kula zaidi vyakula fresh kuliko vya kusindikwa.

Utajikuta ni mwenye kuvutika hata kupanda mti mmoja nyumbani kwako wa maua ili upate harufu za asilia kuliko za Air freshener Super Market.

Hii ni kwa sababu mwili wako utakuwa ni wenye kukuamuru kufuata zaidi maisha ya kiroho kuliko kufuata maisha ambayo yanakunyonya nguvu za kiroho na kukufanya kuwa mtumwa wa maisha ya upofu.

Hivyo ukizingatia utakuwa na mitetemo mikubwa na uelewa zaidi katika hii dunia kuliko watu wengine wanavyoitizama.

Ndoto za kama upo macho ama ndoto za kujielewa unaota​

Jicho hili la tatu kwa wengi tuliofungua ndoto hizi kwetu si ngeni lakini pia ni moja kati ya maliwazo ambayo mtu huyapata anapolala.

Imagine kwenye ulimwengu wa kawaida ulikuwa unatamani nini uweze kukifanya kisha unashindwa na huku ukirejea kwenye ndoto za kuota unakuwa unajua kabisa kwamba hii ni ndoto na nina nafasi ya kufanya ninachotaka?

Ndoto zako zitakuwa ni ndoto ambazo zipi wazi zaidi na utakuwa ni mwenye kujua unachoota vile vile kuna siri hapo ya kuwasiliana na malaika wale uliokadiriwa achilia mbali majini na mashetani nayo hutegemea jinsi ulivyolala.

Humo utapata kuita ama kutafuta malaika nae anaweza kufika na kuzungumza na wewe wengi hupinga hili kwa nadharia tu lakini hawajui ni nini hiki?

kwenye ndoto unaweza kuzungumza na malaika na kupokea ujumbe kutoka kwa mwenyezi Mungu kwa maana hasa ukizingatia ndoto zipo za aina tatu:

  1. Ndoto ya Mwenyezi Mungu
  2. Noto ya Shetani
  3. Ndoto ya Ubongo

Ndoto za ubongo zinaweza kuwa taarifa za kimwili au kiakili lakini zinapoingia kwenye taarifa za kiroho hapo ndio fahari ya jicho la tatu huja kwa maana hizi ni ndoto ambazo zina ujumbe mzito na mkubwa sana katika maisha yako na mafanikio yako.

Nitakuja kuelezea ndoto hizi na kina chake.

Vyovyote vile hakuna jambo zuri kama kuongoza kila ndoto inayokuijia imagine ni ndoto ngapi ungekuwa na uwezo wa kuziondoa ungeondosha au kuzigeuza?.

Pia tatizo lolote linapotaka kukukuta basi utaona moja kwa moja jicho la tatu linakuongoza katika ibada. Na maombi ya mtu aliyefungua jicho hili la tatu ni yenye kupokelewa kwa haraka zaidi kwa sababu anakuwa na heshima na hekima katika maombi.

Kuliko wale wenye kujiona Miungu watu na wengine ni wale wenye kuamini upumbavu na kupenga uwepo wa roho na kauli mbiu yao huwa.

"I can do all things with my own knowledge, you are just deceiving yourselves"

Na pale inapokuijia ndoto ya wakati ujao basi hakikisha unachukua kalamu na karatasi unaandika chini ili kuweza kujua details muhimu kama;-
  • rangi ya siku hiyo?
  • mchana au usiku?
  • mwenyewe ni nani?
  • anafanya nini?
  • anafaida gani baadae?

Muhimu chukua na andika chini kila details ili utakapo pata kufikia siku hiyo ujue ni nini cha kubadirisha na nini cha kuacha.

Unakuwa ni mwenye kuwa na uwezo wa Clairvoyance safi​

Clairvoyance safi ni ile ambayo mtu hujua jambo kabla halijatokea ama katika mambo watu wengi hugombania kuyajua ni kujua jambo kabla haijatokea unaweza kuona ni watu wangapi wenye kugombania kujua jambo kabla halijatokea.

Basi katika faida hii nyingine mtu anaweza kujua ni nini kinachotaka kutokea kama kizuri au kibaya na wala hatakuwa na tatizo katika maamuzi yake.

Lakini pia kwa watu wengine huweza kuwakuta second sight kali ambayo akikaa tu utaskia anakwambia hapa anakuja fulani na punde tu anafika.

Hata kwa wengine pia huwatokea picha picha ambazo zinaonyesha tukio lijalo katika akili zao ukienda kwa watu wenye roho za kwanini watakwambia unajidanganya na akili yako na unachezewa na mashetani huku hao hao watakwambia dalili hizi huwakuta marafiki wa Mwenyezi Mungu.

Mungu marafiki zake anawajua yeye mwenyewe na wala hajawawekea alama usoni kwamba hawa ni marafiki zangu, na huwezi jua ni tukio gani dogo au kubwa ulilofanya likaweza kukufanya kuwa rafiki wa mwenyezi Mungu.'

Hii hawajui wengi ila wachache sana kati ya hao marafiki wa Mwenyezi Mungu ambaye ndio muumba wa Ardhi na Mbingu Mungu ambaye hana haja wala kutaka msaada wa yoyote katika kufanya mambo yake hivyo usiwe na shaka nae.

Ikikufungukia Nguvu hii moja kwa moja utaona ni mwenye kuepukana na mabalaa mengi na kutengana na watu wenye roho za kutaka kukuangamiza au kukutawala akili na mwili wako kwa matumizi yao binafsi.

Baadhi ya watu huwa ni watumwa wa watu wengine kwa kukosa tu elimu kama hizi ambazo zimezibwa na wengi wanaotaka uwe mtumwa kwao.

Kama vile siku zote mtu mwenye maarifa ya hekima hawezi kutaka mwanadamu mwenzie alale chini ili yeye amkanyage kuvuka daraja.

Hii ni lugha ya hekima na ya kiutu uzima katika kuwapa ujumbe wa kiroho watu wazima kwa hivyo maana yake isiwe tofauti ama kuchukuliwa tofauti huu ni mfano wa karne zilizopita.


Haya matukio mengi wala hayata kufanya kuwa kama Mungu mtu isipokuwa yatakufanya kuelewa zadi ni vipi unatakiwa kuuendea ulimwengu ambayo ni makazi yako ya muda.

Kuliko kukaa chini umeshika tama hebu kaa chini dakika ishirini za kuangalia yaliyomo kwenye jicho la tatu ili uweze kupata muongozo mpya na mtizamo mpya wa sura mpya ya maisha yako.

Ikiwa hutaamini unachokiona ndani ya jicho lako la tatu basi moja kwa moja utapoteza ladha na thamani ya zawadi hii uliyokadiriwa na mwenyezi Mungu.

Kuwa na Uwezo wa kuamuru akili za wengine (Telepathy)​


Ghafla utaanza kuona ni mwenye kuhisi na kujua fikra za mtu na akitaka kusema kitu unaweza kujikuta unakimalizia au hata kabla yeye hajasema unakuwa umeshajua anataka kusema nini,

Waliowahi kuwa karibu na wenye uwezo huu wanalijua hili, vile vile wale waliowahi kubahatika kukutana nami katika mood nzuri hulijua hili.

Kupitia matendo na maneno ya watu basi kwako itakuwa ni rahisi sana kuweza kujua ni nini malengo na hatima za maneno au matendo yao.

Na utaelewa kwa urahisi watu wanakufikiria nini kwa muda huo au ni nani anakusema kwa muda huo na ukimtafuta moja kwa moja unakuta ni kweli na yeye huthibitisha hilo.

Mfano;
Unaweza kuhisi ama kufikiria mtu anakuwazia na punde tu akaanza kukutafuta kwenye simu au simu ikaanza kuita kisha akipiga utasikia anakuwambia nilikuwa nakufikiria hapa.
Hii ni hata kama kwa mtu ambaye hujawasiliana nae muda mrefu utaona anakutafuta.

Pia ukijua jinsi ya kuwashtua kwa njia ya fikra utaskia mtu anakuuliza unaniita au? Hali ya kuwa hujatoa sauti, Baadhi ya watu huwatokea hili bila kufungua jicho la tatu.

Moja kati ya wawili hawa huwa ni mwenye Kuskia sauti za fikra za mtu.

Mwanzoni haya mambo huwa yanatisha na kuogopesha kidogo kwa maana watu huamini nguvu hizi ni msaada unaotoka kwa shetani kwa maana mashetani hudanganya watu kuwa wanaweza kuwapa nguvu hizi jambo ambalo sio kweli.

Ni vile tu wao wana maarifa ya kukusaidia kuboost kwa haraka nguvu hizi bila kufanya mazoezi lakini nguvu hizi ni zako na ndio maana katika imani ya Dini ya kiislam utaskia wanasema hakika ya shetani na mwanadamu basi shetani ni Mdhaifu.

Zitumie nguvu hizi zinazokuja ukifikia hatua ya kuamsha jicho la tatu kwa uwajibikaji mzuri kuna usemi katika Sinema za watoto husema

"With a great power comes great responsibility" Uncle Ben from SpiderMan

yaani;

"Ukiwa na nguvu kuu basi wajibu wako utakuwa mkubwa pia"

Well, chanzo cha usemi huu ni kwamba wengi hasa watu waliozaliwa miaka ya 50 kurudi nyuma watakumbuka usemi huu ulikuwa maarufu kwenye vipengele tofauti tofauti;

Tukianza katika dini ya kiislamu usemi huu unaweza kurelate na Ayah inayomzungumzia Dhul Qarnain ama wengine humfahamu kama Cyrus katika Biblia ama wengine huona ndio Alexander the Great mwenyewe kwa watu wa historia.

Lakini kwa kifupi huyu ni maarufu kwa kutengeneza Ukuta uliotenganisha kabila la wanadamu na (Kabila lingine la viumbe maarufu kama Yajuj Maajuj) yaani GOGS & MAGOGS

na mwenye kugundua kuwa Jua huzama kwenye Chem chem ya matope ambapo ukumbuke kuwa huyu alikuwa sio mtume bali ni mtu aliyepewa maarifa kwenye Playlist ya wajue

https://www.youtube.com/watch?v=xy81xqlBwBY&list=PLCxOn3pv1vHPJflWzi1UTNafcV74sCign

tutaendelea nae kwa hapa tunachukua maana ya kauli,

"Ukiwa na nguvu kuu basi wajibu wako utakuwa mkubwa pia"

tunachukua kuanzia kwake kusema:

"Hii ni rehema itokayo kwa mola wangu mlezi"

Quran: Kahf 89 - 98

kwa wasomi wazuri wa Quran basi wataangalia hapo kuanzia aya ya 89 hadi 98 kisha watajua waandishi wa vitabu vyake walipata Idea kwenye kifungu gani cha Quran.

Maana ya kwanza tunapatia hapo katika Quran tukufu,

Maana ya pili ni katika biblia Takatifu inasema:

"Na yeyote aliyepewa vingi, kwake vitatakwa vingi"

Hiyo ni Luka 12: 48

Kwa wasomi wengi wa biblia wataiona hapo.

Maana ya tatu tutaipata kwenye Maarifa ya kawaida:

Eeh! Rakims anaanza kuleta udini tena hapana ni katika kuwaelewesha makundi ya watu watakao tizama hii video.

Usemi huu kwa vijana wa miaka ya 2000 utakuta kwao ni maarufu sana katika sinema yao pendwa ya Spiderman moja kati ya sinema nzuri zenye kushawishi watoto nguvu za miujiza zipo kwa kuwapumba na kuwatia gizani watu wazima kuamini kwamba Nguvu za Miujiza ni Fikra tu wala hazipo ili kutoka katika Imani ya roho na kuendelea kupumbazika.

Wala huu usemi haukuanza hapo na sio maarufu hapo usemi huu ni maarufu kwenye vyanzo hivyo vya dini lakini pia ulisikika ukitumika kwenye

Mpango wa kazi, ufuatiliaji na mawasiliano, uliopendekezwa na Kamati ya Usalama wa Umma kwa Wawakilishi wa Watu, manaibu waliokuwa karibu na Majeshi ya Jamhuri ya Mkataba wa Kitaifa wa Ufaransa mnamo mwaka 1793,

Kuna sentensi hii:

"Ils doivent envisager qu'une grande responsabilité est la suite inséparable d'un grand pouvoir"

Maana yake;

Lazima wazingatie. kwamba jukumu kubwa huja kwa wale wenye nguvu kubwa hivyo wao ni wawakilishi wa taifa lao na wana majukumu hayo na makosa kidogo yanaweza kuwaletea matokeo yasiyoweza kutenganishwa ya mamlaka kuu

Hivyo wao wawakilishi lazima watambue hilo.

Mnamo mwaka wa 1817, Mbunge wa Uingereza William Lamb alirekodiwa akisema,

"kumiliki mamlaka kuu kunamaanisha wajibu mkubwa."

Vile vile haikuishia hapo pia Mnamo mwaka wa 1906, Katibu Msaidizi wa Ofisi ya Kikoloni Winston Churchill alisema,

"Palipo na nguvu kubwa kuna jukumu kubwa”

hata ikionyesha kuwa tayari ilikuwa kanuni ya kitamaduni iliyoletwa kwa serikali wakati huo

Hivyo huu ni ukumbusho na kukujulisha kuwa Movies zinazotengenezwa kuhusu mambo haya ni chanzo cha ukweli uliokuwepo wa matendo yaliyowahi kutokea nyuma na pia ili uelewe kuwa ukiweza kufikia nguvu kuu basi usitumie kama wanavyotumia wengine kuweza kuwafanya watu vitega uchumi.

Maumivu ya kichwa mara kwa mara​

Kama vile jicho la tatu litakavyofunguka basi moja kwa moja utaona kuwa kichwa mara kwa mara kitaanza kukuletea maumivu madogo madogo na hii ni kwa mwanzo kutokana na nguvu ya Kundalini inaanza kumalizia kukujaza nguvu ya jicho lako la tatu.

ukumbuke Nguvu ya kundalini nishati yake hutokea kwenye Chakra ya Base yaani Root Chakra hivyo kuna umuhimu wa kuzingatia kama nilivyoeleza awali kuwa kila chakra inategemea chakra nyingine kuweza kuwa Angavu.

Na inapozidi kujaa hiyo basi nguvu hii itaenda na kucharge zaidi Pineal grand yako ambayo ipo katikati ya ubongo na ambayo ndio source ya nguvu za miujiza zote.

Baadhi ya imani fulani fulani huamini humo unaweza kuona wewe zamani uliwahi kuwa nani?

Dhana ya Lincanation ipo hapo?

Na pale ambapo nguvu yako ya Kuamsha jicho la tatu ndio itaanza kuamsha matumizi ya chakra moja baada ya nyingine,

Hivyo elewa ya kwamba kuna kucharge kwanza chakra kabla ya kuziamsha. Na kila chakra ina kazi yake rejea katika playlist ya chakra na video nyingi zitazungumzia chakra na matumizi yake.

https://www.youtube.com/@rakimsspiritual/playlists

Hivyo kufunguka kwa jicho lako la tatu hakumaanishi ndio utapata nguvu za miujiza hapana isipokuwa unapokuwa Jicho lako la tatu limeamka litataka kukuangazia nguvu ambayo wakati wa kufyonza Nguvu kwenye chakra zingine.

Ndio utaona mabadiriko yanaanza,

Ili chakra hizo ziweze kutoa nguvu zitahitaji nguvu kutoka katika Plexus Chakra ambayo ni chakra ya tumbo na ili Chakra hii iweze kutoa nguvu itahitaji Base Chakra katika Surviving ili kuweza kupata chakula.

Na ili Base chakra iweze kutoa surviving mode itahitaji kiwingu cha Womb Chakra kiondoke na ili iweze kutoa nguvu.

Na Chakra ya Tumbo la uzazi ili iweze kutoa kiwingi cha maarifa ya surviving itaituma Chakra ya Solar Plexus vitu inavyotaka ili iweze kuingiza sumu ya kuua kiwingu hicho ambapo Chakra hii itapeleka taarifa kwenye 4th chakra yaani Chakra ya Moyo Na ili chakra ya moyo iweze kutoa mapigo ya moyo na mapenzi ya moyo yaweze kubadili tamaa za vyakula ambapo ikisha piga moyo ndio itatoa na yenyewe taarifa kwa

Throat chakra kwamba inataka kiingie nini ndani ya Tumbo kisukumwe na Plexus Chakra,

Kisha throat chakra hiyo itaipa taarifa third eye Chakra (Jicho la Tatu) ambapo third eye itaomba kwa Crown Chakra maono yajao yaani nguvu ya future seeing katika chakula ili Kundalini power iweze kuwa activated na kuamsha nguvu zote na chakra zote.

Sijui mnanielewa!!!!!!!!!!!!!?


Kwa hivyo hadi hapo utakuwa umefahamu nini faida za Jicho la tatu twende kwenye hasara zake.

Hasara zake ni zipi?​


Kama unavyofahamu kwamba teyari nimeshakuelekeza jinsi faida za Kufungua jichohili la tatu moja kwa moja twende kwenye hasara zake;

Ingawa kuna faida nyingi unaweza kuzipata kwa kufungua jicho la tatu ambazo zingine sijaamua kuorodhesha hapo moja kwa moja tuangalie hasara za haraka na kubwa anazoweza kupata mtu mwenye kufungua jicho la tatu.

Bila shaka faida ni nyingi kuliko hasara ama hatari, lakini mwenye kufungua jicho la tatu sio tu atapata faida pekee maana yake na hasara zipo hivyo utatakiwa ujiandae nazo na uzikwepe.

Kama mtu atafungua bila maelekezo marefu kama nilivyoelekeza awali na nitakavyozidi kuelekeza katika video zijazo basi moja kwa moja utaanza kuhangaika na kuhisi umeelemewa kuanza kutumia nguvu hii.

Madhara ya kufungua jicho la tatu yanahusisha mambo yafuatayo ambayo yanatakiwa kuwa nayo makini sana pale yanapoanza kujitokeza.

1. Ndoto za kijinga na Ndoto za kutisha​

Pale jicho lako la tatu linapofunguka upinzani huwa ni mkubwa sana kwa forces ambazo zilipenda ubaki kuwa kipofu ili usijue shere unazochezwa hivyo unaweza kulala ukaota mtu analazimisha kukulisha kitu kibaya unamtandika kibao ama ngumi ama unamchoma kisu kisha unaamka ukiwa na wasiwasi which hauumizi mwili isipokuwa akili yako itakuwa na wasiwasi,

Ikiwa umefungua jicho lako la tatu kwa bahati mbaya bila kujiandaa basi moja kwa moja usingizi wako unaweza kuvurugika sana na kuona ni bora uwe unalala mchana.

Kifupi unaweza kuota ndoto za kutisha na ambazo zinaweza kukukosesha raha kwa siku chache za mwanzo lakini niamini it worth it.

Utaamka ukiwa ni mwenye kujihisi mchovu sana na kuona picha ulizokuwa unaota ndotoni zinakuijia kichwani mfano kumbe kila siku huwa unalala na jini mahaba ama mchawi na humuoni kisha unamuona na kumtimua basi kwa wengine hujihisi vibaya kiuhalisia.

Hii point ya wachawi itasababisha video hii kuwa na wenye kuipenda wachache kwa maana hata comment zao utaona tu wanavyotoa kwa mtu mwenye kufuatilia video hii kisha aje asome comment za wachangiaji ataelewa ninachosema.

Ila wengine wameumbwa na haya ukiwataja hawa comment kashfa.

Vile vile ni kitu ambacho kitakufanya ujihisi kukosa utulivu na raha ndio maana huwa nashauri watu kabla ya kufungua jicho la tatu basi uwe umejiground vema sana kwa chakras muhimu kama Base chakra na Solar Plexus.

Hizi chakra pekee ukizicharge unaweza kumshika jini ukamwambia tulia hapa mtoto nikulee ukaoa na akakuzalia waototo na mashetani ukapiga vibao.

Ni ngumu kuamini kwa watu ambao roho zao zimetawaliwa na shetani mwenyewe.

Unaweza kujisaidia na kuondoa hii side effect kwa kufanya meditation kabla ya kulala ama kulalia ubavu wa kushoto.

Kwa ajili ya kubalance maono ya jicho la tatu

Zaidi ya hapo tunza kumbukumbu ya ndoto zote utakazo kuwa unaota kwa kipindi chote hiki unapitia hizi side effects.

Ili uweze kuzimudu katika lucid dreams. nitakuja kuelezea lucid dreams kwa kirefu pia.

2. Kujihisia dhana za kutisha​

Unapokuwa umefungua Jicho la tatu kwa mara ya kwanza utaona ni kama Jicho hili la tatu ni majanga kuliko kuwa na faida na utaona kuwa linakuletea mawenge na utatamani kurudisha ama kulifunga jambo ambalo sio sahihi

Elewa ya kwamba hichi ni kipindi cha mpito ambacho kinakupitia na kikiisha utafurahia maisha. Nakumbuka niliwahi kufundisha wanafunzi kipindi cha nyuma walikuwa 20 online mwaka 2012.

Kabla ya kufundisha phase 2 ya Jamii Forums ilikuwa na watu 76 kuna mwanafunzi mmoja aliwahi kunifuata na kusema tufanye mpango tufunge Jicho la tatu maana akikaa anaona jamaa anamwambia

"sasa unaogopa nini"?

Anafanana kila kitu kama yeye. Nilipokuja kumsikiliza vema alikuwa ni Doppel Ganger wake ambaye ni Qareen alikuwa anatokea vivid na kupotea hivyo nikamfundisha kujiweka sawa kwa kupitia meditation hivyo ni vema kutokuwa muoga wakati wa kuanza hili jambo kwa maana wapo ambao huona vivuli vikikatiza maeneo ya karibu.

Hivyo ukitaka kuanza kufanya hakikisha unarejea kwanza kwenye video ya Channel hii inayohusu meditation usikilize kwa makini kisha ufanye ndio uje kwenye hatua za kufungua chakra moja baada ya nyingine.

Vile vile mtu huanza kudhani na kuogopa uwezo wake wa kujua mambo yanavyokwenda kwa maana huanza kujitahidi kupush hizi nguvu zisiwe nae jambo zaidi la kuogopesha ni pale anapojihisi na kudhani je ikifika siku nakufa nikaona ndotoni?

"Kufa kupo tu, unaweza kufa ukiwa unafanya chochote hata ukikaa unakunya utakufa tu".

Aliskika baba mmoja akiwa anasema hili.

Hivyo ili kuweza kuwa sawa na hii hali unatakiwa uikubali na kila kitu utaweza kucontrol kwa namna yake.

Jaribu kuelewa kwamba nguvu kama hii ni nzuri wala usiiangalie kwa ubaya kwa maana madhara kama haya yanavyo kutokea unajua ni jinsi gani unaweza kusolve,

3. Unaweza kuwa mtu asiye Muoga.

Yes, kwa wengi hii ukisema ni hasara wanaweza kuchukulia kama faida yenyewe. well katika wengi wenye kufungua jicho la tatu huonekana kuwa hawana woga wowote kwa maana wanajihisi ni wenye uwezo mkubwa na wana nguvu za miujiza teyari.

Japo ni jambo zuri lakini kama Crown chakra haifanyi kazi ni hatari kwa maana ukimuangalia mnyama anayekutisha unaweza kumtia kibao lakini kama Crown chakra haifanyi kazi anaweza kurudisha mapigo.

Ila kama Crown chakra inafanya kazi vizuri basi hata mnyama au mtu unaweza kumwambia kaa kimya au ondoka kwa sauti ya fikra nae akakimbia na kuogopa hata Simba pia.

Wengine hupima nguvu hii kwa wanyama wapole kama mbuzi na paka kwa kuwaangalia hadi damu kutoka mapuani au kuzirai kitu ambacho sio sawa na ni madhambi, hivyo ukumbuke usemi unaosema ukiwa na nguvu kuu basi uwe ni mwenye kuwajibika vikubwa na watu wasidhurike na uwezo wako.

Je, nini cha kufanya kuweza kubalance kutokuwa kwako muoga?​

Kwanza kabisa elewa ya kwamba kufungua jicho la tatu hakukufanyi wewe kuwa nabii ama mwenye ukuu zaidi kiasi cha kwamba unataka watu wakutii.

Pili, Angalia vema katika mtizamo wa Jicho lako la tatu unakushauri nini kuna na kiburi na mwisho wako utakuwa ni nini?

Mfano;
Jitahidi kuandika chini unachotaka kukifanya na uangalie je, ungefanyiwa wewe ungejihisi vipi? Hekima za kufungua jicho la tatu huwa nazo watu waliohimiri meditation vema ukifungua haraka na kutaka kupata nguvu haraka basi madhara ni makubwa kuliko faida.

4. Kutoka nje ya mwili​

Ikiwa bado hujajua kuhusiana na kutoka nje ya mwili basi rejea katika video nilizoelezea jinsi ya kutoka nje ya mwili na faida zake,

Unapotoka nje ya mwili basi unaacha mwili wako na kwenda sehemu nyingine. Ni jambo nilielezea ni faida lakini kwa hapa kwenye jicho la tatu ni hasara.

Mtu anaetoka nje ya mwili akiwa ni mwenye kufanya meditation ni tofauti na mtu mwenye kutoka nje ya mwili ikiwa kafungua jicho la tatu, pia ni tofauti na mtu anayetoka nje ya mwili hali ya kuwa hafanyi meditation wala hajafungua jicho la tatu.

Lakini vile vile jicho la tatu linapokuwa wazi na ukatoka nje ya mwili nguvu ya maono inakuwa kubwa kitu kinachopelekea muhusika kuanza kuona vitu zaidi ya yule anaetoka kwa hekima za meditation au yule anayetoka kwa bahati nasema anaetoka kwa bahati kwa maana unajikuta upo nje ya mwili bila kufanya mazoezi ya kiroho na hii mara nyingi huwatokea watu wengi wenye kufanya michezo ya hatari roho hujaribu kumwambia acha ujinga kuna kufa anapokuwa kalala.

Hivyo maono huwa makubwa ambayo hupelekea mtu kuanza kuhisi katoka nje ya mwili dimension gani?

Aisee kuna mengi ya kujifunza nitajitahidi kuwafunza vipindi vijavyo, kuna kitu kinaitwa dimension hizi ni vituo ambavyo mtu huweza kuaccess akitoka nje ya mwili na hii hutegemea na daraja la roho yake.

Kina roho mtakatifu amekuja ndotoni akanipeleka nikatembea Jerusalem hapa watakuwa wanaelewa namaanisha nini.

Yaani kuna vituo tofauti unapotoka nje ya mwili maarufu kama vituo vitatu cha kwanza ni kidogo cha pili ni cha kati na cha tatu ni kikubwa.

Tamaa ya kila mtu ni kufukia kikubwa lakini wengi wanaotoka huishia katikati ya kituo kidogo na kikubwa vituo hivi ni dunia hii hii isipokuwa ni kwa mtizamo wa roho yaani.

  • Ukitoka nje ya mwili unakuwa upo peke yako basi wewe umetoka cha kati,
  • Ukitoka nje ya mwili na umetolewa na jini basi wewe upo cha chini,
  • Ukitoka nje ya mwili na umepokelewa na malaika hichi ni cha juu

Break down ya hivi vituo ni;

  • Kwenye 1000 wanaotoka kituo cha kati ni 500,
  • Kwenye 1000 wanaotoka kituo cha chini ni 750,
  • Kwenye 1000 wanaotoka kituo cha Juu ni 1,

Nitakuja kuelezea vituo hivi kwenye video zingine.

Ili kuepuka uzito unapotoka nje ya mwili bila kutarajia Yes, bila shaka wengi waliofungua jicho la tatu hutoka nje ya mwili bila kutarajia.

Pia elewa jambo moja kwamba sote hutoka nje ya mwili tunapolala dini zinasema hili.

Sasa unapokuwa umetoka bila kutarajia basi moja kwa moja hapo hapo ukijua tu nipo nje ya Mwili jiambie hakuna kinachotisha nje ya mwili na pia hapa nilipo sina tofauti na nikiwa hai hivyo kila mtu na mambo yake.

Utakutana na jamaa wengi tu wa kibinadamu na kijini ukiwa nje ya mwili, usianze kupalikia watu kwa maana huko kila mtu anajaribu kuwa na experience yake tofauti.

Jiweke mwenye furaha ukiwa nje ya mwili ili roho yako iamke kwenye kujaza nguvu chanya ambayo itakufanya ujihisi upo in a wonderful Dimension otherwise ukirudi utaenda kusumbua mashehe na wachungaji wakuombee utoe pepo la kutoka nje ya mwili.

Mapepo yapo kweli lakini kwa hapa utakuwa umejibandikia mwenyewe,

Raha ya kutoka nje ya mwili ni sawa na kufumbua macho katika usiku uliyokuwa umelala hivyo chukulia hasara hii kama faida.

Ukiweza kumaster hili utafikia hatua nyingine ambayo ni hasara pia.

5. Jicho lako la tatu litakuwa na maono kupitiliza​

Jicho lako la tatu linapokuwa sensitive zaidi basi utakutana na changamoto ambazo nimezieleza hapo awali kwenye chakra ya 6 lakini pia nimeeleza kama tabia za mtu aliyefungua jicho la tatu yaani utapata tabu na utakuwa na uadui na mwanga mkali pamoja na sauti kali

6. Kuchanganyikiwa​

Moja kati ya hasara zinazoweza kukukuta ni kuchanganya mambo yaani unaweza ukaona jambo mtu analotaka kufanya kisha ukamwambia tulishaongea hili unalirudia na mtu anakuwa hajui mliongea wapi unajikuta unashindwa kutofautisha hali ya kiroho na hali ya kimwili

Ingawa haichukui muda utakaa sawa.

7. Tabia ya Machafuko/Vurugu​

Hii huwakuta wengi waliofungua jicho la tatu kabla ya Meditation, Kitu kidogo tu unaweza ukawa na hasira kupita maelezo kila mtu kwako anaweza kuwa mbaya na kila unaemuona unaona kama anakung'ong'a tu ama anakucheza shere unajikuta ni mwenye tamaa ya kukaa mbali na watu.

Ili kuweza kuepukana na hali hii unatakiwa ukumbuke kuwa fikra ya mtu sio maneno yake mtu anaweza kukufikiria vyovyote ama kukusema chochote katika akili yake la muhimu wewe jiliwaze kwa kusema binadamu ya kwao ni maneno na hakuna jema kwao.

Hii itakuumiza kwa kipindi fulani hasa ukija kuzingatia kuna watu unawaheshimu lakini fikra zao kwako sio nzuri na wanachokudhania ni mabaya na hata ufanye wema vipi watakuona hufai.

Vile vile utakosa raha kwa maana itaboost Clair audience yako na kukufanya usikie watu wakiwa mbali na wanakusema mabaya au kukudhania mabaya.

Fuatilia video hii kujifunza kuhusu Clair Audience https://youtu.be/hSr27z-mfsQ.

Utajikuta ni mwenye kujitenga na watu na kuishi peke yako.

Stahamili ni kipindi cha mpito baada ya hapo utawachukulia jinsi walivyo na utawasaidia baadae katika maisha wakikuhitajia.

Kwa leo tuishie hapa

ONYO
Si, ruhusa kunakili makala hii kwenye forums, platforms au tovuti nyingine nje ya muhusika na Jamii forums ipo chini ya uangalizi,

Hii ni haki kwa kunakili kwa wenye kutaka kujifunza tu kwa maana ni makala haijakamilika. Jihadhari na wenye kuloa.

Hii ni Rakims Spiritual Mpaka wakati ujao tena Asante.

Wasiliana nasi​

Ikiwa ni mwenye kupendezewa na makala hizi, basi jihisi huru kuendelea kutufuatilia kupitia Youtube channel yetu ya

https://www.youtube.com/@rakimsspiritual

lakini pia kama unahitaji mawasiliano yetu, tunapatikana kwa ajili ya misaada ya mfano wa makala hizi.

Unaweza kutupata kwa kupitia Email, nambari za simu,kupitia fomu ya mawasiliano katika tovuti yetu. Msaada wa kirafiki zaidi unatolewa na team yetu ya huduma kwa wateja na kujibu maswali yoyote ambayo unaweza kuwa nayo,

Ikiwa una maswali kuhusu makala zetu pia unaweza kuacha kwenye comment katika makala husika na kama ni huduma ya msaada wa tiba za kiroho au ushauri ama unahitaji kuagiza ama una suala lolote lingine basi tupo kwa ajili ya kutoa msaada pia.

Usisite kuwasiliana nasi kwa hekima za mawasiliano nifuraha yetu kusikia mahitaji ya wateja ama rafiki wa tovuti zetu za unajimu na rakimsspiritual na tunatoa huduma nzuri za kumridhisha mwenye shida ikiwa tu atakidhi vigezo vya kuwa mteja ama rafiki wa tovuti hizi asante.

Tahadhari
experience ya mtu na mtu ni tofauti kwetu

Na kwa maswali ya dharula kuhusiana na makala zetu kwa members pekee;

Jihisi huru kututafuta masaa 24 ya week kupitia

Email: Rakimsspiritual@gmail.com
WhatsApp: +255 783 930 601
Rakims
 
Mada zinazo wavutia masikini
Ila za kwako za vitendawili tega zinawavutia matajiri????

Kuna maskini wa pesa

Kuna maskini wa imani

Kuna maskini wa maarifa

Kuna maskini wa roho

Kuna maskini wa akili...

Wewe hapo ni maskini wa AKILI

Na hao unaowaona maskini ni vile hujielewi hata kidogo.
ndio maana unapost upumbavu...
Kwa mtu mwenye heshima na adabu hawezi kuona post yenye kumchafua kisha aka quote upumbavu mwenye kuquote upumbavu ni mpumbavu..

Na sifa unazojipa hao unaojilinganisha nao hizi thread ndio favorite zao...

Mtu akiangalia tu thread zako atajua ni kwa nini nimekuita mpumbavu

Username yako yenyewe inaonyesha ni Mpumbavu kiasi gani.!

Rakims
 
Ila za kwako za vitendawili tega zinawavutia matajiri????

Kuna maskini wa pesa

Kuna maskini wa imani

Kuna maskini wa maarifa

Kuna maskini wa roho

Kuna maskini wa akili...
Ungeishia hapa,

Na hao unaowaona maskini ni vile hujielewi hata kidogo.
ndio maana unapost upumbavu...
Kwa mtu mwenye heshima na adabu hawezi kuona post yenye kumchafua kisha aka quote upumbavu mwenye kuquote upumbavu ni mpumbavu..

Na sifa unazojipa hao unaojilinganisha nao hizi thread ndio favorite zao...

Mtu akiangalia tu thread zako atajua ni kwa nini nimekuita mpumbavu

Username yako yenyewe inaonyesha ni Mpumbavu kiasi gani.!
kwa kuendelea na hizi pumba, umekamilisha msemo wa:
"it is better to remain silent and be thought a fool than to talk and remove all doubt.

Hapa umejidhirisha ni mpuuzi mmoja, huna hili wala lile zaidi ya kusherehesha huu utumbo wa hekaya za kusadikika.

Na uko hapa kukamata wenye akili ndogo, na hizi tope zako wakufuate PM ukawapange na utupolo huu na kuwalia hela, wewe ni tapeli mpuuzi, bado unatumia njia za kizamani kula vichwa kwa sababu ya umasikini wa nchi husika na imani potofu ya kuwa kuna watu kama nyiyi mnasaidia jamii kwa mutumia miujiza isiyokuwepo wala kuthibitishwa na mtu yeyeto mwenye akili timamu, ni bora hata ya yule mpuuzi mwingine Mwamposa.

Miaka nenda rudi, unakuja na mada zako ni kilozi, watu wa aina hii, hamna faida kwa jamii, bali saratani ya maendeleo.

Dunia imeenda mbali sana kwa kipindi hiki, halafu bado unakuta kuna watu kama wewe kenge fulani unabwabwaja mataputapu yaliyotumika kwenye karne za giza.

Wewe ni useless bogus kwa jamii ya Tanzania, KEEP OUT AND STAY OUT.
 
Kwa mtu mwenye heshima na adabu hawezi kuona post yenye kumchafua kisha aka quote upumbavu mwenye kuquote upumbavu ni mpumbavu.
Na posti yangu ya kwanza kwenye hii mada, sija kuquote, ila wewe ndio umeniquote upumbavu wangu kwahiyo wewe ni mpumbavu wahedi, end off
Haya sasa nitupie hayo majini unayotishiaga watu humu, kenge wewe
 
Na posti yangu ya kwanza kwenye hii mada, sija kuquote, ila wewe ndio umeniquote upumbavu wangu kwahiyo wewe ni mpumbavu wahedi, end off
Haya sasa nitupie hayo majini unayotishiaga watu humu, kenge wewe
Mbona unatoka nje ya Mada? wewe ni Mpumbavu fahamu hilo ya kwamba wewe ni Mpumbavu jua hilo bado mapema kabla hujachelewa.. hakikisha ukikomaa uwe na akili nzuri maana Upumbavu utakupeleka pabaya sana hasa ukizingatia unaongea Pumba bado.
Haijarishi ni mwaka gani utakuja kurudia hii quote na kujiona wewe ulikuwa Mpumbavu kiasi gani. Ila ukumbuke tu huyu bwana mwenye hii makala aliniita Mpumbavu na uamini hivyo.
Sema ni bahati mbaya hata mjinga ukimwambia wewe ni Mjinga haelewi lakini ukimuita kila mara yeye ni Mjinga unakuwa uradi wake hivyo siku akipona anasema hakika nilikuwa mjinga.
Hivyo wewe ni MPUMBAVU you have a brain with 0.0001% IQ.
Believe me ipo siku utakuja jua.

Rakims
 
Mbona unatoka nje ya Mada? wewe ni Mpumbavu fahamu hilo ya kwamba wewe ni Mpumbavu jua hilo bado mapema kabla hujachelewa.. hakikisha ukikomaa uwe na akili nzuri maana Upumbavu utakupeleka pabaya sana hasa ukizingatia unaongea Pumba bado.
Haijarishi ni mwaka gani utakuja kurudia hii quote na kujiona wewe ulikuwa Mpumbavu kiasi gani. Ila ukumbuke tu huyu bwana mwenye hii makala aliniita Mpumbavu na uamini hivyo.
Sema ni bahati mbaya hata mjinga ukimwambia wewe ni Mjinga haelewi lakini ukimuita kila mara yeye ni Mjinga unakuwa uradi wake hivyo siku akipona anasema hakika nilikuwa mjinga.
Hivyo wewe ni MPUMBAVU you have a brain with 0.0001% IQ.
Believe me ipo siku utakuja jua.

Rakims

Kuanzia sasa kila nikikutana na hizi mada zako za kipuuzi, nakuanzishia, makende wewe
useless waste of space
 
Kuanzia sasa kila nikikutana na hizi mada zako za kipuuzi, nakuanzishia, makende wewe
useless waste of space
Search results

Bonyeza hapo utaziona zote, Tukana hadi uchoke lakini mimi na wewe sote tumekwisha fahamu kwamba wewe ni Mpumbavu na hata utukane vipi haitabadiri maana ya kuwa wewe ni Mpumbavu hivyo siku ukijua wewe ni Mpumbavu au ukichunguza kwa nini nakuita Mpumbavu wala usije kuniomba radhi lakini kumbuka kila atakae kuita Mpumbavu basi ujue kati yao mimi ndio nilikuita Mpumbavu kwa hekima sana na kwa lengo la kukusaidia kujitambua kuwa wewe ni Mpumbavu.

Rakims
 
Search results

Bonyeza hapo utaziona zote, Tukana hadi uchoke lakini mimi na wewe sote tumekwisha fahamu kwamba wewe ni Mpumbavu na hata utukane vipi haitabadiri maana ya kuwa wewe ni Mpumbavu hivyo siku ukijua wewe ni Mpumbavu au ukichunguza kwa nini nakuita Mpumbavu wala usije kuniomba radhi lakini kumbuka kila atakae kuita Mpumbavu basi ujue kati yao mimi ndio nilikuita Mpumbavu kwa hekima sana na kwa lengo la kukusaidia kujitambua kuwa wewe ni Mpumbavu.

Rakims
wewe ni mbulula
Hujui hata kuweka search results link,
Nimezipata hizi hapa, kazi inaanza sasa, mlozi kigagula wewe
Search results
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom