Kikwete: Waliochochea ukabila ndio wanachochea udini leo...

Status
Not open for further replies.
Kauli ya J.K kuwa kuna watu walijaribu kuwagombanisha watanzania kwa kutumia ukabila wakashindwa na kwamba sasa wanatumia udini ni ishara kuwa Mungu ameamua CCM wajiumbue wenyewe kwani CCM na wapambe wao walikuwa mstari wa mbele kuwahadaa wananchi kuwa kuna vyama vya siasa vya ukabila dhana ambayo ilishindwa kama JK mwenyewe alivyokiri jana na hili la udini aliloliasisi mwaka 2010 na kulilea kwa serikali yake kuachia mihadhara ya kukashifu kanisa ikifanywa nchi nzima bila kificho ili mradi pia wahubiri hao wakikisema vibaya CHADEMA. Rais na serikali yake ya CCM waliona hilo halina madhara bora CHADEMA inasemwa vibaya na wahadhiri hao. Leo anapokuja JK na kusema hayo anayoyasema huo ni UNAFIKI, nchi imefika hapa ilipo kwa udhaifu wake na upuuzi wa CCM.
Naomba watanzania tuukatae unafiki huu. Tulikataa kugawanywa na CCM kwa ukabila na sasa tusikubali kugawanywa na CCM kwa udini.
 
Huyu jamaa hajaumbuka. Ataumbuka zaidi hasa kama tutafanikiwa kuiondoa CCM ili yeye na wenzake waishie Keko kama siyo Segerea. Maana jamaa ameturudisha nyuma zaidi ya miaka 500 kutokana na uhovyo na ukilaza wake. Kwa sasa Kikwete hata hajui anachofanya zaidi ya kutapatapa na kujigonga. He is good for nothing so to speak. Uliona wapi rais mzururaji akawa na la maana kwa taifa lake zaidi ya kuleta aibu na hasara?
 
Udini,ukabila,ukanda na rangi.yote haya yatatokea tu maana hatuna cha kuwaambia wananchi wetu.jamani hali ni mbaya sana huko tuendako yatupasa kuwa na roho mgumu kama ya paka maana ukifika ule ubaguzi wa rangi ndio balaa kubwa maana hapa pana maslai ya watu tofauti na ubaguzi mwingine wa waswahili.
 
CCM na JK ni janga la Taifa hili!. Uwongo wao, wizi na ubadhilifu wao, Matumizi mabaya ya vyombo vya dola na madaraka wao, mauaji ya raia wasio na hatia wao. Hawa si binadamu sahihi. Lakini mwisho wao umefika. Muda si mrefu mambo yao yatakuwa historia na somo katika nchi zote za Afrika. Unafiki wao una mwisho.
 
Acheni hizo yeye kama Rais wa nchi alitakiwa aseme ni kina nani hao Walijaribu kutufarakanishakwa kutumia ukabila lakini hili lilishindikana na sasa wamegeukia dini ili tuwaogope kama CANCER. Tafadhali Rais wetu wewe ni Mkuu na Kiongozi wa Nchi wafichue Bayana hawa watu ili washindwe nia yao hii mbaya ya Hotuba za Chuki kila kukicha.

"The Only way of a Woman to hide a Secret is to refuse to tell who told it to her".
 
Mtu akiwa nyuma ya keyboard anajiamini.Jitokezeni hadharani mseme hayo maneno machafu machafu muone.Huu ni ushamba kutukana viongozi hovyo
 
Jk kama walivyo watanzania wengi upeo wake ni mdogo sana kwa hiyo mi sishangai.Kuna thread humu ndani inayosena ningekuwa mimi jk ningekimbia nchi.Jk ni rais ninatii urais kama kiti lakn siyo m2 bogus anayeitwa rais wa tz aliyeko madarakan sasa
 
Huyu jamaa hajaumbuka. Ataumbuka zaidi hasa kama tutafanikiwa kuiondoa CCM ili yeye na wenzake waishie Keko kama siyo Segerea. Maana jamaa ameturudisha nyuma zaidi ya miaka 500 kutokana na uhovyo na ukilaza wake. Kwa sasa Kikwete hata hajui anachofanya zaidi ya kutapatapa na kujigonga. He is good for nothing so to speak. Uliona wapi rais mzururaji akawa na la maana kwa taifa lake zaidi ya kuleta aibu na hasara?
Keko na Segerea hapana, Linatakiwa yale Magereza wanaponyea kwenye NDOO.

Mods ondoa huu UZI wa udini hawa chadema wanaeneza sana udini. wao ndio wanaendesha siasa kupitia makanisani wakiambiwa wanakataa lakini mwisho wake ni kuumbuka tu.
 
Mtu akiwa nyuma ya keyboard anajiamini.Jitokezeni hadharani mseme hayo maneno machafu machafu muone.Huu ni ushamba kutukana viongozi hovyo

mi nitafurahi matusi halisi yakiwa siku ya kupiga kura..........pale watu tutakapoamua kuachana na hawa viongozi wababaishaji.
 
Rais wetu anawajua wajua kwa majina wauza unga,wala rushwa, wachochezi wa udini na ukabila, nyie subirini tu, atawapa muda wa kujirekebisha kama alivyowapa muda watu wa EPA kuzirudisha pesa, Rais wetu safi sana.
 
Mods ondoa huu UZI wa udini hawa chadema wanaeneza sana udini. wao ndio wanaendesha siasa kupitia makanisani wakiambiwa wanakataa lakini mwisho wake ni kuumbuka tu.
Wakati sheikh Mohamed Issa, KUNDECHA, BASALEH, BUNGO, PONDA na wengine wanazunguka nchi nzima kutukana kanisa na kukisema vibaya kanisa na CHADEMA mbona mlikaa kimya bila kukemea?, mlikuwa mnakenua kwa kudhani ni mazuri. MOD pse acha ukweli usemwe na hawa wafitinishaji CCM waumbuke ikibidi siku moja wawaombe radhi WATANZANIA kwa hali hii waliyotufikisha.
 
jk kama walivyo watanzania wengi upeo wake ni mdogo sana kwa hiyo mi sishangai.kuna thread humu ndani inayosena ningekuwa mimi jk ningekimbia nchi.jk ni rais ninatii urais kama kiti lakn siyo m2 bogus anayeitwa rais wa tz aliyeko madarakan sasa
ya jk nadhani ina kati ya 0.01kb hadi 10kb ikzidi sana
 
Mods ondoa huu UZI wa udini hawa chadema wanaeneza sana udini. wao ndio wanaendesha siasa kupitia makanisani wakiambiwa wanakataa lakini mwisho wake ni kuumbuka tu.

Nilijua tu, angejitokeza mwanamagamba au "mshikaji" wao kama huyu CUF ngangari kuwatetea. CUF ngangari ana hasira za kuitwa "mchumba" wa CCM. Kwa posting hii amejitanabaisha si mchumba tu bali mke kabisa. Mwacheni aone uchungu jamani; mumewe aumbuliwe na yeye akae kimya?
 
JK ndiye muasisi wa siasa za udini tz. Alizianza mwaka 2010 baada ya kuona kuwa maji yamemfika shingoni
 
Kauli ya J.K kuwa kuna watu walijaribu kuwagombanisha watanzania kwa kutumia ukabila wakashindwa na kwamba sasa wanatumia udini ni ishara kuwa Mungu ameamua CCM wajiumbue wenyewe kwani CCM na wapambe wao walikuwa mstari wa mbele kuwahadaa wananchi kuwa kuna vyama vya siasa vya ukabila dhana ambayo ilishindwa kama JK mwenyewe alivyokiri jana na hili la udini aliloliasisi mwaka 2010 na kulilea kwa serikali yake kuachia mihadhara ya kukashifu kanisa ikifanywa nchi nzima bila kificho ili mradi pia wahubiri hao wakikisema vibaya CHADEMA. Rais na serikali yake ya CCM waliona hilo halina madhara bora CHADEMA inasemwa vibaya na wahadhiri hao. Leo anapokuja JK na kusema hayo anayoyasema huo ni UNAFIKI, nchi imefika hapa ilipo kwa udhaifu wake na upuuzi wa CCM.
Naomba watanzania tuukatae unafiki huu. Tulikataa kugawanywa na CCM kwa ukabila na sasa tusikubali kugawanywa na CCM kwa udini.

.
Jk tungemuona muungwana kama tu angeomba radhi direct ya kuligawanya taifa kiukabila/ukanda na udini badala ya kujaribu kuomba radhi indirect.
.
 
Nadhani ni raisi wetu aliyewahi kusema Wachungaji wanajihusisha ba biashara ya sembe-haram, mie nilishangaa sana kinywa Cha rais kufanya Kazi Za msemaji wa polisi lakini pia kwenda mbali Na kuachia kinywa chake kuwatenga watu wake watanzania Kwa misingi ya udini.. Kwanini asingesema wapo watanzania wanaofanya bizines hiyo?!,

Kumtamka kiongozi wa Dini au wadhifa wake kwenye mabaya ni udhaifu mkubwa Kwa kiongozi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom