Kikwete: Waliochochea ukabila ndio wanachochea udini leo...

Status
Not open for further replies.
watanzani wanasikitisha sana linapokuja suala la ku face reality.

Udini upo na umeshatugawa big time.Rohoni wahanga wanayo chuki,wana kutowaani watendaji wa maangamizi,na pia mitaani tunasikia watu wakisema vibaya dini nyingine.Na hii imekuwepo miaka mingi sana.

Labda niwashauri watu wanafiki na waoga ambao ni wabaya sana..kukiri tatizo ni ushindi tosha na sababu tosha litatua.Mfano,suala la ukimwi ,wagonjwa walipokiri na kujitokeza ukimya na unafiki ukakoma,madhara yakaoonekana. Kila kundi likaonekana lina waathirika.

Leo hakuna asiyeona na kujua nani anaua ,nani katukana dini na viongozi wa dini yake,angalau kwa eneo lake la kazi na eneo analoishi.Sasa hao ni watu wachache?Au ndio kutupooza tushuhudie mengi zaidi km ktk elimu,ktk madawa ya kulevya,rasilimali za nchi?yote haya yana mikono ya makundi yote.

Wanabodi mtanzania anayedai udini ni wa watu wachache hana tofauti na aliyesema mambo fulani ni upepo tuu. Hembu tujiulize km ni wachache na madhara yake ni makubwa na aibu hivi je wakiongezeka kidogo?ingawa ukweli ni kwamba kila mahali kumeoza udini.
 
kama kawaida yao.... Watu wachache wa udini hawawataji, waliorudisha hela za EPA hawawataji, magamba hawawataji, waharifu wa bandari list wanayo lakini hawawataji, wa meremeta hawawataji maana watatikisa nchi (kumbe kuna wenye nguvu kumshinda raisi), wa richmond hawawataji, wa Kibanda hawawataji, wa Dr. Ulimboka hawawataji, ..... Yaani hakuna wa kuwataja....
 
Inasikitisha kusikia kutoka katika kinywa cha mkuu wa nchi yetu kwamba hajui nini chanzo cha umasikini wa wananchi wake. Hii inaweza kuwa kweli, lakini je ni hatua gani madhubuti na mipango gani ya muda mrefu JK anafanya au ameifanya kuhakikisha tunaondokana na hali hii?

Soma hapa jinsi jirani zetu walivyo na vision katika kutatua hali hii. I hope JK na viongozi wake watajifunza.

Link: Paul Kagame: Rwanda and the New Lions of Africa - WSJ.com
 
Paul Kagame achana nae, tungempa tanzania, ndani ya miezi sita, tungeona tufauti kubwa, na ndoto ya maisha bora kwa kila mtanzania ingewezeka ndani ya miaka miwili tu!
 
Paul Kagame achana nae, tungempa tanzania, ndani ya miezi sita, tungeona tufauti kubwa, na ndoto ya maisha bora kwa kila mtanzania ingewezeka ndani ya miaka miwili tu!
Pole zao Watanzania, Utajikiaje ukipanda ndege afu ukushapaa hewani unasikia tangazo la Nahodha kwamba hajui kuendesha, wala anakokwenda wakati ndo ndege iko hewani? Maneno kama hayo aliwahi kuyasema Mh. Sumaye wakati anatoka kusoma degree yake kule Marekani "kwamba sasa ndo ninajua kwa nini Tanzania ni maskini kwa nini" Huyu alikuwa kiongozi mkuu wa shughuli za serikali Bungeni kwa miaka kumi. DU IKO KAZI TANZANIA
Tafakari!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kwa rasilimali tulizo nazo kama tungekuwa na uongozi dhabiti na wenye uzalendo wa kweli hakika tungekuwa nchi ya mfano Mashariki mwa Afrika kama sio Afrika nzima lakini ndio hvyo tena kama tuna viongozi wenye udhubutu wa kuwaita wananchi vyura sina hakika sana kama viongozi hao wanaweza kututoa hapo tulipo kwama licha ya tambo zao kuwa ni wasomi waliobobea na kujiona wao ni wajuzi wa kila kitu na wasio taka katu kutolewa kasoro.Safari ni ndefu na huko tuondako ni kiza kinene hakuna matumaini kwa vizazi vijavyo na rasilimali ndio hvyo zinazidi kuvunwa kila uchwao na kwa kasi ya ajabu huku wananchi wakiachwa katika lindi la umasikini.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom