Mwana Mpotevu
Platinum Member
- Sep 7, 2011
- 3,295
- 2,500
"Ndugu zangu, siku zote tumekuwa na dini zetu, kila mmoja akiwa na uhuru wake wa kuabudu anachokitaka na kukiamini na kwa namna anavyotaka yeye. Ni muhimu tuendelee kuheshimu tofauti zetu za dini bila kuzigeuza tofauti hizokuwa chimbuko na sababu ya ugomvi."
Jamani wana JF
Someni haya asemayo Kikwete sasa kuhusu udini na ukabila kisha mtafakari wenyewe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jana, Jumapili, Oktoba 28, 2012, ameanza ziara ya siku nne kukagua shughuli na kuzindua miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Kilimanjaro kwa kuwaambia Watanzania kuwa moto wa dini ambao umeanza kujitokeza katika Tanzania hautakuwa na mshindi.TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
JK: Moto wa dini hautakuwa na mshindi
Rais Kikwete ameanzia ziara yake kwenye Wilaya ya Same ambako amehutubia mkutano wahadhara kwenye eneo la Stendi ya Mabasi ya mjini Same ambapo amewaambia mamia ya wananchi kuwa baada ya watu wasioitakia Tanzania mema kushindwa kuwafarakanisha Watanzania kwa kutumia ukabila sasa wamegeukia dini.
Kuna watu hawana raha na utulivu na amani ya nchi yetu. Walijaribu kutufarakanisha kwa kutumia ukabila lakini hili lilishindikana na sasa wamegeukia dini. Lakinindugu zangu moto wa dini hautakuwa na wa kuuzima na hautakuwa na mshindi, Rais Kikwete amewaambia wananchi kwenye mkutano huo.
Amewataka Watanzania kuendelea na utulivu wao wa kidini na wakatae kufarakanishwa kwa tofauti za dini.
Ndugu zangu, siku zote tumekuwa na dini zetu, kila mmoja akiwa na uhuru wake wa kuabudu anachokitaka na kukiamini na kwa namna anavyotaka yeye. Ni muhimu tuendelee kuheshimu tofauti zetu za dini bila kuzigeuza tofauti hizokuwa chimbuko na sababu ya ugomvi.
Rais Kikwete pia amewahakikishia wananchi wa Same kuwa Serikali imedhamiria kumaliza tatizo la maji katika maeneo ya wilaya hiyo na wilaya za jirani za Mwanga na Korogwe katika Mkoa wa Tanga.
Amesema kuwa mradi mkubwa wa kusambaza maji katika vijiji 34 katika wilaya hizo kutoka Bwawa la Nyumba ya Mungu utaanza kutekelezwa Februari mwakani. Mradi huo wenye thamani za dola za Marekani bilioni 34 utawahudumia wananchi katika vijiji 14vya Wilaya ya Same na utachukua kiasi cha miezi 18 kukamilika.
Rais Kikwete ataendelea na ziara yake leo, Jumatatu, Oktoba 29, 2012 kwa kuzindua Kiwanda cha Tangawizi kilichoko Mamba Miamba na kufanya mkutano hadhara na wananchi. Baadaye kesho, Rais Kikwete atazindua Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Asha-Rose Migiro iliyoko Mwanga.
Imetolewa na:
Kurugenziya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu. Dares Salaam.
29Oktoba, 2012
My Take:
Hivi ni nani aliyekuwa anachochea ukabila kama sio CCM?? Kwahiyo na udini unachochewa na CCM? Je, JK anakishtaki chama chake kwa wananchi???
kumbe sheh ponda na farid nao ni cdm?
samahani usinishushie hasira pliiiiiiiizzzzZa kwake zipi? Asingedandia gari kwa mbele kama angalau angekuwa na za kwake kidogo tu!
Imetolewa na:TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Amesema kuwa mradi mkubwa wa kusambaza maji katika vijiji 34 katika wilaya hizo kutoka Bwawa la Nyumba ya Mungu utaanza kutekelezwa Februari mwakani. Mradi huo wenye thamani za dola za Marekani bilioni 34 utawahudumia wananchi katika vijiji 14vya Wilaya ya Same na utachukua kiasi cha miezi 18 kukamilika.
Kurugenziya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu. Dares Salaam.
29Oktoba, 2012
Mradi huo wenye thamani za dola za Marekani bilioni 34 utawahudumia wananchi katika vijiji 14vya Wilaya ya Same na utachukua kiasi cha miezi 18 kukamilika.
Salva naye atasema kateleza vidole?......dola bilioni 34? ama kweli ikulumawasiliano@yahoo.com