Kifo cha CCM kimetimia

Kadri siku zinavykwenda naona dalili zote za CCM kuanguka. Hakuna atakayeweza kuiokoa chama hiki kongwe. Naona anguko hilo litatokea ndani ya miaka kumi na tano (15). Watakaokingusha CCM ni wana CCM wenyewe, si vyama vya upinzani.

Zifuatazo ni dalili ya kuanguka kwa CCM
1. Upendo kati ya wanachama umekwisha, ni ugomvi usiokwisha ( Sitta camp Vs Rostam camp)

2. Fedha ni kipaumbele siyo Sera au hoja.

3. Wasemaji wa chama ni wapayukaji ( makamba, Hiza Tambwe, Sofia simba)

4. Wazee wenye busara wamesusa chama ( Warioba, Salim, Butiku, Sumaye)

5. Familia ya viongozi wamekiteka chama ( Makamba's, JK's, )

6. Kampeni zimebadilika kuwa concert ( wanamuziki kibao)

7. Kununua wapinzani

8. Kukataa midahalo ( mchakato majimboni- TBC)

9. Ahadi nyingi wakati huu wakati za mwaka 2005 hazijatekelezwa ( Mikopo ya wanafunzi maisha bora kwa kila mtz n.k)

10. Chama kujadili issue binafsi zaidi badala ya maslahi ya wananchi.

CCM kwa sasa ina uwoga sana kuliko cha chama chochote hapa nchini. Wanaelewa wanakoelekea.

Ilitabiriwa na maono yakaonesha miaka minne iliyopita "CCM inafia mikononi mwa Kikwete" Vilio vya wanyonge ambao magoti yao yameota sugu kwa kumwomba Mungu wao na Mungu ameyaona machozi yao. CCM inasambaratika. Mithali 24:24-25
 
Yaani hii nchi kila mtu anaamua tu kufanya kile anachoona kinamfaa yeye na familia yake si tumeona Marais wanaingia madarakani baada ya miaka 10 wanakuwa matajiri wa kufa mtu,Mawaziri tunawaona mitaani walivyokuwa wamechoka baada ya muda huwezi kuwaona tena maake wako juu ni mbya i mean wamekuwa matajiri hata kule kuwaona mpaka basi wanajiona wamefika Lol!!
Police wanauwa raia kama kawa na hakuna wa kuwazuia,watu wanauwa watu Albinos ati wapate utajiri na wauaji wanakamatwa na baadhi ya viungo lakini cha ajabu unasikia Mkuu flani sijui kamanda wa Police au DDp sifahamu ati wanaagiza mtu huyo aliyekamatwa na viungo vya binadamu aachiwe kwani hawezi kupelekwa koti mwee hii kali sana.Nilikutana na jamaa mmoja tuko kwa usafiri kaniuliza where are you from nikamwambia natoka Tanzania Lol!! ngoja maswali na hata wale ambao walikuwa jirani yete ngoja wanishambulie na kubeza Tanzania kwa mauaji ya Albino,Rushwa,Ukandamizwaji wa Demokrasia hasa kwa vyama vya siasa especilly Chadema kwa kweli nchi yetu imepoteza sifa sana tu najua mtaminyana kwa kukataa lakini ukweli ndo huo.
Nawakilisha mie mie
 
Acha kulalama tu,toa suluhisho basi tufanye nini ili tuondokane na hali hii
 
Hakuna ubishi kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeonyesha wazi kushindwa kutawala nchi yetu. Kimekuwa kinara wa auonevu na ufisadi huku kikifumbia macho makundi yenye ajenda za siri kupitia mgongo wa dini hasa uislam. CCM imefumbia macho matapeli wanaotumia majoho kuwaibia na kuwadanganya watanzania hasa kwenye madhehebu ya kikristo ambapo matapeli wa dhahiri kama Getrude Rwakatare, Sylvester Gamanywa, Kakobe, Lusekelo, Mwakasege na wengine wengi wamekuwa wakiwaibia watu maskini huku serikali ikiangalia ukiachia mbali kuwasamehe kodi katika biashara zao.
CCM imegawa na kuuza mali zetu bila kujali kuwa kuna kesho. CCM imeshindwa kuhimili matatizo ya muungano. Rais anakesha nje huku wasaidizi wake wakipigana vikumbu kutafuta rushwa. Imefikia mahali hata mbunge ambaye anapaswa kuwa mwakilishi wa wananchi anakamatwa na rushwa wazi wazi!
Hakika CCM inakufa vibaya na itatuacha pabaya tusipoingilia kati kuzuia jinai hii inayoiendekeza kwa faida zake.
 
Sasa hivi mtandao wa urais ndani ya CCM ni zaidi ya Alqaida, kwani karibu mafisadi wengi ni wenyeviti wa CCM wilaya/mikoa mf. Mudavida a.k.a ARV project
 
kunja ngumi kwa hasira zote halafu useme peoooples kisha kama hujajiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ujiandikishe kwa ajili ya kutengeneza maangamizi ya ccmabwepande
 
Nyieemu kwisha kwisha kabisa, ndio mahana mr prisedent" bongo hakukaliki. Sasa hii ni kali ya mwaka Ponda amekanatwa wafuasi wake wametinga kwa kishindo makao makuu ya Polisi kushinikiza kiongozi wao haachiwe kazi hiyo this year.
 
Tuna wajibu sawa wa kujenga na kuendeleza nchi yetu,hakuna mjomba wala shangazi atakae kuja kutusaidia kuondoka ktk dimbwi hili la matatizo,Serikali iliyopo madarakani imekuwa kiziwi sasa mambo yanapamba moto na kila mtu naloliamua yeye na familia yake ama halimashauri ya kichwa chake basi lifuatwe na kila mtanzania.kama mtanzania kazi ya kwanza niliyonayo ni kujikomboa kuanzia kichwani ili kujenga mtaji where i will be always free na from there ni kuhakikisha Sheria,Haki,Usawa na kila fursa inayojitokeza naitumia vema si kwa maslahi yangu bali kwa Taifa langu na kizazi kijacho kwa taifa.Im sure hakuna atakae thubutu kuchezea uhuru na haki zetu.
Viongozi wa chama cha mapinduzi pia wamechoka na hawajitambui,Lakini najua Mh.Nape atasaidia kuijenga CCM kuwa chama makini cha upinzani kwa muda mrefu.
 
Hivi yule bwn salva Rweyemamu mkurugenz wa mawasiliano Ikulu alienda wapi? Au alishaacha kazi!
 
Mungu akusaidie ndugu! hata siku moja usijaribu kuwakejeli watumishi wa Mungu kwa kuwaita matapeli! wewe u nani Mpaka uwaite matapeli!!! Usimtangazie Mungu vita kupitia watumishi wake kwa kuumusisha na CCM!!! bwana Mungu hajalala na hayupo tayari jina lake kuaibika atakuchapa
 
Tunahitaji raisi mwenye uthubutu wa kukemea anayetambua kuwa watz walimwamini awatetee ila yanapotokea naye kukimbilia nje, hiyo ziara ina ulazima gani, Raisi anakuwa busy pale kunapokuwa na uchaguzi ndani ya ccm tu, no its tooo much now brothers.
 
Kwenye orodha hujajitosheleza bila kumtaja mtume na nabii Josephat Mwingira yaani huyu jamaaa sema sio mpayukaji kama hao wengine jamaa ni bilionea kupitia matatizo ya watu eti anaowaombea kumbe anawaibia
 
Mijadala tu kila kukicha. Je 2015 mtaenda kupiga kura? Mnasema tu hapa i hope though Changes is coming
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom