Kifo cha CCM kimetimia

Stop dreaming and drink KoolAid!
CCM will win by a landslide on October 31st.
Love it hate it, CCM is the people's choice.
Let's vote CCM and help JK finishing what he has started. Go CCM

Ninahakika unasumbuliwa na laana au uko mbioni kulaaniwa kama unaweza kukaa ndani wakati unasikia kelele nje moto unawaka. Na hakika maneno yangu utayakumbuka, si mwanasiasa ni mwananchi wa Tz.
 
Kadri siku zinavykwenda naona dalili zote za CCM kuanguka. Hakuna atakayeweza kuiokoa chama hiki kongwe. Naona anguko hilo litatokea ndani ya miaka kumi na tano (15). Watakaokingusha CCM ni wana CCM wenyewe, si vyama vya upinzani.

Zifuatazo ni dalili ya kuanguka kwa CCM
1. Upendo kati ya wanachama umekwisha, ni ugomvi usiokwisha ( Sitta camp Vs Rostam camp)

2. Fedha ni kipaumbele siyo Sera au hoja.

3. Wasemaji wa chama ni wapayukaji ( makamba, Hiza Tambwe, Sofia simba)

4. Wazee wenye busara wamesusa chama ( Warioba, Salim, Butiku, Sumaye)

5. Familia ya viongozi wamekiteka chama ( Makamba's, JK's, )

6. Kampeni zimebadilika kuwa concert ( wanamuziki kibao)

7. Kununua wapinzani

8. Kukataa midahalo ( mchakato majimboni- TBC)

9. Ahadi nyingi wakati huu wakati za mwaka 2005 hazijatekelezwa ( Mikopo ya wanafunzi maisha bora kwa kila mtz n.k)

10. Chama kujadili issue binafsi zaidi badala ya maslahi ya wananchi.

CCM kwa sasa ina uwoga sana kuliko cha chama chochote hapa nchini. Wanaelewa wanakoelekea.


SIR R ULIKUWA SAHIHI KABISA. Ona JK mwenye dhamana ya kudnhibiti rushwa huku akiwa na all resources analia lia badala ya kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria tulizojiwekea.

This is shame......
 
Hivi CCM bado wanaamini kwamba..

1.wana hati miliki ya nchi hii pamoja na watz wote?
2.kwamba wanapendwa sana na watz pia wataendelea kushnda tukiwa na tume huru ya uchaguzi?
3.vyama vingine haviwezi kutawala nchi hii?
4.huwa wanashinda kihalali majimbo yote watz huwa wanawapigia kura,na walioshindwa eti wamewaachia tu wapinzani wakiamua wanachukua?

HAKIKA KAMA MUNGU AISHIVYO CCM MWISHO WAKE NI kati ya 2014 au 2015,japo hawataki kukubali ila naamini ma-ccm wenye akili timamu wameshasoma alama za nyakati kwamba enzi ya ccm imekwisha,nani aliamini kwamba KANU itakufa kirahisi hivyo?bt leo kiko wapi?ma-ccm machumia tumbo yamekalia kufikilia ni jnsi gani yataweza kuisambaratsha cdm ili yaendelee kutawala hata kama watz hawayataki na si kutumikia watz so sad,wameacha ilani wamebaki kuimba cdm na dr.slaa basi 2015 tukiwa na tume huru na daftari la wapiga kura likiboreshwa hata ma-ccm yanajua ndo mwisho wao.CCM OYEE?
 
Wana bodi,
Katika kila namna, kwa mtu yeyote anayeangalia mambo kwa kina atakubaliana na mimi kuwa kuna anguko kuu la CCM linakuja. Naweka majina ya wanaoratibu anguko hilo na majukumu yao katika kuhakikisha kuwa CCM inapotea kwenye ulimwengu wa siasa.


  1. JK - Akiwa Mwenyeketi wa CCM, ameshindwa kuwaondoa mafisadi kwenye chama (mapacha wawili waliobaki), ameshindwa kurudisha nidhamu ya chama (angalia matusi ya Nchemba na Kigwangwala), ameshindwa kusimamia utendaji mzuri kwa wabunge wa Chama chake (angalia wabunge wa CCM na Spika wao) na mwisho ameshindwa kusimamia utendaji wa mawaziri wa serikali ya chama chake.
  2. Phillip Mangula - Ni mzee hana mawazo mapya. Hata hivyo, alitoswa na JK hapo mwanzo kwa hiyo ni rahisi kuwahujumu.
  3. Kinana - Hana mawazo mapya na anajishughulisha na biashara haramu ya pembe za ndovu.
  4. Mwigulu Nchemba - Hana maono wala busara za uongozi. Kazi yake ni kutoa matusi kwa wapinzani badala ya kutoa hoja za kuelezea mazuri ya chama ili kukirudishia mvuto. Kwa akili yake finyu hajui kuwa anazidi kukimaliza chama. Amegeuka kuwa mwana propaganda za kizamani kazi ambayo ingefanywa na mtu mwingine (zamani Tambwe Hiza).
  5. Nape Nnauye - Ni mropokaji. Hajui kujenga hoja na sio mbunifu. hali hii imekuwa ikimfanya achukiwe na pia amekuwa anakifanya chama kikose kabisa mvuto kwa sababu hakuna jipya analofanya zaidi ya propaganda zilizopitwa na wakati na matusi kwa Dr. Slaa.
  6. Makinda na Ndugai - Wameshindwa kabisa kuendesha mhimili mwingine wa nchi yetu, yaani bunge. Unazi wanaouonyesha bungeni unazidi kuididimiza CCM kwa sababu sasa hivi wananchi wanaona na wameamka wanaweza kuchagua mchele ni upi na pumba ni zipi. Kwa kifupi hawa wanaizika CCM kwa kasi ya ajabu kuliko wengine.

Copy to: Ritz, Wingu & Zomba.
 
Mkuu Chigwiyemisi yaani wewe ndo unajua leo, mbona CCM ilisha jinyonga yenyewe mda kitambo tu, wananchi tunasubiri kuizika rasmi ifikapo mwaka 2015. Mie naona hao uliowataja wanazidi kurefusha kina cha kaburi la CCM.
 
Nawe, usiwe mbaguzi mh.Mizengo Pinda wa kupindisha issue, ambaye pia ni mwongo (kwa mujibu wa G.Lema) mbona hayumo kwenye orodha yako.

Pia, usisahau polCCM kuanzia igp hadi akina kamhanda wote wa mikoa na wilaya.
 
Hali ngumu ya maisha kwa watanzania pamoja na kuwa na rasilimali kibao ndiyo sababu kuu ya kifo cha ccm...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom