Halima Mdee ndiye Mtu Pekee aliyekuwa Sahihi kumpokea Uwenyekiti Mbowe

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,302
9,729
Ndugu zangu Watanzania,

Leo nataka niwapeni uchambuzi wangu na Elimu kidogo juu ya nani angefaa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA baada ya Mbowe kung'atuka uongozini na kuruhusu mawazo mapya na fikra mpya na mikakati mipya ndani ya chama kuchukua nafasi yake. Kwanza ni lazima tukubaliane kwa pamoja kuwa ni ngumu sana kuirejesha CHADEMA ile ya Dkt Slaa ya 2010-2015.pili ni ngumu kwa CHADEMA kuitikisa nchi tena na kuliteka kundi la vijana kama ilivyokuwa miaka hiyo.tatu ni ngumu sana CHADEMA kupata imani kubwa na kuwa na ushawishi mkubwa kama iliyopata kuwa nao kwa watanzania miaka hiyohiyo ya Dkt Slaa.

Miaka ambayo kuvaa tisheti na sare za CCM na ukakatisha nazo mjini kama pale Mbeya mjini au Tunduma ilikuwa ni ngumu sana, miaka ambayo katika uchaguzi wa serikali za wanafunzi vyuo vikuu vilitekwa na vijana wa CHASO, miaka ambayo CCM ilionekana ni chama cha wazee na cha watu wasio na Elimu, miaka ambayo msomi kuwa mwana CCM ilionekana kama wewe ni fisadi, miaka ambayo magwanda na kombati za CHADEMA zilitamba sana mijini,miaka ambayo CHADEMA mikutano yao ilikuwa inafurika watu pale Luandanzovwe pale Mbeya mpaka unahisi watu wameisha majumbani mwao.

Miaka ambayo CHADEMA iliteka na kuwa na ushawishi katika miji na majiji yote makubwa hapa Nchini,miaka ambayo CCM ilipata wakati mgumu sana kufanya mikutano yake mijini na kupata wahudhuriaji kama wale waliohudhuria kwenye mikutano ya CHADEMA. kwa hakika miaka hiyo haitakaa irejee tena kwa kuwa wananchi wameshatambua kuwa CHADEMA ni wababaishaji na wasakatonge tu na ndio maana wamekuwa vigeugeu na wasio na misimamo kwa mambo wanayoyasimamia ,na hapa unaweza rejea kilichotokea 2015.

Sasa turudi kwenye mada.napenda kuwaambia ya kuwa Mheshimiwa Halima James Mdee ndiye mtu pekee ambaye alikuwa anastahili na kuweza kuiongoza CHADEMA baada Ya Mheshimiwa Mbowe. sababu ni kuwa Mdee ni mtu aliyekulia ndani ya CHADEMA,ni mtu ambaye tangia ubinti wake amekuwa CHADEMA,hajawahi kuwa chama chochote nje ya CHADEMA,ni mtu ambaye anaweza endana na vijana ndani ya CHADEMA,ni mtu ambaye anakubalika na vijana wengi.Ni mtulivu na asiye na Papara.ni msiri na msatahimilivu sana.hapa unaweza kurejea namna alivyokuwa mtulivu katika kujibu majibu pale anaposhambuliwa na baadhi ya vijana kuhusiana na uwepo wake Bungeni kwa sasa.

Hana hasira wala jazba ndio maana majibu yake yamekuwa ya staha sana hata ukimfuatilia mitandaoni.ni mtu ambaye anakubalika hata nje ya chama chake,ni mtu ambaye anaweza watuliza na kuonyesha njia anaowaongoza bila kuacha mpasuko ndani ya chama.ni mtu mwenye staha,adabu,hekima, busara na muungwana sana.ndio maana huwezi kukuta akitoa lugha za matusi au kumsikia akiwatukana viongozi wa serikali au CCM Kama wanavyofanya waropokaji na wenye mihemuko kama Lissu au Lema au Heche .Mdee hana mihemuko wala kukurupuka wala kuropoka ropoka hovyoo, ni mtu mwenye nidhamu ya kinywa ,ulimi na mdomo wake.ni mtu mwenye muunganiko mzuri kati ya akili yake na mdomo wake na anajuwa wakati gani aongee na wakati gani akae kimya na wakati gani apuuze tu jambo na maneno yaliyoelekezwa kwake kama mshale..

Ni mtulivu sana tena sana.amejaa hekima,mcheshi, mkarimu wa maneno na mwenye kujuwa hasa namna ya kujenga hoja.ni mtu anayeweza kiungaisha chama vizuri sana kwa sababu anakifahamu vizuri sana na anafahamu wapi kimetoka na njia kilizopita.

Ikumbukwe ya kuwa CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani hapa nchini lazima kipate mtu aina ya Halima Mdee, ambaye anaweza kukaa hata na mtawala mezani kuzungumza kwa maslahi mapana ya pande zote mbili.unajuwa siasa za mabavu, kutunishiana misuli na kukimbizana na mabomu mtaani na hata kupelekea majeraha,vilema na hata vifo havina sababu na wala siyo siasa zinazohitajika kwa wakati huu. Kwa sababu zinajenga chuki, uhasama, uadui, visasi na kutokuaminiana na hatimaye kuligawa Taifa letu. Hivyo anahitajika kiongozi aina ya Mdee ambaye anaweza kuwa na kifua cha kuhakikisha kuwa siasa anazoziongoza ni siasa za maridhiano ,kukubaliana kutokukubaliana na kufikia muafaka katika meza ya mazungumzo.

Watu kama akina Lissu au Lema waropokaji,ikiwa CHADEMA ikarogwa ikawapa uwenyekiti ndio utakuwa mwisho wake kwa sababu watakisambaratisha na kukivuruga sana CHADEMA na kukiacha kikiwa hoi bin taabani juu ya mawe.

Nampenda sana Mheshimiwa Halima Mdee namna anavyofanya siasa zake,anavyojenga hoja kwa utulivu na ninatamani sana angekuwa mwana CCM na kuwa ndani ya CCM.

Lakini mwisho naomba kumkaribisha sana tena sana ndani ya CCM ,Chama ambacho ni mtetezi wa watanzania na kilicho dhamiria kuwainua Watanzania kiuchumi na kubeba matumaini yao. Naomba kama itampendeza ajiunge CCM ili aje aungane na Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania mama Samia Suluhu Hasssan katika kuwapigania watanzania. CCM ni mahali ambapo anaweza kutimiza ndoto zake za kuwasemea wananchi tofauti na huko kwa pinga pinga.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

IMG-20240201-WA0046.jpg
 
Hii ni sawa kusema Ali Karume ndio wa kumrithi dkt Hussen Mwinyi? Mdee si ashafukuzwa? Halafu unatumia muda mwingi wa kuandika vitu kama hivi
Huyu kula kulala bure ndiyo ana muda wa kuchezea kuandika haya magazeti yake yasiyokuwa na maudhui yoyote.
 
Naunga hoja ya mleta mada. Halima Mdee anafaa kuwa kiongozi wa juu nchini. Kuwa rais wa nch kwa kweli sina uhakika kamili lakini nadhani ana uwezo wa kufika akipata washauri wazuri. Kwa kuchukua nafasi ya Mbowe anafaa kabisa.
 
Baada ya kumuingiza kwenye chama la majizi ndio mnatamani apewe uongozi wa cdm? Kuliko cdm iongozwe na hao COVID ni Bora ife. Siasa za kujipendekeza pelekeni ACT, NCCR, CUF nk.
Mheshimiwa Halima James Mdee bado ni mwanachama halali wa CHADEMA na ndio maana kupitia yeye na wenzake chama kimepokea Riziki ya Billion mbili millioni mia saba.na bado kinaendelea kuvuta zingine ambazo ndio hizo zinakisaidia chama kufanya shuguli mbalimbali za chama.
 
Mheshimiwa Halima James Mdee bado ni mwanachama halali wa CHADEMA na ndio maana kupitia yeye na wenzake chama kimepokea Riziki ya Billion mbili millioni mia saba.na bado kinaendelea kuvuta zingine ambazo ndio hizo zinakisaidia chama kufanya shuguli mbalimbali za chama.
Kumbe wewe kilaza hata hujui hiyo ruzuku inakokotolewaje.
 
Wewe CHAWA umetumwa siyo bure!
Mtu aliyekubali kununuliwa huko awe mwenyekiti CDM?!
Alinunuliwa na nani? Unajuwa kazi aliyoifanya Mheshimiwa Mdee katika kuijenga CHADEMA? Hujuwi kuwa wakati wewe ukilala ndani na kuota unaoga porini Mheshimiwa Mdee alikuwa anapambania chama kwa jasho na Damu?
 
Hii ni sawa kusema Ali Karume ndio wa kumrithi dkt Hussen Mwinyi? Mdee si ashafukuzwa? Halafu unatumia muda mwingi wa kuandika vitu kama hivi
Bado ni mwanachama halali wa CHADEMA na ndio maana bado yupo bungeni na anatambulika kama mbunge wa viti maalumu wa CHADEMA.
 
Hii ni sawa kusema Ali Karume ndio wa kumrithi dkt Hussen Mwinyi? Mdee si ashafukuzwa? Halafu unatumia muda mwingi wa kuandika vitu kama hivi
Bado ni mwanachama halali wa CHADEMA na ndio maana bado yupo bungeni na anatambulika kama mbunge wa viti maalumu wa CHADEMA.
 
Haumtakii halima mema, mbowe ni dictator hawezi kuachia uenyekiti hata kwa kung'olewa na tingatinga
Mbowe ni lazima akubali tu kumuachia chama Mheshimiwa Mdee, maana muda wake umekwisha. 2015 aliahidi kuachia uwenyekiti lakini tunashangaa mpaka leo ameng'ang'ania tu kwenye uwenyekiti utafikiri sumaku.
 
Mheshimiwa Halima James Mdee bado ni mwanachama halali wa CHADEMA na ndio maana kupitia yeye na wenzake chama kimepokea Riziki ya Billion mbili millioni mia saba.na bado kinaendelea kuvuta zingine ambazo ndio hizo zinakisaidia chama kufanya shuguli mbalimbali za chama.
Huna ujualo kwenye siasa, ruzuku za CDM zinatokana na kura za urais alizopata mgombea wa urais, na huyo mbunge mmoja wa kuchaguliwa. Hao covid walifaidika na idadi ya kura za mgombea wa urais. Na ufahamu hao COVID walishafukuzwa cdm muda mrefu.
 
Back
Top Bottom