Joshua Nassari MB.

Daaaa kuna haja ya kuepuka siasa za majitaka kuepuka ya lusinde,mbona hoja za kuwashinda magamba ziko kibao tuu life lenyewe sio!!!
 
Kusema rais atoke upande gani haimaanishi kuwa unakata kipande cha nchi hivyo haiwezi kuwa sawa na kusema wewe unakuwa rais wa jamuhuri ya meru
utakuwa umekosea km ukiwa ni mwana CDM,WALE CHAKULA BARAFU WA Bagamoyo wapo siwa,AU HUJUI WALIKUWA NA RIZ1.
 
Daaaa kuna haja ya kuepuka siasa za majitaka kuepuka ya lusinde,mbona hoja za kuwashinda magamba ziko kibao tuu life lenyewe sio!!!
Tatizo kubwa ni kuchukuliwa baadhi ya maneno na kuanza kuhukumu na wengi wanaofanya hivyo wana malengo yao.
 
Kirlo wameru walimpeleka un kudai uhuru na mashamba yao mpaka leo bado kaburu anamiliki mashamba. Nassari ni mkombozi wa wameru MUNGU ibariki meru MUNGU ibariki Tz.
 
baada ya Nasari kumaliza kuhojiwa na kuruhusiwa kuondoka..Riz1 alimpigia simu Isaya Mngulu na kumtaka amkamate Nassari ndipo nasari akapigiwa simu na kuambiwa arudi kituo cha polisi...
Hebu tuhakikishie maana tuna hasira! tujue kama ni kweli huyu dogo alipiga simu yeye akiwa kama nani?
 
Hebu tuhakikishie maana tuna hasira! tujue kama ni kweli huyu dogo alipiga simu yeye akiwa kama nani?
Huyu riz1 amekuwa akiwatumia sana polisi wa Arusha pamoja na mkuu wa mkoa wa Arusha...anadai anachafuliwa kufatia maelezo haya " Ridhiwani Kikwete anao marafiki wa kike anaowatambulisha kwa baba yake Rais Jakaya Kikwete ambaye huwateua kushika nyadhifa mbalimbali kutokana na ushawishi wake."
 
Ni kweli mkuu hata mimi sikuyapenda matamshi ya dogo, ila nilijua hii kesi siyo serious sana kwa vile matamshi yametolewa wakati akifanya siasa, ingekuwa serious case kama matamshi yange rekodiwa sehemu ya siri.

Ila viongozi wa CDM lazima wawe waangalifu sana kwa kila wanachofanya, wajue polisi huwa wanazitumia sheria effectively hasa wanapodili na kesi za CDM, siyo kwamba polisi inawaonea CDM la bali wanakuwa na double standard kwa kosa lile lile linalofanywa na mwana CCM.

Mkuu umenena. Ni kweli kinachoudhi ni double standardization ya vyombo vya dola. Na haipo kwa CCM pekee bali pia kwa baadhi ya makundi fulani fulani ndani ya jamii. Polisi na vyombo vingine vya dola vina tabia ya kujifanya havioni au havisikii "upuuzi" unaofanywa na CCM na hayo makundi.

Mfano hai na wa hivi karibuni kabisa ni KIKUNDI CHA UAMSHO kule Zanzibar na mihadhara yao ya kutaka kuuvunja Muungano. Hivi matusi na lugha kali zinazozungumzwa kwenye mihadhara ya hawa jamaa na maneno aliyozungumza Mh. Nasari ni yapi ya hatari zaidi?

Mh. Nasari ni mwanasiasa na alizungumza akiwa kwenye mkutano wa kisiasa lakini hawa jamaa wa UAMSHO sio wanasiasa na mikutano yao sidhani kama ni ya kisiasa; well this is not a big problem; tatizo ni ujumbe unaotolewa kwenye mikutano yao.

Doble-standadization ni miongoni mwa characteristics za dola ya kifisadi ambayo kwa kawaida hushindwa kusimamia sheria kwa ukamilifu wake. Hiyo ndio Tanzania.
 
Huyu riz1 amekuwa akiwatumia sana polisi wa Arusha pamoja na mkuu wa mkoa wa Arusha...anadai anachafuliwa kufatia maelezo haya " Ridhiwani Kikwete anao marafiki wa kike anaowatambulisha kwa baba yake Rais Jakaya Kikwete ambaye huwateua kushika nyadhifa mbalimbali kutokana na ushawishi wake."

Wanasiasa wajanja, kutegemea aina ya ujumbe, mahali, na hali halisi hawawataji kwa majina yao moja kwa moja. Angeweza kueleza tu kwa mafumbo na akaeleweka na kila mtu na isiwe na madhara yoyote kisiasa kwake au chama chake. Mfundisheni huyo dogo siasa; aache munkari usio na sababu.
 
Amekana kuwa hakusema Arusha itakuwa kama Sudani Kusini. Anawaomba Watanzania wamwelewe vizuri na kama kuna watu amewakwaza kwa kuelewa kauli vinginevyo wamsamehe. Atarudi polisi kesho. Source Sunrise Radio. M4C Aluta continua!
 
Policcm bwana yani wanampa mtu presha utafikili kaua!! Kama rais tu mbona hata manzese kuna rais?
 
Kwanini aende akasemee plosi?
kwani hayo wanayo dai amesema aliasemea polisi?
 
Siasa siku hizi ni Maneno ya mtaani tupu yasiyokuwa na maana, maneno ya kawaida kaongea Nasari mnashikia bango mbona Mkapa, lusinde, Wassira wakiongea hamsemi? R1 angekuwa mtoto wa Dr. Slaa au Mbowe ingawa CDM haijachukua dola leo mngepigaje mdomo? Nawaambieni Kujitenga KUPO
 
hao wamechoka kufikiri lakini watu wa Biafra walipoona wananyanyaswa na serikali ya Nigeria waliamua kupigana vita ya kutaka kujitenga na NYERERE aliitambua serikali yao
TAFAKARI CHUKUA HATUA
 
Japo sipendi kauli zilizotajwa na Dogo Janja, kwenye debate nyingi nimegundua kanda ya kaskazini ni lulu ya Tanzania.
Tatizo kubwa ni kuchukuliwa baadhi ya maneno na kuanza kuhukumu na wengi wanaofanya hivyo wana malengo yao.
 
Back
Top Bottom