Joshua Nassari MB.

Haya ni baadhi tu maneno machache ya Mbunge Joshua Nassary ktk mahojiano yake na polisi baada ya kujisalimisha.
Kasema hivi" Mimi sikuwa na nia mbaya juu ya kauli yangu bali ilikuwa ni kutoa hamasa ya mabadiliko kwa mikoa mingine iige Arusha,Mbeya,Musoma,Manyara, kwa mabadiliko walioonyesha pia Mimi ni mtu mdogo sana ktk nchi hii so sina mamlaka ya kumzuia Rais kuja Arusha wala sina uwezo wa kuigawanya nchi kwani kama ni kweli mm ninaweza kuigawanya nchi na kumzuia Rais basi HIYO ITAKUWA SIYO NCHI WALA HAIPASWI KUWEPO maana mi ni mtu mdogo sana"
 
Polepole na mdomo wako Mh. Nassari. Kuna njia nyingi na pengine bora kuliko unazotumia muda huu (hasa kwa wiki hii) ambazo zinaweza kuleta ukombozi, haki na ustawi kwa wananchi wa Tz.

Nakupa benefit of doubts. But plz try and learn quickly so that you may rightfully play role-model mantra.

Nimeipenda sana hii Comrade umetoa elimu ya juu sana,nchi tushaiweka mikononi mwetu sasa taratiiibu kuelekea Ikulu cha msingi tusiache majeruhi wengi sana
 
hahahahaaaa! nchi hii bwana ukijua kucheza na akili za wajinga tu basi,mtoto mdogo anawagaragaza watu na vitambi vyao,mvinyo haunyweki,safar haziendeki."kosa vyote ukipata akili vyote vitajileta vyenyewe"
 
Huyo ndo dogo janja, duuuh! Dogo kacheza na ngeli kweli kweli! Big up
 
Kikwete na timu yake ya jeshi la polisi wanawatambua Lema na Nassari kama watu tishio kwenye utawala wao.
 
Amesema jambo ambalo kwa haraka linaonekana lina mantiki lakini linapuuzia uzito wa alichokisema. Kama ni mtu mdogo hivyo aligombea ubunge wa nini? Kama anakosa hekima ya kupima madhara ya maneno yake - watu wanaweza kuumia kwa kauli moja tu ya mtu mwenye ushawishi - kwa sababu yeye ni 'mtu mdogo' ananitisha. Yeye anaweza kuwa na umri mdogo lakini nguvu ya ushawishi wake inashinda baruti na siyo watu wote wanaomsikiiliza wanamchukulia kuwa ni mtu 'mdogo'. grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
 
Naanza kudoubt uwezo wa huyu kijana umbile la mtu haligawi nchi bali maneno ya mtu.Mimi naona bora anyamaze mambo ya poe kwanza.Mbowe mwambie afyate mdomo huyu kijana.
 
Kwa kweli kucheza na mjinga sio kazi kama polisi wameweza kutumia masaa sita kumhoji Nassari kweli hatuna jeshi la polisi bongo mana mambo kama haya ndo wanaweza kushadadia,Lusinde matusi ya nguoni alitukana wapi kama sio Arusha?au matusi sio uchochezi?mnaboa sana polisi wa bongo.:hat:
 
hivi hawa polisi wanawasikia cdm tu,yale matusi ya lusinde haukuwa uchochezi craaaaaaaaaaaaaaaaaaap
 
hapa "siasa" ikitengamishwa na "maisha halisi" itakuwa rahisi sana kumwelewa dogo joshua.......!

joshua bado hajaelewa kwamba "siasa" ni sanaa...and full of protocals!..

nyie wazee hapa jf elewen kwamba "tumewachoka".....mnamfelisha nassary kijinga sana...wote ni members humu....nassary ameongea gani mbaya zaidi ya lusinde?????......tumieni akil kidogo ninyi wazee....hii dunia si mliyoiishi....

long live nassary....!
 
Kama hawa polisisiem wangekuwa na weledi wangefanya uchunguzi kidogo tu tena kwa gharama nafuu na kugundua kuwa Joshua Nassary is not a threat. But kwa kuwa wametumwa na Riziwan na hawana ujanja wa kukataa amri ya mwana mfalme wamejikuta wanampa publicity nyingine dogo janja. Come on polisi, mkitumwa muwe mnachanganya na akili zenu sio kukubali kubali tu kila Riziwan anachosema kumbukeni kuwa 2015 sio mbali
 
Amesema jambo ambalo kwa haraka linaonekana lina mantiki lakini linapuuzia uzito wa alichokisema. Kama ni mtu mdogo hivyo aligombea ubunge wa nini? Kama anakosa hekima ya kupima madhara ya maneno yake - watu wanaweza kuumia kwa kauli moja tu ya mtu mwenye ushawishi - kwa sababu yeye ni 'mtu mdogo' ananitisha. Yeye anaweza kuwa na umri mdogo lakini nguvu ya ushawishi wake inashinda baruti na siyo watu wote wanaomsikiiliza wanamchukulia kuwa ni mtu 'mdogo'. grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
Hapa mimi sikubaliani na wewe kabisa. Udogo anaomaanisha Nassari ni wa yeye kuigawa nchi. Najua hata wewe unajua Nassari hana uwezo wa kuigawa nchi kwa sasa. Na hana maana kwamba kila siku atakuwa mdogo. Haya maneno kayatamka leo lakini haina maana kwamba atakuwa mdogo na kesho pia
 
Amesema jambo ambalo kwa haraka linaonekana lina mantiki lakini linapuuzia uzito wa alichokisema. Kama ni mtu mdogo hivyo aligombea ubunge wa nini? Kama anakosa hekima ya kupima madhara ya maneno yake - watu wanaweza kuumia kwa kauli moja tu ya mtu mwenye ushawishi - kwa sababu yeye ni 'mtu mdogo' ananitisha. Yeye anaweza kuwa na umri mdogo lakini nguvu ya ushawishi wake inashinda baruti na siyo watu wote wanaomsikiiliza wanamchukulia kuwa ni mtu 'mdogo'. grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr

Hakuna chembe ya mantiki hapo hata kidogo ndugu yangu! Amefanya kosa then analeta mzaha. CHE GUEVARA alikufa akiwa na miaka 38, ndani ya muda huo mfupi akawaadabisha mabepari wakubwa kama Marekani.
Kwanza ni kujidharirisha mwenyewe, anajifananisha na mtoto asiyejua jema na baya, hali lukuki ya wana-arumeru wana tumaini naye? Anataka waamini wamekosea kumchagua?
1. Akiri kuteleza ulimi, na kuomba radhi, ni jambo la kawaida sana, sisi kama watz tuko tayari kumsamehe, na ajipange upya, tuko nyuma yake.
2. Chadema itoe tamko la kulaani, na kutoa karipio kwa maneno hayo. Na sio kuishia kusema "hayo sio maneno ya chadema", kwani ametoa nani na wapi?
3. Asipokubaliana na yote hayo, basi chdma kama chama makini, kisisite kumuwajibisha. Lakini sitegemei kufikia huko!
Mungu wetu anaita?
 
Back
Top Bottom