Joshua Nassari MB.

Mbona mdomo wa Jk hauna brake?
Unadhani tulisahau Jk alipowatishia wafanyakazi kuwa wakileta nyokonyoko watakutana na nguvu ya dola, tena akasema hizo bunduki siyo mapambo zinaua.
Inabidi dogo mdomo wake uwe na brake
 
hivi kauli kwamba Rais ajaye hawezi kutoka kaskazini na kuwa jina la rais huyo analo JK haiwezi kuleta uvunjifu wa amani na sio kauli ya uchochezi mbona hakuna aliyehojiwa???

Mkuu

Ilikuwa ni kauli ya hatari sana ile. Watakwambia familia ya rais haihusiki, haijawahi kutoa kauli yoyote tata ya kuchochea vurugu na uvunjifu wa amani wala haina mpango huo kamwe maishani.

Double standards za wazi zinazofanywa na waliokabidhiwa dhamana itazidi kuongeza chuki mioyoni mwa watu dhidi ya watawala, Liko wazi hili halina ubishi.
 
hivi kauli kwamba rais ajaye hawezi kutoka kaskazini na kuwa jina la rais huyo analo jk haiwezi kuleta uvunjifu wa amani na sio kauli ya uchochezi mbona hakuna aliyehojiwa???

hiyo wala hawajawahi sikia labda angesema mtu wa cdm wangesikia
 
Mh. Nassari ameongea kwenye taarifa ya habari ya saa mbili kwenye kituo cha ITV na kusema kuwa kama Tanzania inaweza kugawanywa na kauli za mtu mdogo kama yeye basi hii nchi haipaswi kuwepo kwani inakuwa nchi isiyokuwa na msimamo..............
 
Dogo Janja bana!
Safi sana kamanda!
Mh. Nassari ameongea kwenye taarifa ya habari ya saa mbili kwenye kituo cha ITV na kusema kuwa kama Tanzania inaweza kugawanywa na kauli za mtu mdogo kama yeye basi hii nchi haipaswi kuwepo kwani inakuwa nchi isiyokuwa na msimamo..............
 
hiyo wala hawajawahi sikia labda angesema mtu wa cdm wangesikia

Na hapo ndipo CCM inapowazidi ujanja. Haikusikika kwa sababu CDM hawakutaka iwe hivyo wakati ilikuwa turufu muhimu sana kisiasa kwao.

Walitakiwa wai-propagate to the maximum and as soon as possible; kwa wanojua siasa huo ndio mchezo wa kisiasa - yaani hiyo ndio siasa yenyewe - kuonesha udhaifu wa mwenzio kwa faida yako.

Ndicho wanachofanya Nape na watu wake lakini chances muhimu kama hizi zinapotokea utashangaa CDM kimya!
 
Alafu ilikuwa je lusinde nae hakuhitajibu kuhojiwa maana yeye aliropoka yale ya ndani ya ndani ya nguo ya ndani


Double standards mkuu, zitaua nchi hii. Umeona mtu mwingine ametoa mfano wa ile kauli iliyowahi kutolewa na wale vijana wa Pwani chini ya usimamizi wa mwanafamilia wa familia kuwa rais ajaye hatatoka kaskazini. It was pure hate speech, incitement...
 
INGAWAJE MABADILIKO YA KWELI NDANI YA NCHI HII KITOVU CHAKE A-TAUNI, TSUNAMI LA KISIASA LITAKALOLIFUNIKA KABISA CCM NA MAFISADI WAKE SASA MIKONDO YAKE KUKUTANIA IDODOMYA

Wanabodi bado nakumbuka; Wanaharakati tulipoanza wengine walitubeza, CHADEMA ilipoanza kuwakabili sana MAFISADI kwingineko chama chetu hiki kikapata kubatizwa jina 'Vyama vya Msimu',

na hivi sasa, kwa kuwa CHADEMA imebadilika na kuwa zaidi ya msumari wa moto kwa MAFISADI hao hao na kwa jinsi hiki chama cha Rostam Aziz kinavyoendelea kuzama fasta ajabu kwa Kimbunga Cha Lema wenzetu sasa wanatukaba kwa kuua wanachama wetu.

Hebu mwenzenu mwachieni Mh Nassari akahimize kitu Utaifa mbeeeele kama tai LAKINI katika kweli, heshima kwa utu wa Mtanzania katika mazingira ya HAKI na HAKI tu na wala si kwa kutegemea tabasamu katika uso wa rais wa nchi na viongozi maswahiba wake!!

Naam, japo ni kweli mabadiliko ya kuikomboa nchi hii yalianza rasmi na ule umwagaji damu kule A-Town lakini hivi sasa Tsunami ya kisiasa yaja kutoka kanda ya Ziwa
(Bukoba, Mwanza, Mara na Shinyanga) ...

... na hivyo kuja kukutana na ule mkondo wa Kanda ya Juu Kusini
(Njombe, Mbeya, Iringa, Songea) na siku zitakapokutania pale katika Jiji la Idodomya basi hapo hapo ndipo CCM pamoja na MAFISADI wooote watakapoDIDIMIA kimoja na kusahaulika na historia hata kabla ya 2015.

Habari ndio hiyo wanabodi kwa wale waliodhania kwamba kimbunga CHADEMA ni kule kaskazini tu.
 
Mh. Nassari ameongea kwenye taarifa ya habari ya saa mbili kwenye kituo cha ITV na kusema kuwa kama Tanzania inaweza kugawanywa na kauli za mtu mdogo kama yeye basi hii nchi haipaswi kuwepo kwani inakuwa nchi isiyokuwa na msimamo..............

Na hapa ndipo CDM mnapozidi kukosea! Hivi unadhani CCM hawajui hilo? Wanajua tena vizuri sana kwamba kauli kama hizo hazina madhara yoyote kwa taifa - they know very well.

Kosa mnalofanya ni kusahau kwamba CCM ni mabingwa wa kugeuza maneno na kwa turufu ya uelewa finyu wa wananchi hutumia hata mambo ya kipumbavu "yasiyokuwepo" kwa faida za kisiasa ambayo at the end losers inakuwa CDM!

So, even though they were/are so insignificant, ni muhimu kuepuka hila zozote kadiri inavyowezekana. Asiwe mbishi.
 
Polepole na mdomo wako Mh. Nassari. Kuna njia nyingi na pengine bora kuliko unazotumia muda huu (hasa kwa wiki hii) ambazo zinaweza kuleta ukombozi, haki na ustawi kwa wananchi wa Tz.

Nakupa benefit of doubts. But plz try and learn quickly so that you may rightfully play role-model mantra.
 


Double standards mkuu, zitaua nchi hii. Umeona mtu mwingine ametoa mfano wa ile kauli iliyowahi kutolewa na wale vijana wa Pwani chini ya usimamizi wa mwanafamilia wa familia kuwa rais ajaye hatatoka kaskazini. It was pure hate speech, incitement...

Makene msiishie tu kulalamika. Kama kauli hiyo ilwahi kutolewa na mtu mzito na nyie mkaa kimya basi mjilaumu wenyewe. Mlishindwa kuitumia "chance" muhimu kama hiyo kwa faida za kisiasa - ndicho wanachofanya CCM kila sikuuuuuu!!!!!

Jambo lolote hata kama lingekuwa dogo vipi alimradi linaweza kuwa "fabricated" CCM wanalitumia barab'bara. Jifunzeni na acheni kulalamika kila siku.
 
Back
Top Bottom