Joshua Nassari MB.

Naona hawa ni ccm tu na mbinu zao nyingi za kuendelea kuwafanyia visa wabunge wetu wa Chadema, ili wakose muda wa kwenda bungeni. Kujadili mambo ya msingi yanayohusu wananchi na kuwahumbua mafisadi, ili wabaki kutafakari kesi sizizo na msingi na muda uende
 
hotuba ya Nassari pale NMC ililenga kulaani mauaji ya mwenyekiti wa CDM Usariver, ambayo hayaja shughulikiwa ipasavyo. Kuna wabunge wa CDM walicharangwa mapanga, na jeshi la polisi lipo kimya. Nassari alitishia kujitenga au kumpiga raisi marufuku, lakini uchambuzi wako wenye "MANTIKI" na wengine wengi mnachambua kama kwamba tayari ameshatoa tamko rasmi la huko kujitenga! Alisema KAMA, polisi wasipo shughulika kuwapata wauaji na kuwachukulia hatua.... Labda hatuna "MANTIKI", tunaongozwa na hisia na ushabiki, lakini nashawishika kuamini kwamba Nassari alisukumwa na mauaji ambayo yana sura ya visasi vya kisiasa na ubutu wa polisi kufanya kazi yao kutoa kauli tunazotumia kumhukumu. Ndo maana naomba tuangalie context kabla ya kufanya hitimisho la uchambuzi wa maneno.
Mimi ni mfuasi na muumini wa Mungu aliye hai, na jina langu hapo juu ni halisi, and I gave you my number. Sina unafiki, na siyo mwanachama wa CDM, lakini naijua haki na ntasimama kwenye haki tu.

Usituhukumu ndugu...
Tunachomshutumu Nassari ni kutoa kauli ya uchochezi dhidi ya watz na utaifa wao, labda alifikiria kumgusa JK tu, lakin ukweli raia imewatisha pia! Sijasema ametoa tamko. Yeya kama kiongozi, kuna kauli anapaswa kuzkwepa kabisa. Akiwa mwerevu atakiri kuwa ameteleza, nasi tutamwambia "kuteleza sio kuanguka kaka, kaza buti mlima tupande", lakini kama ataendelea kujitetea kitoto, basi kutakuwa ndio kuanguka kwake! Mimi na umri wangu mdogo, na elimu yangu ndogo, nisingeweza kutamka maneno yale! Labda ni kwa ujinga wangu!
Kinachonikera kingine ni kila anayejaribu kutoa maoni ya kumpinga Nassari basi ni gamba, matusi, kejeli, nk. Hata Mwanakijiji leo ameshutumiwa kutokuwa na akili. Swali... Je, tunajenga au tunabomoa? Watu wanaichukia ccm kwa mambo hayo, kwann chdm isiyakwepe? Mtu anajenga hoja, eti mbona fulani wa ccm alitukana, ndio nini sasa? Inamaanisha dhambi ikishatendwa na ccm, inabadilika kuwa baraka kwa wengi kuiga?
Mungu wetu anaita! Calling his sons from exile. africanandnottanzanian.
Mungu wetu anaita!
 
Alichoongea Nassari hakina tofauti na alichoongea Jussa, au wanachoongea wana-uamsho kule Zanzibar
 
Kwa taarifa tu, mh. Nassari aliomba msamaha kupitia Radio Sunrise juzi jioni baada ya kutoka Police Central.
Alipigiwa simu na kufanyiwa mahojiano ambapo alikiri kuteleza nami kwa kweli sikurekodi ila kilikuwa kipindi chao (Sunrise) maarufu cha kuanzia saa 2 usiku cha matukio ya siku. Sasa kwa ushauri wangu/wetu angejitokeza humu JF. aombe msamaha kwani ile radio haisikiki nchi nzima. Kuteleza sio kuanguka.
 
Kwa taarifa tu, mh. Nassari aliomba msamaha kupitia Radio Sunrise juzi jioni baada ya kutoka Police Central.
Alipigiwa simu na kufanyiwa mahojiano ambapo alikiri kuteleza nami kwa kweli sikurekodi ila kilikuwa kipindi chao (Sunrise) maarufu cha kuanzia saa 2 usiku cha matukio ya siku. Sasa kwa ushauri wangu/wetu angejitokeza humu JF. aombe msamaha kwani ile radio haisikiki nchi nzima. Kuteleza sio kuanguka.

maandiko matakatifu yanasema akitubu msamehe,hata kama alikukosea mara 7.Na akaja x7 kutubu msamehe.ARUSHA 1,Katueleza dogo ametubu na kuomba msamaha kupitia Sunradio ya A.town,AJE ajioshee na hapa kwa Wakuu maana hiyo radio haifiki mikoani.
 
hebu jamani mwenye rekodi/ aliye rekodi maneno hayo ya joshua nasari siku ya mkutano atuwekee hapa tuyaone wengine tuko blank kabisa na nini kilitokea. mtuwie radhi laakini
 
Alichosema wala hata siyo mambo ya kaskazini, ingawa nilikuwa mkutanoni na nilirekodi ila kwa kweli kabla mh. MBOWE hajasimama na kuhutubia wale senior leaders MC wa siku ile aliwapa ten minutes each including baadhi wa wale waliovua gamba; ilipofika zamu ya mh. Nassari alianza kulaani mauaji ya m/kiti wa Usa River then ugawaji wa mashamba ya wameru kwa settlers, then akalaani kujeruhiwa kwa wabunge Machemli na Kiwia kule Mwanza na kunyanyaswa na kunyimwa maendeleo kwa sehemu ambazo kuna wabunge wa Chadema na hasira zilipompanda ndio akasema lile NENO. Kuwa anaweza kuamua kuwa wasifike Arusha Pinda na Kikwete. Akaendelea kwa kusema kama hawaleti maendeleo sehemu hizo, kuanzi Kilimanjaro Arusha Manyara Musoma Mwanza Shinyanga na Kagera zijitenge kwani zina milima Kilimanjaro, Meru Hanang na hifadhi za wanyama za Arusha, Manyara, Tarangire, Ngorongoro na Serengeti ambazo zina uwezo wa kuingiza kipato cha kutosha kuwaletea maendeleo watu wa sehemu alizotaja pamoja na ziwa Tanganyika na Victoria kwa mikoa ya kule kuwa yana samaki wa kutosha kuuza nje na kuwapa maendeleo. Kwangu mimi nadhani dhamira yake ni kuishtua serikali kuhusu kutoa huduma bila kubagua hapa ni chama gani kinaongoza. Kwa kuwa sehemu zote alizotaja kuwa zijitenge zina ardhi watu mifugo na rasilimali za kutosha so ingekuwa busara kwa watawala wakafuata maneno aliyowahi kusema mh. ZITTO kuwa jimbo ambalo lilichagua upinzani mpango wa maendeleo ufuate sera za maendeleo za taifa na siyo sera za CCM. Kiongozi mkuu wa taifa lolote anapaswa kupeleka huduma nchi nzima bila ubaguzi wa kisiasa ili kuepusha mambo kama ya juzi kutokea tena. Natoa mfano mdogo tu kuhusu uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki uliompa ubunge Mh. Nassari, tarehe 2 April baada ya kutangazwa mshindi, aliangalia sehemu ambayo haikumpa ushindi na ukiangalia matokeo kata ya Maroroni ndiko alikopata kura chache sana. Wale watu wanashida sana na kimaendeleo wako nyuma mno na tatizo la karne nyingi ni maji! Alianza uchimbaji wa visima tar 3 maroroni! Why government doesnt do the same???
 
Back
Top Bottom