Jamii Forums Get Together

WE FURAHA YAKO NI KUONA MABINTI TU?
TEAMO ANA NIKOSHA SANA MZEE WA MA INFIDELITY, NTAFURAHI SANA KUMUONA, YEYE PAMOJA NA NGULI.
PIA PAKA JIMMY ANANIKOSHA SANA.:lol:

quote_icon.png
Originally Posted by ELNIN0
Tuje na familia zetu au kivyetu vyetu? nitafurahi sana kukutana na akina FL1, Maria Roza, Zion daugher na wengineo live - i wish..Ha


Chachandu muhimu Mkuu.
 
napendekeza kuwapo na zawadi kwa wachangiaji bora wa Mwaka huu katika kila forum, Invizibo awepo ili awakilishe zawadi zetu kwa wahusika.

Siasa
Hoja Mbalimbali
Mambo ya Wakubwa - Maria Roza
Utani
n.k

Ndo nimempendekeza huyo kwenye hiyo forum - wengine tuwatafute na zawadi ziandaliwe mapema kabla ya siku ya tukio.
 
Invisible mbona hachangii hoja?it sounds great ila sijui itafananaje au tuje na majina yetu original tusijitambulishe jf names maana inaweza kuwa soo.Au mnaona vp hii wadau?Mintakuja kuwacharge kama nikiona upepo mzuri
 
Good idea bujibuji lakini hujasema ni wapi ukumbi pia nafikiri invisible aje na computer tusign in ndio tuingie ukumbini!
 
makatibu wakuu wa vyama vyote vya siasa waalikwe ... pamoja na Dr. Slaa.... Maalim Seif.... Yusuf Makamba.... tusimsahau Dovutwa Yahmi Hugo Chavez awe mgeni Rasmi
 
napendekeza kuwapo na zawadi kwa wachangiaji bora wa Mwaka huu katika kila forum, Invizibo awepo ili awakilishe zawadi zetu kwa wahusika.

Siasa
Hoja Mbalimbali
Mambo ya Wakubwa - Maria Roza
Utani
n.k

Ndo nimempendekeza huyo kwenye hiyo forum - wengine tuwatafute na zawadi ziandaliwe mapema kabla ya siku ya tukio.


Zawadi si tutashea eennhee
 
Naruhusiwa kubeba take-away? maana kwaweza kua na kitimoto huko??? Uuuwi mamsapu siji naye naskia kuna vidume vina uchu na wake za watu!!! mie naogopa, ntamtuma Rostam aje kuniwakilisha, au nimtume Sitta? Chagueni, Maana ntakua pale La-Kairo mida ya saa tano usiku tukipanga list ya wakuu wa mikoa na wilaya.
 
mie nitakuwepo hapo kama ni dar ila hii kutojuana majina ya ukweli then tuonane sura mmmhhhh, labda watu kuonana ila hakuna kuulizana majina ya humu ndio itaweza endeleza utamu wa JAMII FORUMS
 
kuna michango? maana siku hizi kila ukigeuka mchango hahahhahahhahhaha
au ndiyo patakuwa na bakuli hapo
 
Hii kitu imekaa uzuri, ila sasa inakuwaje au invisibo atakuja na komputa, una sign in ndio unaingia, ahaaaaaaaaaaaa
 
Napenda kuwaalika wana Jamii Forums wote kufika kwa ajili ya mishikaki na nyama choma siku ya tarehe 09.12.2010.
Siku hiyo tutaweza kujumuika kama Forum na kufahamiana.
Nawakaribisha sana.

natamani sana hii siku ifike nimpasue mmoja wa MODs kwa uonevu wnaoufanya..nikikosa kabisa ntamrushia kiatu au ntanyanyuka na kutoka nje ya ukumbi maana siku hizi wamekuwa waonevu sana na wanakiherehere kujipendekeza kwa wakubwa flani sijui wameahidiwa nini
 
Mkuu wazo zuri ila naogopa JF itapoteza umaarufu na kuwa kama facebook.
mi usinipe kadi.
 
Jamani wahusika wa hii shughuli mpooooo?
Ili isiwe kienyeji mimi ni mjasiliamali nipeni tenda ya kuorganise hii kitu iwe kitaalam zaidi kwa punguzo kubwa la hadi 60% kwa shughuli ya kuratibu zoezi zima.
Ntaandaa utaratibu fasta mwenyekutaka atatuma kama elf15 kwa mod atakae teuliwa, kisha tutam pm kumpa location na ratiba kamili na namna itakakavyokuwa,
kwakuwa muda umekwisha tutaratibu utumaji pesa kwa m pesa nk, au hata vocha ya hiyo thamani.
Nasubiri kusikia toka kwenu
 
Venue ni ufukweni mwa bahari ya Hindi, pale Ununio Beach.
Baadae kidogo ntawatumia picha ya mandhari ili muweze kupata picha kamili ya eneo lenyewe.
Usalama upo, kwa ajili yenu na mali zenu.


Time gani mkuu ?
 
Napenda kuwaalika wana Jamii Forums wote kufika kwa ajili ya mishikaki na nyama choma siku ya tarehe 09.12.2010.
Siku hiyo tutaweza kujumuika kama Forum na kufahamiana.
Nawakaribisha sana.

mkuu vipi shughuli imechakachuliwa nini? Mbona kimya
 
Back
Top Bottom