Nisaidieni: Naogopwa sana na watu

Lakabu

JF-Expert Member
May 26, 2023
330
767
Habari za Leo wadau wa jamii forums.

Ninashuhudia baadhi ya watu wakiniogopa sana na sijawai kuwasemesha Wala kuwatania. Hali hii inanifanya nikose amani maana wao wanahisi kukosa amani utulivu na mtiririko wa mahali husika.

Mfano leo nimeenda mahali nikakutana na watu wengine lakini akatokea kijana mmoja ananiogopa, muda wote ana wasi wasi Kila anionapo. Mwanzoni nilikuwa nadhani labda ni utoto lakini jinsi muda unavyoenda nashuhudia watu Wengi wanaonigopa.

Hii ni nini? Nisaidieni niondokane na Hali ya kugopwa maana napenda kujumuika na wengine ila inatokea wanaanza kuniogopa TU bila sababu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi hua wananishangaa tu, yaan naeza nikaenda mahali unakutana na watu wanakuangaliaa na kukupa Salam ni ishu, haswa jinsia ke ambao ni age mates .. naeza Kutana nao Kwa mbali maybe walikua wanapiga stori ila the moment tukiwa tunapishana wananyamaza ghafla.. hua sielewi
 
Mimi hua wananishangaa tu, yaan naeza nikaenda mahali unakutana na watu wanakuangaliaa na kukupa Salam ni ishu, haswa jinsia ke ambao ni age mates .. naeza Kutana nao Kwa mbali maybe walikua wanapiga stori ila the moment tukiwa tunapishana wananyamaza ghafla.. hua sielewi
Labda wewe ni handsome
 
Habari za Leo wadau wa jamii forums.

Ninashuhudia baadhi ya watu wakiniogopa sana na sijawai kuwasemesha Wala kuwatania,Hali hii inanifanya nikose amani maana wao...
Nilikua nagombea uongozi mahala Fulani, shemeji yangu akanipa Mafuta ya Simba, eti nikienda kwa kampeni nijipake usoni kidogo tu, nitakua naogopwa kama simba.

akanambia nikichanjia nitatisha zaidi na kuogopwa. Lakini pia mimi sitakua nikiogopa chochote mbele yangu...

Vipi wewe umechanjia nini au kupaka nini usoni au mwilini?
 
Mimi wananiita mkurugenzi,bosi,tajiri..na huwa kama kuna sehemu foleni napishwa nitangulie mimi..nikipanda daladala huwa sichukuliwi nauli..nishatoa mara kadhaa nauli konda akakataa huku akisema acha tu bosi..je mimi nani?
 
Hivyo ndivo Mungu kakuweka kubali hilo kwanza maana ni Edeni yako kama samaki anavotegemea maji, badala ya kupasua kichwa kutafuta usichokua na uwezo nacho boresha asili yako uone itakusaidiaje kufikia mafanikio yako, nakuhakikishia kadri utavojichangamsha kwa watu ndivo utakua kituko zaidi
 
Labda ww ni handsome
Ingekua ivo basi nadhan ingekua rahisi wao kunichangamkia. Yaan hata Salam ndo nisipewe.

Najitahidi sana kwenye mavazi, usafi na muonekano kama Mwanaume, ila ni ngumu sana watu kujimix na mm casually
 
Kama ni mtu ambaye una haiba ya kuwa serious na mkimya kwenye maeneo mengi, watu lazma wawe intimidated na wewe kutokana na ile hali ya kuhisi hauingiliki kirahisi na hivyo kuwajengea hofu..

Halafu kuna wale wenye look za pesa 😁😁, unakuta mtu unavaa official au kizee sana kiasi ukiingia sehemu ya vijana wanaona huendani nao hivyo, hamuwezi kuwa na vitu common vya kuongelea. Yani mtu kukuona tu anaviona vitabu, taarifa za habari, CNN, aljazeera, BBC etc wakati wao wanataka kuongea vitu soft 😁😁
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom