Nahisi siku zangu za kuishi Dunia zinakaribia kuisha, sielewi!

X_INTELLIGENCE

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
9,679
12,249
Mimi ni kijana ambae nina mshukuru sana Mungu tokea nimezaliwa hadi hapa nilipofikia, watu wamenisaidia na bado wana nisaidia.

Kuna Muda huwa nina kufuru au kukana kutkukubaliana na uwepo wa Mungu😭 hii ni kutokana na asilimia kubwa ya matarajio yangu tokea nikiwa mdogo hayakuwahi kutimia.

Maisha yangu yamekuwa ya mitihani sana, kila nilichojaribu kuanzisha hakikuwahi kufika mwisho 😭😭😭 kwakweli nimeishi nikiwa na huzuni na furaha chache, mpaka hapa nilipofikia nina watoto wa 3 ambao ninawapenda mno.

Vipo vitu vichache ambavyo vinanitokea hivi sasa vinapelekea mimi kuhisi pengine siku zangu hapa Duniani zina karibia kuisha.

Hivi karibuni kichwa changu kimekuwa kizito mno kutoa maamuzi na ni kama kichwa kinanielemea, kimekuwa na maumivu fulani mithili ya kichwa kilicho toka kuuma!

Kwa taaluma mimi ni Mwandishi wa Habari ambaye napenda sana kusoma vitabu na asilimia kubwa ya vitu vingi nimejifunza kutokana na kusoma vitabu, lakini hivi karibuni nimepatwa na hali ya kutokuelewa kila ninacho kisoma.

Vitabu vyote ambavyo nilikuwa navipenda nikivisoma nahisi vinanichanganya, hata baadhi ya mada nilizokuwa nazipenda hapa JAMIIFORUMS nazo pia nimekuwa sizielewi.🥲

Nimepatwa na hofu hata nikikaa karibu na watu ninaowapenda sifurahii uwepo wao, nahisi kujitenga tu nikae peke yangu tu muda wote.

miaka ya nyuma nilikuwa na ndoto pengine za kuwa fulani nikawa naziishi ndoto hizo kwa kuzipambania kwa vitendo lakini siku bahatika kuishi maisha ya ndoto zangu.

siku hizi ni kama siioni future yangu kabisa... muda mwingine mpaka najiona kabisa kama napoteza tuu muda 😭😭😭😭

kama ninge kuwa simu hope ingekuwa kwenye flight mode ✈️🤣🤣🤣

Ikitokea hamjaniona hewani mwezi mzima mfululizo mjue siku zangu niliziona kabisa zinahesabika hivyo malaika mtoa roho atakuwa amesha fanya yake.

Sifikirii kabisa kujiua kwa aina yoyote ile japo kwenye maisha yangu udogoni mwanangu nilishawahi mara 2 kujaribu kujiua. 😭

Mara ya kwanza nilijaribu kunywa sumu haikuniua, hapo nilikuwa na miaka 9 au 10, mwaka mmoja baadae nilijaribu kujinyonga bahati mbaya kile kitanzi pia hakikuondoka na maisha yangu.

Hivyo nichukue fursa hii kuwaaga ndugu zangu wana JAMIIFORUMS ambao tumeishi wote humu ndani kama familia. Kuna member humu nimesaidiana nao bila hata kufahamiana nao big up sana.

Kuna wengine tumekuwa ndugu na hata nje ya JAMIIFORUMS tumekuwa tukionana kwakweli sina cha kuwalipa.​
 
Ushauri:

Wahi hospitali haraka una matatizo ya ugonjwa wa akili, dalili za mental disorder ziko nyingi mno, kabla haijawa very serious, wahi sasa hujachelewa, matatizo ya kuugua ubongo na neva za fahamu ni mengi mno, ujue hata ukiwa unaumwa mno magonjwa mengine hujui yana uwezo wa kuharibu ubongo na matatizo ya akili huanza..!! Hata baadhi ya minyoo tu wakiwa wengi mno waenda kula hadi ubongo, mfano minyoo aina ya tegu au bilharzia au kichocho, huathiri kabisa ubongo wakikaa miaka bila kutibiwa na dalili za awali ni kama zako, matatizo ya akili.

Fanya hivyo hospitali zipo, kitengo cha psychiatric, utapata matibabu vema.
 
mimi ni kijana ambae nina mshukuru sana Mungu tokea nimezaliwa hadi hapa nilipo fikia, watu wamenisaidia na bado wana nisaidia.

kuna Muda huwa nina kufuru au kukana kuto kukubaliana na uwepo wa Mungu😭 hii ni kutokana na asilimia kubwa ya matarajio yangu tokea nikiwa mdogo hayakuwahi kutimia.

maisha yangu yamekuwa ya mitihani sana, kila nilicho jaribu kuanzisha hakikuwahi kufika mwisho 😭😭😭 kwakweli nimeishi nikiwa na hudhuni na furaha chache.

mpaka hapa nilipo fikia nina watoto wa 3 ambao nina wapenda mno.

vipo vitu vichache ambavyo vinanitokea hivi sasa vinapelekea mimi kuhisi pengine siku zangu hapa Duniani zina karibia kuisha.

hivi karibuni kichwa changu kimekuwa kizito mno kutoa maamuzi. na ni kama kichwa kina nielemea kimekuwa na maumivu fulani mithili ya kichwa kilicho toka kuuma...!

kwa taaluma mimi ni muandishi wa Habari ambae napenda sana kusoma vitabu. na asilimia kubwa ya vitu vingi nimejifunza kutokana na kusoma vitabu. lakini hivi karibuni nimepatwa na hali ya kuto kuelewa kila ninacho kisoma. vitabu vyote ambavyo nilikuwa navipenda niki visoma nahisi vina nichanganya. hata baadhi ya mada nilizo kuwa nazipenda hapa JAMIIFORUMS nazo pia nimekuwa sizielewi🥲

nimepatwa na hofu hata niki kaa karibu na watu ninao wapenda sifurahii uwepo wao. nahisi kujitenga tu nikae peke yangu tu muda wote.

ikitokea hamjaniona hewani mwezi mzima mfululizo mjue siku zangu niliziona kabisa zina hesabika hivyo malaika mtoa roho atakuwa amesha fanya yake.

sifikilii kabisa kujiua kwa aina yoyote ile japo kwenye maisha yangu udogoni mwanangu nilishawahi mara 2 kujaribu kujiua 😭😭😭

mara ya kwanza nilijaribu kunywa sumu haiku niua... hapo nilikuwa na miaka 9 au 10 mwaka mmoja baadae nilijaribu kujinyonga bahati mbaya kile kitanzi pia hakikuondoka na maisha yangu.

hivyo nichukue fursa hii kuwaaga ndugu zangu wana JAMIIFORUMS ambao tumeishi wote humu ndani kama familia.

kuna member humu nimesaidiana nao bila hata kufahamiana nao big up sana.

kuna wengine tumekuwa ndugu na hata nje ya JAMIIFORUMS tumekuwa tukionana kwakweli sina cha kuwalipa.​
Kama kichwa kimekuwa kizito na hata mambo unayoyasoma siku hizi huyaelewi na Ili hali huumwi wala huna tatizo lolote mwilini ni kwanini umewaza Direct kuwa unakaribia Kufa??

Akili imekuwa nzito kutokana na matatizo ya uchumi na ugumu wa Maisha, tafuta suluhu. Hiyo wala siyo dalili ya kifo
 
Wengi tu tulio na shida ila hatufikii hatua hii. Mtu wa Mungu, elewa unao wategemezi nyuma yako, utawatesa sana. Wewe una stress na hujawa resilient, umekata tamaa na huna solutions kwa changamoto ulizonazo. Be strong, be man enough to look for self courage. Ujue wanaokufa huwa hawarudi, so usitamani kufa as if it is a solution
 
bila shaka una msongo wa mawazo uliokithiri.
solution ni kubadili lifestyle yako tu. utakuwa poa

acha kukaa pekee yako muda mrefu na jichanganye kwenye michezo au kutizama football.
kwenye swala la michezo kwakweli mimi sio mwana michezo... labda jogging ila sina ushabiki kabisa wa mchezo wowote...!

na mimi ni aina ya wale watu ambao usipo nizoea siwezi kukuzoea...! hivyo kujichanganya na watu hii kwangu itakuwa mtihani sana... nita jaribu​
 
Prince Mhando una psychosis.. una mental I'll iliyokomaa hasa tabgu nikufaham.

Ugumu wa maisha utakupoteza kabisa. Kwa kazi zote ulizofanya hujapata ya kukomaa nayo na kumbkumb zangu zinanambia upo unalinda shamba kisarawe la The bump. Je tatizo nn hasa?

Kama uliwahi kufikiria kujiua maana yake unatembea na wazo Hilo.. unahitaji haloperidol amitriptyline na folic acid. Pia therapy mana kwa hali hiyo utaanza kupata maruwe ruwe yani kuongea peke yako tena hivyo na kuokota karatas.

Nina ndugu yangu ana experience kama yako, unahitaji therapy na matibabbya mda mrefu sana kurudi kuwa kawaida. Umeshaianza kupoteza memory na huwezi kuconceteate? Duh
 
Kama kichwa kimekuwa kizito na hata mambo unayoyasoma siku hizi huyaelewi na Ili hali huumwi wala huna tatizo lolote mwilini ni kwanini umewaza Direct kuwa unakaribia Kufa??

Akili imekuwa nzito kutokana na matatizo ya uchumi na ugumu wa Maisha, tafuta suluhu. Hiyo wala siyo dalili ya kifo
kiuchumi siwezi kusema nina tatizo kihivyo kwani nina jishughulisha... japo sina kipato kikubwa cha kumsaidia mwingine ila nina uwezo wa kula milo mitatu...!

kwakweli sielewi kwanini nimewaza hivyo...!​
 
Back
Top Bottom