Inakuwaje sasa: Mwigulu aendelee kuandika Sheria kwa Kiswahili na Ndalichako aendelee kuandika Upya Mtaala wa somo la historia?

Mackanackyyy

JF-Expert Member
Mar 26, 2019
2,338
5,263
Nafikiri Mama Samia anapaswa kuwaondoa hawa kutoka Baraza la Mawaziri na asitishe pia kazi walizoelekezwa na Hayati Magufuli kuzifanya.

Tunafahamu msukumo wa kutaka Sheria ziandikwe Kiswahili ni kwa sababu Lugha ya Kiingereza ilikuwa ni kama Mama Mkwe kwa Magufuli, na hivyo pengine ilikuwa ikimpa stress za kutosha kuelewa Sheria mbalimbali, naye tunafahamu ni mtu aliyetaka kupambana na kila kundi.

Pia tunafahamu alitaka Mtaala wa Somo la Historia uandikwe upya bila kutaja sababu za msingi au kubainisha mapungufu yaliyopo kwenye Mtaala wa sasa; na kimsingi ni mradi usiyo na mantiki yoyote Ile kwa sababu Kuna somo la Civics/Uraia ambalo linafundisha mambo mengi tu.

Kwa hiyo nirudi kwenye swali langu, hawa mabwana waendelee na kazi zao hizo? Mawazo yangu wakome, na wasiwepo pia kwenye Baraza la Mawaziri la Mama Samia, Fyekerea mbari (hiiiiiii).
 
Binafsi nitashangaa sana kama yataendelea kama yalivyoagizwa, hasa hilo la Historia ya Tanzania.

Naelewa vema na kuikubali hoja ya kuwa na sheria zilizotungwa na kuandikwa kwq Kiswahili na kuendesha mfumo wa mahakama zetu na utoaji wa haki kwa kutumia lugha ya Kiswahili.
 
Kimsingi hapo kwenye somo la bistoria hapo, wapotezee tu kutokana na ukweli kwamba mzee alikuwa amepepesa macho! Labda Serikali iongeze tu baadhi ya vipengele kwenye masomo yaliyopo mashuleni/vyuoni!

Ila kuanzisha eti somo la historia kwa kigezo cha uzalendo! Kiukweli hakuna mantiki kabisa.
 
Ha ha ha! Tatizo la kufanya mambo kwa maagizo ya mtu mmoja; kwa interest za single person! Tungekuwa na mifumo imara badala ya personalities yote haya yasingetokea! Sina hakika kama hii "miradi" itaendelea!
 
Ha ha ha! Tatizo la kufanya mambo kwa maagizo ya mtu mmoja; kwa interest za single person! Tungekuwa na mifumo imara badala ya personalities yote haya yasingetokea! Sina hakika kama hii "miradi" itaendelea!

Uko sahihi sana, mkuu! Alama za personality zingekuwa ndogo sana kwa sababu hizo personality zisingepata nafasi ya kuwa juu sana ya mifumo. Hata miradi haipaswi kuwa personal - ni strategic plans za serikali hivo wote watazifuata!!
 
Hilo LA sheria kwa kiswahili na hukumu za mahakama, Lina mantiki bosi, sio watanzania wote wanaelewa lugha ya malkia, hii itaisaidia sana wa Tanzania kuelewa zaidi haki zao, sharia za nchi n.k..japo mwigulu naye ni genge tu anatakiwa nafasi yake awekwe mwingine
 
Mungu akulinde Samia Suluhu Hassan akuongeze imani, busara na maarifa
Mungu ibariki Tanzania
 
Hilo la somo la historia ltaishia hapo wanaelimu wanaelewa vizuri utata wa utekelezaji wake
 
Back
Top Bottom