Matumizi ya Lugha ya Kingereza Kwenye Mtaala Mpya wa ELlimu Tanzania yasipuuzwe

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

MBUNGE DKT. ALFRED KIMEA ASISITIZA MATUMIZI YA LUGHA YA KINGEREZA KWENYE MTAALA WA ELIMU TANZANIA YASIPUUZWE

Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini, Dkt. Alfred Kimea tarehe 16 Mei, 2023 amechangia hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Elimu huku akiainisha matumizi na faida ya lugha ya kingereza Kitaifa na Kimataifa hususani kwenye ajira.

"Naishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya kunyenyua Sekta ya Elimu ya nchi yetu. Mambo mengi yamefanyika katika Jimbo la Korogwe Mjini; Vyoo, Maabara, Mabweni na miundombinu mingi kwenye shule za Msingi na Sekondari" - Mhe. Dkt. Alfred Kimea

"Mama Samia ametujengea Sekondari mpya kabisa kwenye Kata ya Bagamoyo na Sasa Sekondari nyingine inaendelea kujengwa kwenye Kata ya Mtonga kwenye Kijiji cha Msambiazi na mpaka sasa tumeletewa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule mpya ya Msingi. Baada ya Miaka 10 ya uongozi Rais Samia ataacha historia kubwa Tanzania" - Dkt Alfred Kimea

"Natumia fursa hii kuwapongeza viongozi wangu wa Halmashauri ya Korogwe Mji hasa viongozi kwenye Sekta ya Elimu, Afisa Elimu, Walimu na Wadau wengine wa Elimu kwenye Jimbo la Korogwe Mjini. Halmashauri yetu tunaongoza kwa ubora wa Elimu kwenye Mkoa wa Tanga" - Dkt. Alfred Kimea

"Pamoja na shukurani tunajua vitu vingi vimefanywa. Lakini bado tuna upungufu kwenye shule zetu, upungufu wa Madarasa, Vyoo na shule zingine ni chakavu ila naamini ndani ya Miaka ya uongozi wa Rais Samia changamoto hizi zitatatuliwa" - Mhe. Dkt. Alfred Kimea

"Sipingi kwamba lugha ya Kiswahili ni lugha ya Taifa, tunaipenda na tunajivunia lugha hii na kila Mtanzania anatamani lugha hii izungumzwe Afrika Mashariki na hata Duniani, lakini hatupaswi hata kidogo kupuuzia mchango wa lugha ya Kingereza kwenye Dunia na kwenye mchango wa uchumi wetu" - Mhe. Dkt. Alfred Kimea

"Wanasayansi/Watafiti wanasema mtu mwenye uwezo mzuri wa kuandika, kuongea na kuisikia vizuri lugha ya kingereza ana nafasi nzuri ya kuajirika kuliko mtu mwingine yeyote. Tanzania hatutakiwi kupuuzia utafiti huo. Usahili wowote nchini unafanyika kwa kingereza" - Mhe. Dkt. Alfred Kimea

"Ili uajirike kwenye makampuni makubwa kwenye Dunia hii, nenda Goggle, Facebook, Space X na makampuni mengine ni lazima uwe na uwezo mkubwa wa kuongea lugha ya kingereza." - Mhe. Dkt. Alfred Kimea

"Wanafunzi wetu wakimaliza kidato cha sita wana nafasi kubwa ya kwenda kusoma kwenye Vyuo vikubwa kwenye Dunia hii. Kama unataka mtoto kwenda kusoma Vyuo vikubwa Duniani iwe ni Havard, Oxford bila ujuzi mzuri wa kuongea, kuandika na kusikiliza vizuri lugha ya kingereza itakuwa ni historia" - Mhe. Dkt. Alfred Kimea

"Ili mtu aweze kufanya biashara vizuri, biashara ya kimataifa lazima awe na uwezo wa kuongea lugha ya kingereza. Mikataba mingi ya kibiashara imeandikwa na inakuwa Negotiated kwa lugha ya kingereza" - Dkt. Alfred Kimea

"Ili uwe Consultant mzuri kwenye makampuni ya Kitaifa na Kimataifa ni lazima uwe na uwezo wa kuongea lugha ya kingereza. Hizi ni faida kwa mtu binafsi za kujua lugha ya kingereza" - Mhe. Dkt. Alfred Kimea

"Nchi yetu kwenye Ilani ya CCM 2020-2025 tunasema tunataka kuleta ajira Milioni moja. Lugha ya kingereza ni sehemu ya ajira. Watu wetu wakiweza kuongea Kingereza vizuri watapata ajira nje ya nchi na tutapunguza kugombania ajira za ndani ya nchi" - Dkt. Alfred Kimea

"Issue ya Remittance kwa Dispora. Fedha zinazotumwa na Dispora kutoka nje ya nchi kuja Tanzania 🇹🇿 na zinazotoka nje ya nchi kwenda Kenya 🇰🇪. Tanzania kwa mwaka tunapokea Dollar Milioni 500 kulinganisha na Dollar Bilioni 4 kwenye nchi ya Kenya. Hii ni kwa sababu wananchi wa Kenya wanajua lugha ya kingereza hivyo wanaajiriwa kwenye nchi mbalimbali hasa Ulaya na Marekani. Hatutakiwi kupuuzia uwezo wa Kingereza kwenye Taifa hili" - Dkt. Alfred Kimea

"Nchi ya Kenya 🇰🇪 Remittance kutoka kwa Dispora ndiyo inaongoza kwenye fedha za kigeni (Foreign Currencies) kwenye nchi yao. Kama Tanzania 🇹🇿 hatupaswi kupuuzia. Nchi ya Kenya inatukimbiza na Utalii. Watalii wakati mwingine wanapenda kutalii sehemu ambazo hawatasumbuka kuongea lugha ya kingereza" - Dkt. Alfred Kimea

"Utafiti unaonesha kwamba nchi ya India 🇮🇳 sasa hivi inaongoza kwa Foreign Direct Investment kwa sababu wanaIndia wengi wana uwezo wa kuongea lugha ya kingereza. Nenda Kenya, Ghana 🇬🇭 na South Africa huwezi kulinganisha na Tanzania. Wawekezaji wengi wanaenda nchi hizo kwa sababu wana uwezo wa kuongea lugha ya kingereza na wananchi wao wanapata faida" - Dkt. Alfred Kimea

"Asilimia kubwa, Utafiti unasema mtoto antakiwa kufundishwa lugha ya kigeni hasa Kingereza akiwa na Umri kuanzia Miaka sita mpaka miaka kumi, baada ya hapo tunaweza kumfundisha lakini hawezi kuongea vizuri kama Native Speaker kama lugha yake ya kwanza" - Dkt. Alfred Kimea

"Mfumo wetu wa Elimu Tanzania 🇹🇿 ni Mfumo wa kibaguzi sana. Watoto wa kitajiri, watoto wa viongozi na watoto wa wafanyabiashara ndiyo wanapelekwa kwenye shule wanasoma lugha ya kingereza tangu darasa la kwanza. Watoto wa kimasikini, watoto wa wapiga kura wa nchi hii wanapelekwa kwenye zile shule za Kiswahili" Dkt. Alfred Kimea.

WhatsApp Image 2023-05-21 at 14.59.44.jpeg
 
Back
Top Bottom