Kiranja wa jamii
JF-Expert Member
- Jan 2, 2023
- 222
- 529
Ni suala linaloendelea kubishaniwa, kiswahili au Kiingereza kipi kitumike kuhamishia maarifa kwa vijana wa kitanzania (transfer of knowledge).
Huu ubishi kuna wakati mwamba mmoja (Mungu amrehemu) alitaka kuwaonyesha watu kuwa inawezekana kwa vitendo.
Tukubali tukatae, hakuna mkamilifu dunia wala hakuna anayekosea kila kitu. Kinachotugharimu binadamu mabaya yetu yanatabia ya kufunika kila jema tulilofanya! Hili Mwamba geu lilimkosti sana.
Kati ya vitu nilivyokuwa nasubiri kwa hamu ni somo la historia ya Tanzania kufundishwa kwa kiswahili
Nafahamu huenda watunzi wangeweka mbwembwe kibao za kusifia watawala kulingana na aina ya upepo uliokuwepo lakini hilo lingebaki kuwa umaamuma wa watunzi kutozingatia weledi wao.
Hivi somo Kama history kuna haja gani ya kufundishwa kwa lugha ya kigeni? Wanasema kiswahili hakina misamiati ya kutosha, history ina misamiati gani isiyokuwepo kwenye kiswahili?
Somo la civics au General study, linashindikana nini kufundishwa kwa kiswahili? Hali kadhalika kwenye geography?
Ukiangalia haya masomo ndo msingi mkubwa wa kujenga kujitambua tulikotoka na tunakoelekea Jambo ambalo ndio msingi mkubwa wa kujenga uzalendo wa mtu kulipenda taifa lake.
Ukiangalia ufaulu wa somo la historia na civics unazidi kudidimia kila mwaka.
Kama watu hawajui historia yao wataanzia wapi kulipenda na kulipigania Taifa lao?
Ukiangalia mataifa yaliyoendelea Kama china tamthilia na movie zao nyingi zinasimulia historia yao. Hii huwajenga watoto kulipenda na kulipigania Taifa lao. Huku kwetu tumekazana kuwapeleka watoto wetu English medium waweze kusema mummy na dady wanaporudi na tunawasifia kwa kudhani hiyo ndo elimu
Mama Ndalichako atwambie vile vitabu na ule mtaala wa historia ya Tanzania uliotakiwa kuanza kufundishwa siku chache kabla ya kifo cha Magufuri uko wapi!? Tulitakiwa tuanzie hapo masomo mengine yangefuata baadae