Ushauri: Somo la Historia ya Tanzania na Maadili liwekewe sura maalumu kwenye katiba ili kulipa msisitizo wa kisheria

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,590
4,601
Wasalaam,

Taifa likiwa katika mchakato wa kuandaa sera ya mtaala mpya ya Elimu na mtaala huo kupendekeza kuwepo kwa Somo la Historia ya Tanzania na Maadili ni jambo jema kwa kizazi Cha Sasa na kijacho kulilinda Taifa dhidi ya mmomonyoko wa maadili.

Huu ni mtazamo wangu juu ya uwepo wa Somo Hilo jipya. Kwa kuwa somo hilo bila shaka litakuwa ni mwanzo wa kusisitiza maadili ya Mtanzania na bila shaka litajikita zaidi kwenye masuala ya kisheria basi ni vema katika katiba iwe ya Sasa au katiba mpya iwepo sura maalumu ya kukazia na kusisitiza Somo Hilo.

Somo hilo likiandaliwa kulingana na sura hiyo maalumu ya katiba litawaandaa watoto kufahamu uvunjifu wa maadili ni suala la kisheria na kikatiba na wakienda kinyume watakuwa wanavunja katiba na sheria zaidi ya kufundisha tu ili kuwaelimisha.

Pia, ninaamini likiwekewa msisitizo kwenye katiba itakuwa ni nyenzo ya watoto kuwa na hofu zaidi juu ya uvunjifu wa sheria na katiba.

Huu ndio ushauri wangu.
 
Back
Top Bottom