Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,582
- 113,785
Mzee Mwanakijiji, Kwanza hongera kwa ile likizo yako ulipofika 11,000. Hongera tena kwa kuvuka 20,000 na ushehe nikiamini ule muda wa likizo ya pili utakapofika 22,000 unakaribia.Kilichodhihirika ni kuwa kama tunataka kuleta mabadiliko ya kweli, kelele za hapa mtandaoni zinapoteza muda na kwa hakika hazifiki kunakotakiwa. NI kwa sababu hiyo nimeamua kutilia mkazo na nguvu zangu zote kwenye kukiendeleza kijarida cha Cheche ambacho nataka kiwe ni nguvu ya kupambana na ufisadi na hata ikibidi kutoka kila siku bure nitafanya hivyo. Nataka kuhakikisha kuwa mwananchi wa kawaida anapata access ya mawazo na fikra nzito, na hoja zenye nguvu ili ziweze kuteka fikra zake.
Ni kwa sababu hiyo, naamua kuchukua likizo isiyo na muda ya kuachana na JF na kutilia mkazo uwanja mpya wa mapambano ambao ni fikra za wananchi wa kawaida wasio na mtandao. Tumeanza kuwafikia wiki hii iliyopita na tunataka tuwafikie zaidi sasa. Kuendelea kujibishana hapa JF na kulumbana na kubezena na kuwashiwishana ni kupoteza muda kwa sababu naamini hakuna watu ambao wako so informed kuhusu nchi yao kuliko watu wa JF. Nadhani hapa tumebakia kuhubiri kwa wanakwaya wetu na tumeendelea kuimba pambio ndani ya kanisa. Tunachofanya sasa hapa ni kuendelea kufanya maulidi kwenye madrasa! Lazima tutoke humu na kwenda kuwa mwanga na nuru kule nje.
So, I said it, tulifanya makosa tulipomchagua Kikwete na ni wajibu wa kila Mtanzania anayeitakia nchi mema, na ambaye anataka Taifa jipya, la kisasa, la kizalendo na lilo nona kwa mafanikio kuwepo kufanya kila awezalo kuhakikisha kuwa Kikwete na maswahiba wake hawarudi tena Ikulu 2010 na kuvunja huu uigizaji wa uongozi unaofanywa nao. Sidhani kama kuna kitu chochote ambacho Kikwete atakifanya sasa ambacho kitanifanya nimpe nafasi nyingine ya kumuamini.
I'm done with him. Kesho naanza likizo toka JF hadi mtu mwingine atakapofikia post 11,000!!! au unless Kikwete resign!
Hii posti sikubahatika kuiona wakati huo, nilikuwa bado sijajiunga JF. Ila uliiandika ukiwa too emotional, we are facing the reality now nahofia usije ishia kwenye frustrations kwa vile Octoba ndio hiyo!.
Kwa maoni yangu, hili la JK, its a gone case, its too late now for anything else. Hata kama hiyo CCJ ingekuwa na usajili wa kudumu, bado ingekuwa too little too late.
Tatizo ninaloliona ni kuwa hata baada ya kufanya makosa, hatuangalii nyuma kuona tumejikwaa wapi, njia ni ile ile, tutapita tena na 2015 tutajikwa tena pale pale tulipojikwaa mwanzo, tutaanguka, tutainuka na kujifuta mavumbi huku tikilialia na kuendelea kusonga mbele na kusubiri kujikwaa tena 2020!.