Shomari
JF-Expert Member
- Mar 8, 2008
- 1,112
- 241
You need only speak for yourself in this case.
i do not mean to be selfish, but you asked about the reaction of Dk. Slaa and so on...! but what do you have to give by yourself? think !
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
You need only speak for yourself in this case.
i do not mean to be selfish, but you asked about the reaction of Dk. Slaa and so on...! but what do you have to give by yourself? think !
It is possible to start from the bottom to the top.
Nothing. I am only interested in knowing what you mean exactly by
Takbiru Alaah walibalu!
Haya maneno ni Njabu Ngabu ndiye aliyependelea kuyatumia sana kwenye mabandiko yake.
Nothing. I am only interested in knowing what you mean exactly by
hahahahaaaa kuna post zinaniua mbavu.......Nyama hatari hakatizi kwa Nyani Ngabu....Njabu Ngabu ndie huyu huyu Self Scientific aka Nyama Hatari aka Jokofu Kiwete aka VRS aka PuNyapu Ngabu.....Mods mfungieni huyu jamaa kabla hajaharibu humu..........
wewe umeuliza '' kama hakuna aliyeweza kumkamata mkapa, abasi atawezaje kumkamata mh. Kikwete? '' na umeongezea kuhusu Dk. Slaa na kadhalika, je umekwishawauliza watu hao ( Slaa & n.k ) na wakakueleza nini wanachotarajia?
katika watanzania milioni 40 wewe ni miongoni mwao , na ni wajibu wako kutekeleza wajibu. kipi ambacho umekwishaanza ?
.It is possible to start from the bottom to the top
Ewalaah! Swadaktaah! Alhamdulilaah! Takbiru alaah walibaahlu! Ila naona umesahau the constructive part of your criticism. Sasa baada ya kunena maneno mazito yenye jazba kubwa kama hayo; jee una ushauri gani kuhusu pendekezo au mapendekezo ya suluhisho la malalamiko uliyo nayo dhidi ya Kikwete na serikali yake?
Watanzania Wenzangu,
Baada ya Muungwana kumaliza kusoma Bajeti yake,Mzee Mwanakijiji alitoa rai ya kusita kuandika tena hapa JF mpaka hapo mtu mwingine atakapofikisha post 11,000.Ila baadaye Mzee Mwengangu alirudi na kuendelea kuandika sababu ya uchungu aliokuwa nao kwa ajili ya watanzania wote.Nampongeza kwa hilo!
Toka Muungwana amalize Hotuba ile nimekuwa nikipitia kila kipengele cha hotuba ya masaa manee aliyoyasoma Muungwana,wakati huo huo nikilinganisha na hotuba mbali mbali za wizara za serikali.Alichokizungumza kuhsu kilimo,Madini,maji,mazingira na khali ya uchumi wa nchi hakuna tofauti na kile walichozungumza Mawaziri.
Ukiangalia kwa undani zaidi,watu hawkutegemea hotuba ya namna hii,hata mimi mwnaa CCM nilichukizwa nayo,siyo tu kwasababu ya urefu wa hotuba ile bali mambo yaliyozungumziwa mle ndani.mkulu alishindwa kutupa maji ili kupoza kiu tulichonacho.Hii inasikitisha sana na hasa maneno kama haya kuwa yeye ni Tumaini lilolerejea.
Nimefikira sana,inaonesha Mkuu hana uwezo wa kutatua mambo magumu,ameshindwa kutuambia ni lini bei ya mafuta itashuka ili tuweze kuwa kama nchi jirani za kenya na rwanda.AMeshindwa kusemea kusitishwa kununuliwa kwa magari ya kifahari ili khali walimu wakishindwa kulipwa mishahara yao.
Watanzania wenzangu,kipindi flani niliwahi kuhisi na kukubali kiaina kuwa yawezekana Muungwana anadanganywa na wasaidizi wake ila ana dhamira nzuri kwa watanzania ,na hii niliijenga baada ya yeye kuzoea kutuzuga na maneno haya "Tanzania yenye neema inawezekana".Toka Suala la RDC Niliweza kugunduayeye ndiye anatudanganya sisi na wala siyo wasaidizi wake.Mkulu amsehindwa kutupa majibu ya maswali rahisi sana,
1.Je nini kitafuata baada ya mkataba wa DOWANS kuvunjwa?
2.Je baada ya kamati ya madini kuamliza kazi yake,ni lini mikataba hii itafanyiwa kazi na kunufaisha watanzania?
3.Waliohusika na RDC watachukuliwa hatua zipi za kisheria,Hasa Nationa Negotiation team?(Mawazo ya kina Mwakyembe yametupwa??)
Tumekuwa watu wa kuzugwa kwa kutumia kamati ambazo kila siku zinaendelea kutafuna pesa yetu na ripoti hazifanyiwi kazi.Kamati hivi zinatumia pesa nyingi sana na watu huwa wanalipwa kwa siku wastani wa sh. 400,000 hadi 500,000 kwa ajili ya vikao vya kamati huku wakikaa katika hoteli za kifahali maneno ya bagamoyo.Kamati zinafanya kazi ila HATUA hazichukuliwi.Tuliona tume ndogo tu ya miezi mitatu ya kesi ya kina malima na Mengi ilitumia zaidi ya milioni 100.Je kamati za miezi sita hutumia kiasi gani?
Mwaka Jana nilipokuwa Bungeni,niliwahi kumuuliza kiongozi mmoja wa wizara moja ya serikali,Je ni kiasi gani huwa kinatumika kwa jili ya wizara kuja kuwasilisha bajeti.Yaani kuanzia maandalizi hadi sherehe ya mwisho bajeti imepitishwa.Aliniambia ni zaidi ya milion 600.Je kuna wizara ngapi?hizo ni takribani ya bilioni 30 ukijumlisha na posho za wabgune hutumika kwa akili ya kikao kimoja tu cha bajeti.unadhani kiasi gani cha pesa kinapotea?Ndiyo kuna umuhimu,ila kuna haja gani ya kutumia pesa zote hizi..basi tuwe na kikao kimoja cha bajeti kila bada ya miaka 3!
Tumekuwa waoga sana,tumekuwa wavumilivu wajinga tusitaka kuchukua hatua za kufanya,saa ya ukombozi ni sasa na ingekuwa vyema tukaandamana na kumuunga mkono spika ya kuwa wahujumu uchumi hawatakiwi kuonewa Huruma hata kama ni rafiki zake na Mkulu.Tayari Mkulu ameoneshwa kuchukizwa kwake na spika kufanya majumuisho ya hotuba yake kwa muda wa dakika kumi.Wachunguzi wa mabo wanaelezea pia hata kauli ya spika kutoa mwanya kwa wabunge kuijadili hotuba hiyo kumezua mgongano mkubwa katia ya spika na serikali.Serikali inahoji kwanini wabunge WAJADILI mambo yaliyosemwa na Mkuu wa nchi?
Tumeshakata tamaa vya kutosha,na sasa ni wakati wa kuchukua HATUA ili kuikomboa nchi yetu,tutumie sanduku la kura kuweka viongozi makini na walio na uchungu na nchi yetu.Hii changamoto ianzie katika vyama vyetu kwa kuwakata wale wote wasiyo na machungu na nchi yetu na tuwape wale wanaotaka kufanya yale tuyatakayo.Tutoke kuzimu na tuache kuwa mazezeta hata kama wanatuona mandondocha.
Yes I have said,ni bora kuishi bila yeye ,sababu ameshindwa kutupa yale tuyatakayo.chukua HATUA kwa kuanza kujipanga mapeama sasa ili tumpate yule tumtakaye.tutumie njia iliyo sahihi na ambayo ni haki yetu.WE SHOULD STOP TO MONITOR OUR GOVERNEMENT AND START PARTICIPATING IN CHANGING OUR COUNTRY.
Nasita kuandika mpaka pale uchaguzi wa TARIME utakapoaanza,ki -ukweli Jk ameniangusha sana kwa kushindwa kuchukua HATUA kwa watu wa EPA.Nitaendelea kuwa msomaji tu huku nikitafakari 2010.