Elections 2010 I'm done with Kikwete! - Say NO to Second Term!

Kilichodhihirika ni kuwa kama tunataka kuleta mabadiliko ya kweli, kelele za hapa mtandaoni zinapoteza muda na kwa hakika hazifiki kunakotakiwa. NI kwa sababu hiyo nimeamua kutilia mkazo na nguvu zangu zote kwenye kukiendeleza kijarida cha Cheche ambacho nataka kiwe ni nguvu ya kupambana na ufisadi na hata ikibidi kutoka kila siku bure nitafanya hivyo. Nataka kuhakikisha kuwa mwananchi wa kawaida anapata access ya mawazo na fikra nzito, na hoja zenye nguvu ili ziweze kuteka fikra zake.

Ni kwa sababu hiyo, naamua kuchukua likizo isiyo na muda ya kuachana na JF na kutilia mkazo uwanja mpya wa mapambano ambao ni fikra za wananchi wa kawaida wasio na mtandao. Tumeanza kuwafikia wiki hii iliyopita na tunataka tuwafikie zaidi sasa. Kuendelea kujibishana hapa JF na kulumbana na kubezena na kuwashiwishana ni kupoteza muda kwa sababu naamini hakuna watu ambao wako so informed kuhusu nchi yao kuliko watu wa JF. Nadhani hapa tumebakia kuhubiri kwa wanakwaya wetu na tumeendelea kuimba pambio ndani ya kanisa. Tunachofanya sasa hapa ni kuendelea kufanya maulidi kwenye madrasa! Lazima tutoke humu na kwenda kuwa mwanga na nuru kule nje.

So, I said it, tulifanya makosa tulipomchagua Kikwete na ni wajibu wa kila Mtanzania anayeitakia nchi mema, na ambaye anataka Taifa jipya, la kisasa, la kizalendo na lilo nona kwa mafanikio kuwepo kufanya kila awezalo kuhakikisha kuwa Kikwete na maswahiba wake hawarudi tena Ikulu 2010 na kuvunja huu uigizaji wa uongozi unaofanywa nao. Sidhani kama kuna kitu chochote ambacho Kikwete atakifanya sasa ambacho kitanifanya nimpe nafasi nyingine ya kumuamini.

I'm done with him. Kesho naanza likizo toka JF hadi mtu mwingine atakapofikia post 11,000!!! au unless Kikwete resign!
Mzee Mwanakijiji, Kwanza hongera kwa ile likizo yako ulipofika 11,000. Hongera tena kwa kuvuka 20,000 na ushehe nikiamini ule muda wa likizo ya pili utakapofika 22,000 unakaribia.

Hii posti sikubahatika kuiona wakati huo, nilikuwa bado sijajiunga JF. Ila uliiandika ukiwa too emotional, we are facing the reality now nahofia usije ishia kwenye frustrations kwa vile Octoba ndio hiyo!.

Kwa maoni yangu, hili la JK, its a gone case, its too late now for anything else. Hata kama hiyo CCJ ingekuwa na usajili wa kudumu, bado ingekuwa too little too late.

Tatizo ninaloliona ni kuwa hata baada ya kufanya makosa, hatuangalii nyuma kuona tumejikwaa wapi, njia ni ile ile, tutapita tena na 2015 tutajikwa tena pale pale tulipojikwaa mwanzo, tutaanguka, tutainuka na kujifuta mavumbi huku tikilialia na kuendelea kusonga mbele na kusubiri kujikwaa tena 2020!.
 
Si mnajua JK katoka kule walipotoka akina Tagamaio na Dugumba, what do you expect ukute ana damu ya mmoja wao (based na matendo yake).
 
Uwezo wa kufanya quick decisions,that is the key factor. Quick decisions,split-second decisions,also,to make just decisions. You cannot lead a country if it takes you five minutes to decide anything,kwa sababu problems are being created all the time.
 
Politicians are like diapers. They both need changing regularly and for the same reason,so wadau just be cool that is the way system it is,ni bora mfanye ibada labda maisha mazuri mtayakuta mbinguni lakini kwa hapa mtasema mpaka muiote mvi,hata akija nani kutawala nchi hii,hata nyie mnaochamba mkipewa shavu mtakaa kimya yote hayo ni kwa sababu mmetoswa lakini msikate tamaa,keep on going
 
Mzee Mwanakijiji, heshima mbele.

By the way, have we found a viable alternative? or may be we go for the 'VUVUZELAs'
 
Politicians are like diapers. They both need changing regularly and for the same reason,so wadau just be cool that is the way system it is,ni bora mfanye ibada labda maisha mazuri mtayakuta mbinguni lakini kwa hapa mtasema mpaka muiote mvi,hata akija nani kutawala nchi hii,hata nyie mnaochamba mkipewa shavu mtakaa kimya yote hayo ni kwa sababu mmetoswa lakini msikate tamaa,keep on going
Baby2 you are free to attend churches and pray and sing for others who are doing politics for you. But remember mauaji ya Kimbari in Rwanda people run into the church but they were killed behind the kibweta.
 
Sababu ya kuanzisha hoja hii ni baada ya maneno haya ya Kitila Mkumbo:

"Mimi nafikiri akina MKJJ na wenzako ndiyo wenye matatizo kwa kuendelea kuwa na matumaini na huyu ndugu yetu. Sisi wengine ambao hatukuwa na matumaini yeyote na huyu bwana haitupi shida kabisa!"

Kitila, kwa kweli baada ya kusikilia hotuba hii umenifanya niwe upande wako; Kawaida yangu siyo kwenye siasa tu lakini hata katika maisha ya kawaida napenda kuamini kuwa wanadamu ukiwapa nafasi ya kufanya wema watafanya wema; Nimejifunza kumpa mtu nafasi ya kukosea na kujisahihisha. Nimejifunza kutokuwa na hukumu kali sana kwa mwanadamu mwingine.

Lakini katika hilo pia nimejifunza kuwa kuna mipaka isiyovukwa na kuna mambo ambayo mtu hatakiwi kupewa nafasi ya pili. Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikiamini kuwa somehow Kikwete atajikuta anakaa peke yake na kujikuta yuko peke (alone and lonely) na kutambua uzito alionao wa kuliongoza Taifa. Nimekuwa nikitumaini na kuombea kuwa Kikwete atatambua wajibu wake mkubwa na kuamua kufanya kile ambacho viongozi wa kweli hufanya.

Hivyo mara kadhaa (wakati Baraza limevunjika) niliamini kuwa JK atasimama na kuuteka wakati na hivyo kuanza upya; haikutokea hivyo. HIvyo hotuba hii jinsi ilivyopambwa na kutokea kwake wakati na saa kama hii niliamini kuwa labda amejifunza kitu na sasa yuko kweli anataka kufanya kitu; nilikuwa nimekosea.

Kikwete hawezi kuongoza; Kikwete si kiongozi ni mwanasiasa mpiga porojo; Kikwete si kiongozi ambaye Watanzania walitarajia kuwaongoza kutoka kwenye kilindi cha umasikini kuelekea kwenye mafuriko ya mafanikio. Rais Kikwete na niliandika wiki mbili zilizopita ni mtu ambaye amepewa nafasi nyingine kufunga goli ambapo amebakia yeye na golipa na mara zote amekuwa akifika golini anabakia kukaa chini na kusubiri mtu mwingine aje ampasia afunge goli wakati mashabiki wamekaa pembeni wakishangalia na kuombea afunge kwa sababu ni Kapteni wa timu na alinunuliwa kwa bei kubwa.

Unaposhinda uchaguzi kwa zaidi ya asilimia 80 unaweza kabisa kusababisha mabadiliko makubwa ya Kitaifa na kuongoza Taifa. Unapopata support ya watu wa mjini na kijijini, maskini na matajiri unakuwa na mtaji mkubwa wa kisiasa ambapo ni wewe tu unajua ukiuwekeza vizuri utalipa. Lakini kwa kushindwa mikakati, kugwaya, kuogopa kuudhi watu n.k unabakia na mtaji huo ambao pole pole unazidi kumemenyuka.

Kikwete ni kilele cha kukatisha tamaa na mfano dhahiri wa nini kiongozi asiwe. Kikwete anasimama leo hii kama kiongozi ambaye ameshindwa kuongoza na anabakia kuitwa kiongozi. Rais Kikwete amebakia kuwa yule mwenye "simba wa kuchora" ambaye anasimama kuunguruma kwenye picha na watoto wanabakia kucheka.

Leo kwa hakika ilikuwa ni nafasi nzuri kwa Rais Kikwete kuonesha uongozi Tanzania badala ya kupiga zogo. Kama alitaka kuelezea hali ya Muungano wetu na ya Taifa yetu alikuwa na wakati mzuri pale Aprili 26, Mei Mosi, Nane Nane n.k au kila mwanzoni mwa mwaka kama wanavyofanya Wamarekani. Lakini hili la kuiweka roho juu nchi na kwenda na magwaride na uongozi mzima wa serikali kwenye hotuba maalumu ya Rais Bungeni ni kuchezea hisia za wananchi. Ni kutuzuga kulikotukuka ambako kwa hakika kunamfanya astahili kupewa nishani iya Uzugaji uliotukuka daraja la kwanza na la pili!

Rais anapoenda kuzungumza Bungeni iwe kwa kweli jambo muhimu, zito, na ambalo kwa hakika linastahili mahali kama hapo. Kusimamisha shughuli za Bunge ili uje upigiwe makofi na saluti wakati mijadala muhimu ya Taifa inaendelea ni kuwapotezea muda wananchi na wabunge. Hotuba yake jinsi alivyoitoa ingeweza kutolewa na Makamu wa Rais, au Waziri Mkuu au hata Salva Rweyemamu! Haikuwa hotuba inayoendana na Urais kwani kwenye suala muhimu la Muungano alitakiwa kutoa msimamo badala ya "kuwaomba" viongozi wenzake.

Kilichodhihirika ni kuwa kama tunataka kuleta mabadiliko ya kweli, kelele za hapa mtandaoni zinapoteza muda na kwa hakika hazifiki kunakotakiwa. NI kwa sababu hiyo nimeamua kutilia mkazo na nguvu zangu zote kwenye kukiendeleza kijarida cha Cheche ambacho nataka kiwe ni nguvu ya kupambana na ufisadi na hata ikibidi kutoka kila siku bure nitafanya hivyo. Nataka kuhakikisha kuwa mwananchi wa kawaida anapata access ya mawazo na fikra nzito, na hoja zenye nguvu ili ziweze kuteka fikra zake.

Ni kwa sababu hiyo, naamua kuchukua likizo isiyo na muda ya kuachana na JF na kutilia mkazo uwanja mpya wa mapambano ambao ni fikra za wananchi wa kawaida wasio na mtandao. Tumeanza kuwafikia wiki hii iliyopita na tunataka tuwafikie zaidi sasa. Kuendelea kujibishana hapa JF na kulumbana na kubezena na kuwashiwishana ni kupoteza muda kwa sababu naamini hakuna watu ambao wako so informed kuhusu nchi yao kuliko watu wa JF. Nadhani hapa tumebakia kuhubiri kwa wanakwaya wetu na tumeendelea kuimba pambio ndani ya kanisa. Tunachofanya sasa hapa ni kuendelea kufanya maulidi kwenye madrasa! Lazima tutoke humu na kwenda kuwa mwanga na nuru kule nje.

So, I said it, tulifanya makosa tulipomchagua Kikwete na ni wajibu wa kila Mtanzania anayeitakia nchi mema, na ambaye anataka Taifa jipya, la kisasa, la kizalendo na lilo nona kwa mafanikio kuwepo kufanya kila awezalo kuhakikisha kuwa Kikwete na maswahiba wake hawarudi tena Ikulu 2010 na kuvunja huu uigizaji wa uongozi unaofanywa nao. Sidhani kama kuna kitu chochote ambacho Kikwete atakifanya sasa ambacho kitanifanya nimpe nafasi nyingine ya kumuamini.

I'm done with him. Kesho naanza likizo toka JF hadi mtu mwingine atakapofikia post 11,000!!! au unless Kikwete resign!

Hongera mkuu MMkjj,

tatizo lilopo hapa hakuna mbadala wake,pia wamekamata na kulifuta somo la nani anafaa kuwa kiongozi/mtawala wetu badala yake wamekuja na somo la chgua chama hata kama limesimamishwa shetwani! na hasa hili somo limefaulu sana miongoni mwetu na sasa huko uendako kijijini maana hakuna somo walijualo zaidi ya hili.
Hivyo kabla ya kuwaelimisha juu ya ufisadi naomba anza kwa elimu hii ya kuliondoa somo hili"CHAGUA CHAMA" waelewe chama hakitendi wala kuleta maendeleo kwa wananchi bali mtu aliyepewa dhamana ya kuongoza ndiye mwenye kutakiwa awajibike kwao.

All the best mkuu!!
 
Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania ya mwaka 2000 kifungu cha 40.2, kinasema
Hakuna mtu atakayechaguliwa zaidi ya mara mbili kushika kiti cha Rais.
lakini hakitoi masharti kuwa ni lazima iwe mihula inayofutana, la.

NI kutokana na hili, leo nimeamua nimrudi swahiba wangu Rais wa Jamhuri ya Muungano Mheshimiwa Jakaya Kikwete maarufu kama Muungwana, MSanii, Chekacheka, Vasco Da Gama, Mkwere, Mbayuwayu, Kibuge, Mwanasesere na yule ambaye Disemba 22 ya mwaka 2005, niliandika makala ya Utopia https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/60282-utopia-hercules-marx-robin-hood-and-abramoff.html na kisha ile kubwa kuliko zote ya S C R E W Muungwana https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/2204-on-muungwana-disappointing.html niliyoiandika Machi 10 2007. Kisha ikafuatia ile niipendayo sana ya Thank God for Giving Us Kikwete https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/12532-thanks-god-for-giving-us-kikwete.html niliyoichapa April 24 2008.​

Pamoja ni hizo thread 3, kuna nyingi sana nimeandika kuhusu Kikwete na natambua kwa mujibu wa katiba ya Tanzania ya mwka 2000 kifungu cha 37.1 kinachosema​
Mbali na kuzingatia masharti yali yomo katika Katiba hii, na sheria za Jamhuri ya Muungano katika utendaji wa kazi na shughuli zake, Rais atakuwa huru na hatalazimika kufuata ushauri atakaopewa na mtu yeyote, isipokuwa tu pale anapotakiwa na Katiba hii au na sheria nyingine yoyote kufanya jambo lolote
ushauri wangu, uchambuzi wangu na matusi na hata kumfanyia maskhara, hawajibiki kusikiliza ninachosemana anaweza kukipuuzia maana si kwa mujibu wa Katiba na Sheria.
Ama kwa mtaji huo huo, si ushauri na lawama za Mchungaji pekee, bali ni za kila mtu, Mzee Mwanakijiji, Dr. Slaa, Lipumba hata Mzee Mwinyi, Kikwete ana hiari ya kutusikiliza au kutokutusikiliza. Aidha hata ushauri kutoka kwa watendaji wa Serikali na washauri wake, kama si sheria na kwa mujibu wa katiba, Kikwete hana ulazima wa kusikiliza na kutimiza ushauri anaombiwa na kuaswa.

Kwa mtaji wa kinga hii, ndio maana nakuja na hoja mpya, tena baada ya yeye Kikwete kuamua kugombea tena na nasema wazi, ningekuwa mimi Kikwete, nisingeligombea Urais kwa uchaguzi huu wa mwaka 2010, ningejichukulia muda wangu nikaka pembei nifurahie mafao na marupurupu ya Urais nikijipanga upya.

Sina maan aya kusema kuwa Kikwete ni mtu bora au kafanya kazi bora na anastahili Urais mara ya pili, la hasha! Bali ni jitihada zangu za kumshawishi asikie ushauri na maoni ya watu ili aweze kuwa kiongozi bora na kuheshimika.

Leo hii kama Kikwete angejionda kugombea urais kwa sababu yeyote ile anayotaka, angeheshimika sana na tena kuogopeka hata kama ukweli ni kuwa angekuwa anaficha udhaifu na kuikimbia aibu ya utendaji mbaya wa Serikali yake na maamuzi yake yasiyoeleweka na yasiyo na manufaa kwa Taifa.

Sababu ya kumrudi aleo Kikweta siku anayoanza rasmi kufanya kampeni yake ni kuonyesha wazi kuwa ni wapi ule ushindi wake wa mwaka 2005 wa Tsunami haukuwa na manufaa yeyote kwa Mtanzania na haukuleta tija au ufanisi kama alivyodai kwenye kile kiitikio chake cha Ari, Kasi na Nguvu Mpya.

Kuna Mmarekani mmoja anaitwa James Carville, ambaye alikuwa meneja wa kampeni za uchaguzi kwa Bill Clinton alipokuwa akigombea Urais mwaka 1992 na alitoa kauli moja ninayoipenda na ndiyo ilitumika kwa kampeni ya Clinton an akamshinda Rais aliyekuwa madarakani Geroge Bush wa kwanza. Kauli mbiu aliyoileta James Carville kwenye ule uchaguzi ilikuwa ni hii "its the economy stupid" It's the economy, stupid - Wikipedia, the free encyclopedia

Hi kauli mbiu, ndio nitaitumia leo hii kueleza na kufafanua kuwa kwa nini Kikwete ilimpasa asigombee tena na akae kando mwaka huu.

Katika mahubiri ya" Ari, Kasi na Nguvu Mpya" Kikwete aliwatamanisha Watanzani kuwa katika utawala wake, wataina nuru ya maendeleo na kuwa maisha bora kwa kila Mtanzania yatafanikiwa.

Mimi ni mpenda takwimu, uchumi na hisabati bandia, si mtaalamu bali ni mbwabwajaji ninayependa kusoma magazeti, hotuba vitabu na utundu wa kupekenyua vitu na kuvichambua na kuvijengea maana.

Ukisomayale ya Utopia na S Cre w Muungwana, utabaini wazi kuwa nilitoa ushuhuda wa kiuchungaji kuwa Kikwete hawezi kuliongoza Taifa na kutufikisha katika mafanikio. Mbaa i lile la Utopia nililolito asiku moja baada ya yeye kuapishwa.

Alipoigia madarakani, hazina ya Serikali na deni la Taifa halikuwa hatika hali mbaya ambayo leo hii pamoja na kujigamba kuwa kajenga shule za kata kila kona, kajenga Chuo Kikuu Dodoma na ahadi nyingi, leo hi hali ya Mtanzania kimaisha na mapato na deni la Taifa vinaendeleakuwa vibaya na vinatishia usalama na uhai wa Taifa letu.

Je Kikwete alitufaa kuwa Rais wetu mwaka 2005, jibu ni rahisi sana, hapana kwa kuwa Kikweta si Rais wa kutufaa Tanzania ya leo ambayo inabidi tupige hatua marudufu kujijenga kiuchumi ili tujitegemee na kuondokana na Ujinga, Maradhi na Umasikini.

Labda kwa mtindo wake wa uongozi, labda Kikwete angefikirika kuwa labda anafaa miaka 500 kutoka leo hii ikiwa Tanzania ingekuwa na mfumo wa uchumi na kiutendaji ulio na ufanisi kama wa Marekani, China, Japan, India, Brazil, Ujerumani na hata sayari ya Zebaki.

Tanzania baada ya Mkapa ilitakiwa kupata Micro manager President na si Macro manager the delegator, the unethical, the inneficient, the unmotivated, lazy, laid back President who can not follow up or demand accountability (mnisamehe kwa kuongea Kimombo).

Katika miaka mitano ya Kikwete, ameshindwa kusukuma gurudumu la maendeleo la Taifa kwa manufaa ya Taifa na Watanzania wote. Kasukuma kwa juhudi gurudumu la maendeleo la Wawekezaji wa nje wanaotunyonya hazina yetu na mbaya zaidi kasukuma kwa bidii gurudumu la maendeleo ya wahujumu wa ndani mafsidai na wahujumu wa nje kwa kushindwa kuwa Rais mwenye kufanya maamuzi magumu na kwa manufaa ya Watanzania.

Alipokuja, alianzakutumbua zile ziada ya Hazina kwa kuunda Serikali kubwa mno, akidanganya Watanzania kuwa anataka kila kabila, dini na jinsia ipate wawakilishi, huku ukweli alikuwa analipa fadhila za wale waliokuwa kwenye mtandao wa kumfanya awe Rais.

Katika kulipa fadhila hizi, udhalimu wake wa kuchekea kila mtu na kujifanya mtu wa watu ukaanza tangu Januari ya mwaka 2006, kwa kutokea mpasuko na mgawanyiko katika Serikali yake na kugombea madaraka kwa makundi mawili huku kila kundi likifanya jitihada kuhujumu lingine na kuvuna kwa bidii hazina za Taifa kwa kutumia madaraka na dhamana ya kuongoza.

Alichofanya Kikwete kama Rais au Mwenyekiti wa CCM ni kukaa kando akitafuta uluhisho la win win situation kwa kila kundi na akiyachekea makundi yote bila kusimika mguu wake chini na kufuta mvurugano huo au kukosekana kwa udailifu na umakini kutoka Chama na Serikali yake.

Hivyo hapo tunagundua kuwa pamoja na kuwa anadai yeye ni mchumi, lakini ni mfujaji mkubwa na madai kuwa alitumia miaka 10 kujifunza Urais na ukiongezea ile mingine tangu akiwa Katibu wa Chama Singida, bado hakuwa amejifunza kitu chochote cha kuwa iongozi mahiri bali ni kiongozi ambaye amedhihirisha kuwa ni mwepesi wa kukwepa kazi, ajukumu na lawama na kuachia wengine wabebe huo mzigo.

Je tutaendeleaji kumuamini yeye kuwa atakuwa Jemedari mwenye busara na ukomavu wa kufanya maamuzi yenye kuleta maana na msingi tukiwa vitani? Kama yeye ni kama Kunguru mwoga, kazi kuficha ubawa, iweje leo kwa akili zetu timamu tumpe Urais kwa miaka mingine mitano?

Wala sitapoteza muda kuongelea Ufisadi zaid ya kusema kwa Watanzaiakuwa kumchagua Kikwete, ni kukiri wazi kuwa mmeridhika na maisha ya shida, ya umasikini yaliyojaa maradhi, ujinga ufukara na mmeridhika na mfumo wa kifisadi ambao unawahujumu kila siku nanyi mwabakia kusema liwalo liwe, n imapenzi ya Mungu!

Nitarudi kwenye Uchumi. Takwimu za mwezi uliopita za Benki Kuu, zinaonyesha deni la Taifa likiongezeka marudufu huku uwezo wetu wa kulilipa ukipungua kwa kazi ya hali ya juu, mapato yetu yakiendelea kupungua na matumizi yetu yasiyo ya kimaendeleo yakiongezeka kwa ari, kasi na nguvu mpya na za ajabu na hakuna anayeliona hili kama ndilo tatizo kuu la Tanzania kushindwa kupiga hatua mbele za kimaendeleo kiuchumi.

Katika miaka yake minne ya Kwanza, Rais Kikwete alitumia muda huo kutalii kuiona dunia na kuiza Tanzania kwa wawekezaji. Katika kipindi hicho, kwa maoni yangu ametumia si chini ya dola za kImarekani Milioni 50, kuzunguka dunia kutafuta wawekezaji, huku akisahau kuwa alipaswa kuanza kazi kule vijijini ambako alikuja na kuzunguka nchi nzima akiahidi maisha bora kwa kila Mtanzania.

Inafahamika kuwa Kilimo ndio uti wa mgongo wa Taifa na wakulima na waishio vijijini ni takriban asilimia 75 ya Watanzania na karibia asilimia 85 ya hawa waishio vijijini kama wakulima, wavuvi ,wahunzi, wafuaji na kazi nyingine za mashambani, wanaishi maisha duni kwa kipato cha cha sikukuwa chini ya Dola moja ya kimarekani na ni hawa ambao hufanya na kuishi maisha ya kujikimu, huku wakiwa hawana huduma bora za afya, elimu, miundombinu, maji na hata uwezo wa kuuza mazao na wanachozalsha.

Ni karibu na katikati ya mwaka 2009, ndipo Kikwete akazinduka na kuanza kutembelea nchi yake kila kona akidai Kilimo Kwanza na kuwakimbilia tena Wawekezaji wa nje waje kuwekeza kwenye sekta ya kilimo kwa ahadi zile zile za wachimba madini za kuruhusiwa kuvuna wanachokitaka kwa malipu finyu kwa kipato cha Taifa.

Ni Kikwete huyu huyu alilyeingia madarakani na kusema angerekebisha mfumo wa mapato utokanao na sektta ya madini lakin baada ya miaka miwili ya kamati na kutafakari, kaongeza kipato kwa asilimia moja tu, huku nchi zingine maato yao ni mpaka asilimia 40 kwa kila udongo au kimiminika kinachichimbwa.

Bajeti yake imeendelea kuwa ni tegemezi kwa wafadhili na kwa vituko, mwaka huu 2010 baada ya kukosa msaada kutoka wka Wafadhili, Serikali yake imekwenda kwa Mabenki binfasi na kukopa dola Milioni 250 kukidhi mapungufu ya Bajeti, lakini hapo hapo, tunanunua magari mapya na samani mpya kwa kila Mbunge na Waziri!

Kikwete anaahidi vitu vingi sana, na kajenga shule nyingi sana lakini thamani ya ahadi au alichokifanyia kazi, hakionekani si leo tuu hata huko mbeleni haiwezekani kuonekana labda katika miaka 100 baada ya deni la Taifa kulipwa.

Kiuwajibikaji na kuwajibisha watu na watendaji, huko alikaa likizo. Kikwete katika miaka yake mitano, ametuachia taswira ya Rais ambaye hakuwepo nchini mwake wala kujua linaloendela nchini mwake. Ni sawa na Baba au Mama asiyejua knachoendela nyumbani kwake na wala hana nia ya kujua kinachoendelea.

Amefanya maamuzi na teuzi ambzao hazikuwa na tija, kaliingiza Taifa hasara kutokana na maamuzi mabaya ambayo badaa ya kukiri kufanya makosa, aliyasukumiza kwa wengine na kujiosha mikono.

Kaonyesha udhifu wa hali ya juu kushughulikia suala la Uhujumu, Rushwa na Madawa ya kulevya. Kawakumbatia watendaji wambao kwa makusudi au kwa kiburi wamelitia Taifa hasara kubwa kutokana na uzembe wa kikazi na tamaa binafsi.

Maisha ya Mtanzania iwe ni mjini au vijijini ni ya kubahatsha kwa sehemu kubwa. Dar Es Salaam maish ani mdongamano kila siku, bei za chakula zinaongezeka, gharama za umeme zinaongezeka maradufu, magonjwa yanaongezeka, mafisadi wanaendelea kutamba na kuendeleza mikakati ya kuhujumu na zaidi yeye mwenywe kwa mdomo wake alikiri kuwa asilimia kubwa ya Bajeti ya Serikali yake hupotea kwa rushwa na hakuna udhibiti wa kutosha.

Ninachojiuliza ni hili, zile mbwembwe za kudai yeye na Serikali yake ni ya kwanza kutoa taarifa hadharani za mdhibiti mkuu wa mahesabu zilikuwa za manufaa gani ikiwa mapendekezo ya mdhibiti mkuu hayajafanyiwa kazi na kila mwaka tunaona kuongezeka kwa kuvunjwa kwa kanuni za kibajeti na mahesabu?

Je tutasema tuna kiongozi hodari, shupavu, mkakamavu na mchapa kazi? au tunafurahia kuwa na kiongozi goigoi, zezeta, zuzu, zobwe, zembe, bangaizaji na mwoga?

Alichokifany acha maana sana na hiki sitasita kumsifia ni kutupa uhuru wa kutoa maoni na kubwabwaja, iwe ni ukanjanja au la, lakini tumeweza kujifunza mengi na kujifahamu kama Taifa kwa kuwepo kwa "uhuru" huu bandia usio na mafanikio kwa yeye kuwa msikivu na kujituma, maan akifungu cha 37.1 kina mlinda!

Kama mimi ningekuwa mgombea urais wa chama chochote dhidi ya Kikwete, ningewauliza Watanzania swali kuu moja "je wanaridhika na maisha yao, mfumo wa kiuchumi, utendaji wa Serikali na hatima ya Taifa lao?

Kama wakinijibu, ndio, nitawaambia waendelee na maisha yao ya kufurahia dhuluma, dhiki, ufisadi na umasikini kwa kumchagua Kikwete na kukipa CCM dhamana ya kuongoza Taifa kwa kuwachagua wabunge wa CCM.

Kama wakijibu hapana, ndipo ningewaambia kwa nini basi wanaendelea kuikumbatia CCM?

Lakini lengo langu si kuanza kampeni bali ni kuhalalisha kwa ni ni Kikwete alipaswa kutogombea mwaka huu.

Ni aibu kubwa kwa mtu yeyote makini kudhani kuwa miaka mitani ya kwanza ya Kikwete ilikuwa ya manufaa kwa Taifa na Watanzania. Ni aibu kubwa kwa Kikwete mwenyewe kudhani kuwa amefanya kazi nzuri sana na anastahili apewe miaka ya nyongeza papo hapo baada ya kutumia miaka mitatu kujifunza kazi, kitu ambacho alipokuwa anagombea mwaka 2005, aliliambia Taifa kuwa ametumia miaka 10 kujifunza kazi an alikuwa tayari.

Kama anekuwa msikivu wa ushauri, ningeandika hili mapema sana, tena mwanzo ni mwa mwaka kwa kumtaka asigombee mwaka huu, achukue likizo, akae chini atafakari na kufanya tathmini ya kweli, kama nafsi yake ina dhamira ya kweli na ajiulize ni kitu gani cha msingi na manufaa alikifanya katika miaka mitano yake aliyokuwa Rais.

Kama leo umasikini unaongezeka, hujuma na ufisadi unaongeeka, deni la Taifa linaongezeka, matumizi yasiyo ya msingi au kimaendeleo yanaongezeka, ukosefu wa tija, ufanisi, uwajibikaji, nidhamu ya kazi na kuheshimu dhamana kunaongezeka, ujinga na maradi yanaongezeka, tabu, shida, karaha, kutokuaminiana kunaongezeka, iweje leo akimbilie kusema nipeni miaka mingine mitano, tena kwa kiburi cha kuwaambia wengine sihitaji kura zenu?

Wala suala la Muafaka sitaki kilitaja maana kalifanya bila busara sasa linamlipukia kwa Zanzibar kudai Utaifa wao.

Narudia tenza ningekuwa mimi Kikwete, ningempisha mtu mwingine ndani ya CCM agombee, nigeachia Upinzani ushike hatamu, nirudi kwenye maabara kujifunza makosa ya miaka mitano ya kwanza na kisha nitakapokuwa tayari na nimejizatiti na kuamini kuwa sasa nakwenda litumikia Taifa kwa dhati na nitaketa mabadiliko, ndipo ningetumia nafasi yangu kikatiba kugombea kwa mara ya pili hapo mwaka 2030!
 
Naona umesikia kilio changu lakini mbona hujagonga sana nyundo kama kule?
Umeng'ata na kupuliza
 
Rev naona hali si nzuri. Fimbo ya mbali haiui nyoka.

Besides, huwezi andika haya wakati jamaa kesharudisha form na kampeni kaanza. Wakati muafaka ilikuwa kabla hata hajachukua form ya kuomba wanaCCm wamchague agombee urais kwa tiketi ya chama chao. Lau kama u Shibuda.
 
Ama,

Tangu mwaka jana, CCM walishaamua kuwa mgombea wao ni Kikwete. Wakaanza kauli za ajabu ajabu na kutishana ndani ya chama chao. Wakatokea watu wakidai hakuna mwingine ila Kikwete pekee, kwa nini tupoteze muda nao ilhali kam awalikwenda Butiama kushughulikia Ufisadi na Muafaka walitoka kapa na kutokujali kilio cha Watanzania? Je umeelewa maana ya mimi kunukuu katiba na kuoanisha na uongozi wa Kikwete?

Je hukusoma siku zote nikisema hafai hafai tangu siku kaapishwa? Je CCM walikuwa wapi wasisikilize hilo na kuamua kumchagua mwingine?

Fidel,

Sipulizii kitu, nang'ata tena sihitaji kumtukana kama nilivyomtukana kwenye S C R ew Muungwana, hapa ni suala la can he do the job or not na ni suala la sasa kuwasukumizia wale waliofurahia sura yake na kumpa ushindi wa Tsunami. I hope people will read and understand this plea!
 
You have miscalculated, hata kama unang'ata.

You should have bitten earlier babaa. Huna tofauti na Chadema kwenye miscalculation.

Lete nyimbo nyingine kuhusu Kikwete, hii no please.
 
... ningekuwa mimi Kikwete ... nirudi kwenye maabara kujifunza makosa ya miaka mitano ya kwanza na kisha nitakapokuwa tayari
unaandika kitabu kizima kudadavua na kuanika uozo wa kiongozi halafu unasema aende arudi tena, hakuna wengine mpaka yeye aliyeharibu arudi? Unajuaje kama sio uwezo wake asili unaishia hapo?

Wananchi Afrika wamezoea machifu na wafalme, watu wabovu bado watapendwa waongoze milele
 
You have miscalculated, hata kama unang'ata.

You should have bitten earlier babaa. Huna tofauti na Chadema kwenye miscalculation.

Lete nyimbo nyingine kuhusu Kikwete, hii no please.

You are the one who is miscalculating, living in utopian dreams that are so deceptive to read signs of times. I have already bitten Kikwete, check out Richmond, Meremeta and EPA if you are a fan of kukoromea Ufisadi or go to other issues such as energy, minerals, budget and such it you are thoughtful on economy and maisha bora.

Check out my profile and go through threads and come back again with your miscalculation tone.
 
unaandika kitabu kizima kudadavua na kuanika uozo wa kiongozi halafu unasema aende arudi tena, hakuna wengine mpaka yeye aliyeharibu arudi? Unajuaje kama sio uwezo wake asili unaishia hapo?

Wananchi Afrika wamezoea machifu na wafalme, watu wabovu bado watapendwa waongoze milele

Have you ever read literature or Kiswahili wanaita fasihi?
 
Katika miaka mitano ya Kikwete, ameshindwa kusukuma gurudumu la maendeleo la Taifa kwa manufaa ya Taifa na Watanzania wote. Kasukuma kwa juhudi gurudumu la maendeleo la Wawekezaji wa nje wanaotunyonya hazina yetu na mbaya zaidi kasukuma kwa bidii gurudumu la maendeleo ya wahujumu wa ndani mafsidai na wahujumu wa nje kwa kushindwa kuwa Rais mwenye kufanya maamuzi magumu na kwa manufaa ya Watanzania.

Haswa!! Swala la wawekezaji kutoka nje badala ya Taifa kusimamia na kutekeleza uwekezaji wa ndani kwa ndani limefanyika shaghalabaghala na kuliacha Taifa likiwa limeingia kwenye mamikataba yenye kulaani vizazi vya leo na vijavyo.
 
Have you ever read literature
fiction literature, you had to. The Anthills of Savannah, Dunia Mti Mkavu, Song Of Lawino, Ngoswe: Penzi Kitovu cha Uzembe, The River Between, Hawala ya Fedha, No Longer At Ease, Adili Na Nduguze, Weep Not Child, Kuli, The Arrow of God, Shida, Petals of Blood, and what not

in fiction literature they may say you can lambaste a failing president then suggest he come back
 
Since you are such a laureate, then you can figure between the lines what am stating and to whom I am directing the message.
 
You are the one who is miscalculating, living in utopian dreams that are so deceptive to read signs of times. I have already bitten Kikwete, check out Richmond, Meremeta and EPA if you are a fan of kukoromea Ufisadi or go to other issues such as energy, minerals, budget and such it you are thoughtful on economy and maisha bora.

Check out my profile and go through threads and come back again with your miscalculation tone.

I am checking you today as you mimic your environment. You keep on murmuring of events but you fail to substantiate your opinions and suggesting the way forward and how to go about it.

Your call for Kikwetes term off at this point and time is a defect, period
 
Back
Top Bottom