Elections 2010 I'm done with Kikwete! - Say NO to Second Term!

Huyu ni Gembe yule yule au aliacha laptop yake huku email yake ikiwa wazi so mtu akatuma hii post???????kama ni wewe Gembe original ushajua mwenyekiti wako wa Taifa ni msanii,unafikiria nini 2010?nami sasa naanza kukubaliana na ule msemo wa Nyani Ngabu

Mr kiroboto, huu ndio ukomavu humu JF, wote tunapaswa kuwa kama Gembe. Kwa kweli si lazima mtu awe anajadili kuelekea upande ule ule siku zote. Hongera sana Gembe, na wengine waige
 
Tuna kila sababu za kutomchagua tena Rais Kikwete (Ashauriwe pia a withdraw nia yake).
Nakaribisha michango...
 
Mkuu, mbona hii post inaelea hewani?? Kila mtu ana sababu yake ya kumchagua au kutokumchagua Kikwete. Wewe kila sababu yako unayoisema ni ipi? Weka mlolongo wa sababu zako unazozisema za kwanini tusimchague halafu na sisi tutakuja na za kwetu za ama kwanini tumchague au kwanini tusimchague.
 
Mkuu, mbona hii post inaelea hewani?? Kila mtu ana sababu yake ya kumchagua au kutokumchagua Kikwete. Wewe kila sababu yako unayoisema ni ipi? Weka mlolongo wa sababu zako unazozisema za kwanini tusimchague halafu na sisi tutakuja na za kwetu za ama kwanini tumchague au kwanini tusimchague.
(1) Hawezi kuwawajibisha alio waweka madarakani-->Sophia Simba amewataka wanawake wanachama wa CCM kuwanyima unyumba waume zao. ambao si wana CCM..JK yuko quite kabisa katika hili.
 
Sawa, lakini nchi haiwezi baki bila raisi. Inategemea atagombea na nani, maana bado sijaona mgombea mwingine mwenye maana...
 
Tuna kila sababu za kutomchagua tena Rais Kikwete (Ashauriwe pia a withdraw nia yake).
Nakaribisha michango...
hii post yako ni ki-mini skirt; haijitoshelezi

kwa mwendo huu hatufiki mbali
 
mkubwa hapo umekurupuka na hii post. sawa wengi hatujaridhishwa na uongozi wa miaka mitano ya kikwete lakini tumchague nani sasa? lipumba? OVER MY DEAD BODY! NO. vyama vingine vya siasa havitaki kutuwekea watu wa maana wenye akili zao (nadhani hawana) sasa wapiga kura wafanyaje? wabaki bila rais?
 
Jamani na nyie ma great thinker mbona mie nimemwelewa anamaanisha nini..
1. Hana confidence katika kufanya maamuzi
2. Ni msemaji na si mtekelezaji
3. Anawakumbatia mafisadi
4.Hawezi kuwajibisha wenye makosa
Nk.Nk.
 
Kwa watu wenye akili kumukichwa wanajua hili

""Am done with Muungwana,It is better we go on without a person like him..I second"

Sio Vibaya tukajikumusha ya nyuma ambayo yanaonekana sasa
 
Wakati tunapiga porojo huku tusimsahau MUNGU pia wadau atusaidie kwa tunayotaka kufanya msilalame tu kwa nguvu zenu
 
Mzee M.M.Mwanakijiji

Kijalida cha Cheche kilipotelea wapi???

Kilikuwa ni mhimu sana kwa sababu kuna watu wengi sana wanatakiwa kupata hoja zinazojadiliwa hapa kwenye mtandao ambao hawana access na internet ambao wangeweza kufikiwa na kijalida kama cha cheche, kwa nini usianzishe tena na watu wakalipia kwa subscriptions? siku hizi kuna ZAP, M-Pesa, etc ambazo zinaweza kutumuka kama modes of payment na nina imani kuna watu ambao wangeweza kufanya hivyo mimi nikiwa mmoja wapo, ila mradi procedure ya kulipa iwe rahisi.

Naomba kuwasilisha mkuu.
 
Back
Top Bottom