Ili kupata uzoefu zaidi Ridhiwani apewe nafasi gani serikalini?

Wewe huna kazi ya kufanya na umeishiwa mawazo/fikra,umeamua kupoteza mda wako apa ili uonekane nawe umepost...kama huna la kuongea kaa kimya,ni busara pia..thread yako ni uchochezi usio na maana.
 
Mzee Mwanakijiji, kumbe siku ukikosa cha kuandika, huwa unaanzisha uchokozi?.

Kuna siasa za kujifunza na siasa za kuzaliwa, yaani kwenye damu ya kisiasa, hivyo kama siasa iko kwenye damu, atakuwa tuu bila kujifunza popote.

Kwani hawa wafuatao walijifunza wapi?.
  1. Laurent Kabila na Joseph Kabila?.
  2. Abedi Karume na Amani Karume?, Ali Karume anafuata!.
  3. Ali Hassan Mwinyi na Hussein Mwinyi?
  4. Jomo Kenyetta na Uhuru Kenyatta?.
  5. George Bush Sn na George Bush Jnr?
  6. Fidel Castro na Raul Castro?.
  7. Fredinand Marcos na Imelda Marcos?.
  8. Great Leader, Kim Il Sung na Dear Leader, Kim Jong Hill?.
  9. Marekani ukoo wa Kennedy
  10. India ukoo wa Indira Gadhi, kuanzia kwa Mahatma akaja Indira, akaja Sunjay hatimaye Sonia na wote wameondokea mlango ule ule!.
na wengine wote waliofuatiwa na watoto wao, walihitaji uzoefu gani?.

JF tupunguze uchokozi wa kuisakama first family!.
Pasco
Mbona hujawataja Uday and Qusay Hussein watoto wa Saddam...huwa unajipendekeza mno hadi too much mbona wengine tunakula nao tuu hatufanyi kama unavyofanya wewe?
 
huyu bwana hadi sasa anafanya kazi za waziri mkuu, kazi za waziri wa fedha, kazi za waziri wa nishati na madini, kazi za waziri wa sheria na katiba, kazi na IGP mwema, kazi za mwenyekiti wa chama chake, nafikiri hata kazi ya uspika pia anafanya, tayari ana uzoefu, hahitaji uzoefu zaidi ya huo wa hizo kazi anazofanya hapa,
 
Ridhiwani ukiwa kijana wa kitanzania Msomi wa LLB-UDSM tunajitokeza kukuombea uteuzi wa ujumbe wa LOAN BOARD (HESLB) ili usaidie nyongeza ya bajeti ya mikopo na pia uwe kiongozi wa presidential Guard maana sisi wahitimu wenzio UDSM tunaamini unaweza kuisaidia nchi kwa kuwa hupendi kujikweza na uko kawaida sana tangu ukiwa UDSM, na uteuzi huu utakupa uzoefu wa kazi muhimu kitaifa na UTAACHANA NA BIASHARA UCHWARA ZA BARABARANI na kuanza kujenga heshima yako kwa sasa na baadae.
 
sisi wote hapa JF tuna akili sio peke yako una agenda umeificha halafu hautaki kuwa muwazi hovyooooooooooooooooooooo na wewe siku hizi unatumika kuibomoa JF

Tutamfanya kama watoto wa Gaddafi, mwambie aendelee kuchekelea tuu.
 
Ridhiwani ukiwa kijana wa kitanzania Msomi wa LLB-UDSM tunajitokeza kukuombea uteuzi wa ujumbe wa LOAN BOARD (HESLB) ili usaidie nyongeza ya bajeti ya mikopo na pia uwe kiongozi wa presidential Guard maana sisi wahitimu wenzio UDSM tunaamini unaweza kuisaidia nchi kwa kuwa hupendi kujikweza na uko kawaida sana tangu ukiwa UDSM, na uteuzi huu utakupa uzoefu wa kazi muhimu kitaifa na UTAACHANA NA BIASHARA UCHWARA ZA BARABARANI na kuanza kujenga heshima yako kwa sasa na baadae.
personally napendekeza 2015 agombee ubungo kwa tiketi ya CCM ili ajionee vijana tunavyompenda tutampa kura za ushindi wa kishindo
RZ 1 ni mchapa kazi, ni mjasiriamali na mtu mwenye mwenye mvuto sana kwa vijana hasa wa vyuo vikuu
 
Ninyi hamjamuelewa Mzee Mwanakijiji, anapenda kutoa mada za kuchokoza chokochoko katika mawazo yetu japo hata yeye moyoni mwake ajua kabisa Ridhiwani ana safari ndefu ya kukua fikra za kutawala na MM pia ajua nchi hii si ya Kifalme! Tumekusoma mkuu
 
Bora miraji kikwete ana akili na hawezi kutumia wadhifa wa baba yake kujikweza,riz1 ni mtu anaye jikweza saaaaaaan as if hajui kuwa 2015 watatoka ikulu,hivi mbona wakati mwinyi ni rais watoto wake wa;litulia na wameanza siasa juzi tuuuu,huyu riz 1 ana matatizo gani ya akili?ana tofauti gani na waliopita?????asidhani hii ni nchi ya kifalme,ipo siku atajuta baba yake kuwa rais.
 
Nimejaribu kumwelewa MM , ni kwamba amechoshwa na hili jina kila leo riz1 riz 1 na akiangalia haelewi kama wengi tusivyoelewa, nimewahi kuona kwenye T.V mke wa rais salma akipokewa na mkuu wa mkoa wa lindi nilipata shida sana kuelewa huyu ni nani? Mpaka apokewe na mkuu wa mkoa panoja na RPC na kama haitoshi mkuu wa mkoa akamsomea risara inayoelezea maendeleo ya mkoa wa lindi.

Juzi tumesikia huko arusha kwamba riz 1 kapiga simu akitaka vijana wenzake wa ccm wakamatwe au wasipewe kibari cha kufungua matawi. sasa sijua anafanya hayo kama nani? na hiyo simu kampigia kiongozi wa ngazi ya juu wa polisi, sasa naungana na mm ni bora akapewa cheo ili tujue moja, hata akiongea tusishangae.

Nchi hii imekuwa na marais watatu na hatukupata kusikia upuuzi kama huu kila siku mtoto wa rais mtoto wa rais tumechoka , kila sehemu yupo kwenye biashara ya mafuta , usafilishaji, siasa kote riz1, riz1 too much.
 
Riz 1,Haya ya Mzee Mwanakijiji, ni kukuamsha wewe na Mzazi wako kuamka na kujitazama upya ili kuweka mambo sawa.Ametumia thread hii kuamsha hisia ambazo Mzazi wako akisoma thread hii anawea kuhamaki na kuona kama Mzee Mwanakijiji kamdhihaki lakini kumbe ni sauti ya kuwaamsha kujiangalia vyema na kutengeneza upya picha [image] ya utawala wa baba yako kwa Taifa kuwa kuna Mtawala Baba na kuna Mtawala Mtoto.

Najua mzazi anaweza asione tofauti za matendo ya mwanae kwa jamii,kwa kuwa hili liko dhahiri kwa mzazi ambae anaweza kutokutofautisha hisia za wengine kuhusu mtoto wake.Kwa kuwa wazazi baadhi uamini kuwajua watoto wao zaidi kuliko watu walio nje ya familia husika.

Na kwa kuwa ulikuwa pembeni kumsaidia baba katika kujipanga lakini kwa ushauri wangu ilikuwa sahihi hata kama ingekuwa ni mimi kwa gharama yoyote ile ningefanya hivyo kwa kuwa mzazi ni Mungu wa Pili hapa Duniani.Tofauti yangu mimi na wewe, mimi ningefanya kwa kificho [Indirect] na bado ukawa na nguvu tena kubwa sana kwa kuwa ungekuwa [Invisible] na ungepata nafasi nzuri sana ya kuwajua mahasimu na wenye nia mbaya na utwala wa baba yako pasipo wao kukujua wewe.

Matokeo yake wewe umeenda mstari wa mbele [Front] umegeuka kuwa ngao badala ya kuwa mkuki wa kuchoma ukitokea nyuma ya ngao.Kuna kitabu kinaitwa One Minute Manager naomba ukipitie uenda kingekusaida kukuondolea hiyo tabia ya kutaka kufanya kila jambo wewe.

Riz 1, mambo huwa yanabadilika na chuki uwa inapandikizwa hata wakati mwingine mtu anaweza kuhujumiwa kisha lawama ikamwagwa kwako kwa kuwa wewe ni ngao [Visible] hivyo watu wakakutumia wewe kama escaping got na hivyo wakialibu wao wanajua nani atatwishwa zigo hilo na wao wanakaa pembeni wakiwa safi [clean] pasipo lawama wala bila chuki toka kwa mtu waliemsurubu kwa gharama ya jina la RIz1.Na ndio maana dogo moja msanii kwa kujua uko karibu na msure wako na si wengine labda kakutuma umwambie baba yako uku mtaani soooo.

Kama Baba yako alikuwa na dhamira nzuri ya kukujenga [Like Father like Son] style hiyo kwa karne ya sasa kwa upande wa siasa, ambayo dunia iko na inako elekea kamwe haina nafasi.Ila angekuweka pembeni ukawa Invisible not in Political only atmosphere, even in economical ground, with a low profile records, but strong in connecetion of which matter mostly.

Wewe umetambaa sehemu zote hizo hivyo maadui wa baba pia wamegeuka kuwa maadui wa mtoto na maadui wa mtoto wamegeuka kuwa wa baba basi shida kila kukicha.Wazee hawa wanapokuwa kwenye shughuri zao, wanaheshimika kwa kuwa yuko kwenye kiti hicho,lakini pindi wakitoka hakika mambo ugeuka. Chukulia baba yako alipolazimishwa kuachia baadhi ya wakuu waliopita kwenye madaraka washughulikiwe, na sheria ichukue mkondo wake, kwa kujua hilo baba yako aligoma kwa kuwaambia watanzania wamuache Mzee huyo apumzike.Hivyo basi walee watanzania hawajahama wala kuaacha Nchi ila Mzazi wako kalundika Mzigo ambao pia unaweza kuibuka wakati wowote. Hivyo kukuweka wewe mbele katika siasa za kitanzania,ni kujitia kitanzi yeye binafsi,inajulikana kuwa yeye katumika pia kuwalea baadhi ya watoto wa wazee wengine,basi angewafumba macho Watanzania kwa kukuweka wewe pembeni kisha kwa namna nyingine mtu mwingine ndie angekuja kukuweka wewe kwenye siasa zetu za kibongo.

Kwa sasa wahindi, waarabu na wamatumbi wakikuona wewe na kwa kuwa wanajua wakimuona Mtoto wamemuona Baba,basi wanapitisha hoja zao,ukizingatia na wewe na ujana ndani yake kurubuniwa ni rahisi sana,kupambana na magwiji wa hadaa za ulaghai kuwin ushawishi wa kuambatana na wewe kuwafanikishia access ya kuwa karibu na wao kutumia ukaribu huo kujijenga kiuchumi na kisiasa kwa niaba ya mgongo wa Baba yako,ambao wakati mwingine mengine yanafanyika pasipo ufahanu wa baba yako wala wewe mwenyewe,ila kwa kuwa wanaambatana na wewe basi balaa tupu.

Anyway unaweza kuwa Invisible, muda unaruhusu miaka mitatu ni mingi sana watanzania kukusahau kwenye siasa zao,ukawa undercover wa maendeleo ya baba yako lakini sio,mara uko yanga,mara ccm nini, mara ugomvi na fulani kisiasa,mara zimepanda zikashuka, acha kazi hizo zifanywe na watu wengine, ambao kupitia kazi hizo wanamaslahi yao kwa baba yako na ni wadau wake. [One Minute Manager] uwezi fanya yote.

Vinginevyo hivyo vyeo vilivyosemwa na Mzee mwanakijiji ndugu yangu watu watahesabu kuwa unavyo hasa hicho cha Msaidizi Maalum (without portfolio) au Msaidizi Ofisi ya Katibu Kiongozi - Special Duties.

Najua umezungukwa na wapambe kijana kwa umri wako pole wewe ni mdogo sana wanakulisha uchafu mwingi sana,wanajua wanakutumia kwa faida zao.



 
nikimtazama RIDHIWAN namuona Kikwete Mkweree... mwingine, na kwakua mara kwa mara kijana amekua akirudia kuwa babake ndie role model wake, hii inatoa ishara kuwa hana jipya maana kama failures huyu Bwana Kikwete anaweza kuwa shujaa wako ujue wewe unakasoro katika muundo wa kufikiri.
Ridhiwani ni nyoka mwingine ambae tukimchekea atarejesha mazongezonge ya baba yake hapa Tanzania.
Bado nalaumu sana mtu aliemshauri Kikwete kuwa mwanasiasa, huyu mtu katuletea Tanzania Mateso makubwa.
 
nikimtazama RIDHIWAN namuona Kikwete Mkweree... mwingine, na kwakua mara kwa mara kijana amekua akirudia kuwa babake ndie role model wake, hii inatoa ishara kuwa hana jipya maana kama failures huyu Bwana Kikwete anaweza kuwa shujaa wako ujue wewe unakasoro katika muundo wa kufikiri.
Ridhiwani ni nyoka mwingine ambae tukimchekea atarejesha mazongezonge ya baba yake hapa Tanzania.
Bado nalaumu sana mtu aliemshauri Kikwete kuwa mwanasiasa, huyu mtu katuletea Tanzania Mateso makubwa.

babake kikwete alikuwa mwenyekiti wa TANU/CCM na mkuu wa wilaya enzi hizo, nafikiri ndiye alifanya raisi wetu pia kuwa mwanasiasa.
 
wengi wananona kama mwanakijiji kapotoka tusipotumia box la kura kuitoa ccm tutakuja kushangaa dogo yuko kwenye cheo kikubwa siku moja..
 
Mzee mwanakijiji nakuheshim sana, najua mara zote huwa unaandika mambo ya maana iweje leo uje na story hii, then tueleze kwanza umefikiri nini mpaka kuandika hivyo, au unatetesi zozote kuhusu huyo fisadi?
 
Back
Top Bottom