sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,408
- 19,033
Ni wazi kabisa bila kupepesa macho lengo kuu la wazazi wa Tanzania ni kusomesha mtoto ili aje kupata ajira serikalini.
Ajira zinazidi kuwa adimu sana, wanafunzi wengi wanahitimu vyuo na vyuo vipo vingi sio kama zamani, wahitimu wamekuwa wengi sana lakini ajira haziongezeki.
Wanaoajiriwa ni wachache sana, wanaobaki mitaani baada ya kuona hakuna matumani ya ajira mwisho wa siku wanakubaliana na matokeo na wengi wao huishia kujiajiri ama wafanye biashara, wengi huanza kufanya shughuli hizi bila uzoefu kwasababu walitumia muda mwingi shuleni, matokeo yake ugeni wao unaweza kuchangia shughuli zao ziwe na changamoto na hata kufilisika kwa kukosa uzoefu.
Wengine wana degree zao wanaamua kufanya kazi za elf 80 kwasababu hawajui kitu kingine zaidi ya elimu ya darasani, hawana skills zozote walizowahi kujifunza nje ya darasa na hawana uzoefu wowote wa kufanya biashqra, hapa ndio wengi hudhalilika "fulani ana degree lakini anafanya kazi ya laki 1"
Nitoe rai kwa wazazi wenye biashara ama waliojoajiri kwa skills wawe bega kwa bega na watoto wao waweze kuwamegea uzoefu wao kwenye shughuli zao, mfundishe mtoto kusimamia biashara, mfundishe kodi zinalipwa wakati gani, supplier yupo wapi, jinsi ya kufungua biashara, jinsi ya kukwepa changamoto za ugeni wa biashara, n.k. itamsaidia sana kwasababu wewe mzazi ulishapitia changamoto kibao unamtafunia asizirudie, hapo mbele akikosa ajira aweze kufanya biashara.
Wale ambao, Lipia mtoto wako apprenticeship, Tafuta watu walau wa karibu unaowaamini wanaoendesha maisha yao kwa kuwa wakulima, wafugaji, vinyozi, wapishi, seremala, n.k. uwe unawalipa wamfundishe kazi mtoto. yani kila likizo awe anatumia muda wake huko kujinoa zaidi, azijue abcd za kuingiza hela, hata akimaliza chuo ukimpa mtaji anafungua ofisi yake huku anajua anachofanya na jinsi ya kukabiliana nachangamoto sio kuanza upya.