Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,494
- 113,589
Mzee Mwanakijiji, kumbe siku ukikosa cha kuandika, huwa unaanzisha uchokozi?.Tayari ni kijana ambaye anapata uzoefu mbalimbali wa shughuli za kichama na siasa. Naamini kwa ajili ya kuweza kuja kugombea baadaye nafasi "kubwa" nchini anahitaji kupata uzoefu wa mambo ya serikali. Najiuliza ni nafasi gani zinamfaa ili Rais amteua au (chombo kingine cha uteuzi) ili kumpatia Ridhiwani uzoefu wa mambo ya serikali. Nafikiria kama nafasi zifuatazo:
a. Msaidizi wa Rais Ushauri wa Usalama wa Taifa
b. Mshauri wa Rais (Siasa na Vyama vya siasa)- nafasi iliyowahi kushikiliwa na Kingunge
c. Msaidizi Maalum (without portfolio)
d. Mshauri wa Kisheria - Presidential Guards
e. Msaidizi Ofisi ya Katibu Kiongozi - Special Duties
f. Kwenda Monduli Military Academy na kufanya mafunzo ya Ofisa wa JWTZ - hili nalipenda zaidi kwani akitoka anaweza kupewa Brigage au Kikosi chake Maalum kukiongoza..
Au cheo chochote kile labda wengine mnaweza kuwa na mawazo zaidi. Hii itamsaidia Ridhiwani kupata mwanga zaidi wa shughuli za serikali na kuweza kupanua zaidi wigo wa maono yake kuhusu kutawala nchi yetu. Lakini itamsaidia siku moja kama atataka kugombea Ubunge au nafasi nyingine ya juu kuweza kuwa amepata kuwa na uzoefu wa aina mbalimbali.
Kuna siasa za kujifunza na siasa za kuzaliwa, yaani kwenye damu ya kisiasa, hivyo kama siasa iko kwenye damu, atakuwa tuu bila kujifunza popote.
Kwani hawa wafuatao walijifunza wapi?.
- Laurent Kabila na Joseph Kabila?.
- Abedi Karume na Amani Karume?, Ali Karume anafuata!.
- Ali Hassan Mwinyi na Hussein Mwinyi?
- Jomo Kenyetta na Uhuru Kenyatta?.
- George Bush Sn na George Bush Jnr?
- Fidel Castro na Raul Castro?.
- Fredinand Marcos na Imelda Marcos?.
- Great Leader, Kim Il Sung na Dear Leader, Kim Jong Hill?.
- Marekani ukoo wa Kennedy
- India ukoo wa Indira Gadhi, kuanzia kwa Mahatma akaja Indira, akaja Sunjay hatimaye Sonia na wote wameondokea mlango ule ule!.
JF tupunguze uchokozi wa kuisakama first family!.