Hukumu ya ICC yamtaja Rostam Aziz mmiliki wa Dowans!

Mimi sijamuona, jee, wewe umemuona? Or just circumstantial? Mie naona kama katajwa Mbowe!

Hivi kama nikikutukana ******** nitakuwa nimefanya kosa ndani ya X-Mas hii? wewe siku zote unaniudhi sana na maandishi yako yananipa mood mbaya mara zote
 
Mimi naona suala hili limechukua muda mrefu kulitatua kutokana na kusitasita kwa Serikali kwa sababu zisizoeleweka. Hakuna ubishi kwamba Richmond ilitutapeli kwa kuleta mitambo isiyokidhi viwango tilivyolipia. Kampuni yenyewe ime-prove ni feki huko Merikani.

Pili, Dowans imethibitishwa na Mwarabu (Mwana Mfalme = Prince) aliyetajwa kuwa ndiye mwenye hisa kwamba ni feki. Hata huko Costa Rica kunakodaiwa mmiliki mwingine yupo, Serikali ya nchi hiyo imethibitisha taarifa hiyo ni ya uongo. Kwa hiyo hii Dowans ni feki pia.

Kwa hiyo bila hata kuwahusisha hawa vigogo Wabunge na Wanasheria wa hapa kwetu, wanaotajwa na Kubenea na Samwel Sitta, napendekeza Serikali ichukue hatua ya kutaifisha hii kampuni ya Dowans kwa kupitisha Sheria Bungeni kwa tukitumia nguvu yetu ya Sovereignty. Tutamke katika hiyo sheria kwamba hatutalipa fidia kwa atayejitokeza kwamba ni mmiliki wa Dowans. Sababu ya kutolipa fidia ni kwamba TANESCO wameshawalipa vya kutosha hawa mafisadi.

Serikali ya mafisadi ya CCM itaitaifishaje DOWANS wakati serikali hiyo hiyo imetekwa nyara na hao wamiliki wa DOWANS. Chini ya CCM lazima DOWANS italipwa, tena kwa furaha kubwa. Kuilipa DOWANS ni sawa na kujilipa wenyewe CCM kwa kuwaibia walalahoi.

Kama tumeshindwa kwa sasa kutumia njia ya kistaarabu na ya polepole ya kuwaondoa wafisadi wa CCM kupitia sanduku la kura, njia mbadala na ya haraka ya kutatua tatizo la DOWANS wala haihitaji longo longo nyingi. Wamiliki wa DOWANS kila mtu anawajua, ni watu wachache sana kiasi kwamba umma kuwachukulia hatua ni kitu rahisi tu. CCM wanachofanya ni kuwa ni wao tu ndio wanajua, sisi wengine wote hamnazo.

Kama DOWANS ingeondoa ama kupunguza mateso kwa walalahoi, hakuna ambaye angeichukia hata kama ni mali ya nani.
 
Kuogopa mtu mweupe mwenye Fedha si sawa kabisa na kutokuwa Huru??
Hivi ni Rostam Aziz anayetishia watu au Ni Usalama wa Taifa?? I mean Usalam wa CCM??
 
Tusipobadilisha katiba tutaendelea kuzalisha wamiliki wa Dowans and the like kwa muda mrefu. Kwa katiba hii itakukuwa ngumu kupambana na makundu ya wanyang'anyi kama hawa. Mfano ni kama huu, wawakilishi wetu(TANESCO) kwenye kesi wanashindwa kutueleza tumehamuliwa kumlipa nani.Tuungane kwa hali na mali kudai katiba mpya mapema sana kabla muda wa kuidai kwa maelewano haujaisha kwani tukianza kuidai kutokea misitu ya Kongo n.k itakuwa ni hatari sana.
 
Mkuu yaani umeamua kutuwekea hukumu ya akina Kony...

Umeona nimeisoma nikasema labda pengine nina makengeza but nashukuru na wewe umeliona hilo pengine amechanganya mafile tumsubirie atubandikie hii saga naifatilia nijue ukweli bilioni 180 nyingi tunataka kujua ni akina nani wamiliki wa Dowans!!!!
 
Duuh, kwani Mbunge na business tycoon gani anayehusishwa na Richmond/Dowans siku zote hizo ni nani kama si Rostam Aziz? Soma ripoti ya kamati ya Mwakyembe. Mtu aliyekuwa anaiwakilisha Dowans kwenye kesi ya ICC ni mfanyakazi wa CASPIAN Construction inayomilikiwa na Rostam. Alipobanwa na majaji aseme nani mmiliki wa Dowans jamaa akamtaja Rostam. Hii iko kwenye ruling ya ICC. Eti TANESCO ambao ndiyo wahusika wakuu wa kesi hii hawana nakala kamili ya uamuzi wa ICC.

Hapo kwenye red; Unaamini?
 
MwanaJF anayefahamu anwani au e-mail ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda ampelekee hiyo Thread ya Mzee Edwin Mtei. Kwa vyovyote Dowans ni lazima itaifishwe Bunge letu litakapo kuwa na kikao Februari 2011. Na Wasilipwe compensation yoyote.
 
MwanaJF anayefahamu anwani au e-mail ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda ampelekee hiyo Thread ya Mzee Edwin Mtei. Kwa vyovyote Dowans ni lazima itaifishwe Bunge letu litakapo kuwa na kikao Februari 2011. Na Wasilipwe compensation yoyote.
Utamsumbua tu Pinda alishasema ni bora kumtoa roho kuliko kuzungumzia vitu kama hivyo, yeye hana habari anajiandaa kwenda shambani.

12_10_6jywre.jpg
 
Umeona nimeisoma nikasema labda pengine nina makengeza but nashukuru na wewe umeliona hilo pengine amechanganya mafile tumsubirie atubandikie hii saga naifatilia nijue ukweli bilioni 180 nyingi tunataka kujua ni akina nani wamiliki wa Dowans!!!!
hivi siyo bil 185
 
please jamani watanzania tuache tabia zakutofuatili mambo kwa usahihi wake,huyu mwandishi anatakiwa kutaja kile hukumu inachozungumza na nani anatajwa katika hukumu hiyo,sio swala la kutuambia mbunge,tuna wabunge wengi sio lazima awe rostam.riport ya richimond inasema mmiliki wa kampuni hizi hajulikani ni kampuni za kitapeli,hivi mpaka kampuni inashinda kesi mahakamani bado mmiliki wake ni jambo la kuendelea kuhisi?tuache tabia za uzandiki wa kutumiwa vibaya na wanasiasa mfilisi.nyie waandishi wa habari andikeni vitu kamili na sahihi,sio kutaka kuuza magazeti yenu tu,nasi jf hoja zisizo na kichwa wala miguu hatuna sababu ya kuzizarau na kuwambia wawasilishaji wale fulldata za habari zao.​
Mbona unajaa upepo Christopher ,kinachotajwa kwenye hukumu nikipi kumbe unakijua ,mbona unaguswa sana na kutajwa kwa RA vipi ni mbia wako wenye kuelewa tumeelewa wewe kama hutaki kuelewa kajinyonge
 
Hii inanikumbusha wimbo wa dogo mmoja alikuwa akiimba Tanzania eeeeeeeeeeeeee nchi yangu eeeeeeeeeeeeee .....
Ama kweli tulipofika Tz sasa ni kichwa cha mwendawazimu kama mmiliki wa dowans hajulikani tutailipa hewa!
Kama RA yuko kwa harakati za kuchakachua hukumu hakuna anaeweza pata original copy?
 
Mijitu mingine haina haya kweli kweli, utadhani huyo RA katajwa kweli kumbe ni hallucination!



Njaa na akili haviendi pamoja hata siku moja,pamoja kwamba kwenye msafala wa mamba na kenge wamo, lakini cha kusikitisha wewe hata kwenye hilo kundi la kenge huna nafasi, badala yake unaangukia kwenye kundi la mijusi. Shame on you.
 
Back
Top Bottom