Kwanini usubiri maamuzi ya anayesubiri kupigiwa simu, badala ya kusikiliza maamuzi ya anayepiga Simu?

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,547
41,057
Tatizo kubwa la nchi za Afrika, na hasa Tanzania, ni mifumo mibaya kabisa ya kiutawala. Mifumo ambayo imekaa kinadharia na wala haifanyi kazi. Ni kama tunataka tu tuonekane mbele ya uso wa mataifa kuwa na sisi tumestaarabika.

Kuna wakati nilikuwa Sao Paulo. Rafiki yangu mmoja aliniambia kuwa kuna wakati kuna mitaa Sao Paulo ilikuwa na vibaka wengi, hasa wa kuiba vitu ukiviacha ndani ya gari. Ili kuondokana na tatizo hilo, kampuni ilikuwa inawafundisha mbwa namna ya kukaa kwenye kiti cha dereva kwenye gari. Mbwa anakaa pale kwenye kiti cha dereva ili kibaka akipita aone ndani ya gari kuna dereva. Lakini ukwwlei ni mbwa kakaa;ukimwambia aendeshe gari, hajua, wala hajui aende wapi, na aende akafanye nini. Anachojua ni kukaa kwenye kiti cha dereva.

Ukiyatazama mataifa ya Afrika, na hasa Tanzania, ni kama tumeambiwa nchi ili iwe na utawala bora inatakiwa iwe na mihimili mitatu, Serikali, Bunge na Mahakama. Lakini kiuhalisia ni kama mbwa aliyekalishwa kwenye kiti cha dereva ili walio nje waone ndani ya gari kuna dereva, lakini hatujui maana ya mihimili mitatu, hatujui inavyotakiwa kufanya kazi, hatujui mipaka yake, wala hatujui mamlaka na nguvu ya kila muhimili.

Kukosa kuyajua hayo yote, ndiyo maana kuna wakati mliwahi kusikia:

1) Jaji mkuu akiwaambia majaji kuwa hukumu zao ni lazima zizingatie Serikali inataka nini. Huyo ni Jaji Mkuu! Kama Jaji mkuu yupo hivyo, na ana fikra kama hizo, fikiria hao majaji na mahakimu watakuwaje!!

2) Spika wa Bunge aliwahi kutamka kuwa Bunge lipo chini ya Rais. Lazima wabunge wazingatie hilo. Wabunge walikaa kimya na wengine wakagonga meza kwa furaha. Huyo ndiye spika. Sasa fikiria hao wanaoitwa wabunge, watakuwa ni watu wa vichwa vya namna gani!!

3) Rais aliwahi kutamka kuwa japo kuna mihimili mitatu, lakini wa kwake imejichimbia zaidi. Na waliomzunguka wakatikisa vichwa kuashiria kukubali.

4) Rais aliwahi kumwambia Spika, ukiona kuna wabunge wanakusumbua, wewe wafukuze huko ndani, halafu wakija huku nje, mimi nashughulika nao. Na spika akainamisha kichwa kuashiria kukubali.

5) Rais aliwahi kutamka kuwa katiba ni kijitabu tu. Waliomzunguka wakatikisa vichwa kuashiria kukubali. Lakini huyo ni mtu aliyeapa kuilinda na kuiheshimu katiba!

6) Aliyewahi kuwa mwekahazina mkuu wa CCM, mbunge kupitia CCM, na mjumbs wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, yeye alikuwa mkweli wa nafsi, akanena kwa ujasiri, kuwa majaji wa Tanzania, kabla ya kutoa hukumu huwa wanasubiri kupewa maelekezo na Serikali watoe hukumu ya namna gani, hasa kama katika jambo hilo, ikulu au Serikali ina maslahi nalo. Kwa maneno yake alisema kuwa hakuna mwekezaji makini anaweza kuja kuwekeza Tanzania, nchi ambayo majaji wanasubiri kupigiwa simu kabla ya kutoa hukumu. Hongera sana Rostam Aziz, kwa ukweli na ujasiri maana ndiyo ukweli ambao kila mwenye akili anaujua, lakini ni wachache wenye ujasiri wa kuunena.

Ukweli huo ndio uliowafanya viongozi na wapenzi wengi wa CHADEMA kukamatwa na kushtakiwa kwa mashtaka hewa na kisha kuhukumiwa na majaji wa kuelekezwa wakati wa uongozi wa Magufuli. Alivyokuja Rais Samia, majaji wa kuelekezwa, wakawaachia wale wale waliowafunga.

Yote yanaashiria sisi hatujastaarabika kiasi cha kuwa na mifumo ya utawala bora.

Kama kuna kesi yoyote inayogusa matakwa ya ikulu au Serikali kwa ujumla, hivi kuna sababu gani ukapoteze muda kwenye mahakama za Tanzania, ukasubirie hukumu kutoka kwa mtu anayesubiri kuelekezwa? Si afadhali uende huko ikulu au kwa mkuu wa Serikali, umwulize tu kuwa kwenye hili umeamua nini?

Ikulu iliishaamua kuwa Mdee na wenzake ni wabunge mpaka bunge hili bandia limalize muda wake. Kwanza hata hao wabunge wa CCM waliopo huko karibia wote ni bandia, hivyo kuwaondoa hawa bandia kutoka CHADEMA ni kuwaonea.

Jambo la muhimu, ni kujiuliza, ni lini tunataka tuwe na nchi kamili, mihimili ya utawala kamili, viongozi na watendaji kamili.
 
"Kuna Karne itafika kwa wajinga kuwa viongozi na werevu kuwa wafuasi nadhani Karne yenyewe ndo hii"Shaaban Robert.

"Wenye akili timamu wasipo jishughulisha na mambo yanayo husu taifa lao mwisho hutawaliwa na wajinga"Plato

Tanzania hakuna mahakama,bali majengo yenye nembo na jina mahakama,ndio maana Kuna jaji,aliwahi sema kuna waziri aliwahi kuchana karatasi ya hukumu yake.Kitendo hiki kinaashiria dharau juu ya mahakama na majaji,kwa maana kwamba watawala wanajua akili za majaji ndio maana wanaweza kufanya lolote na hakuna wa kuwakemea.

Nchi inapoteza pesa nyingi za walipa Kodi kwa kuhudumia majitu mapumbavu,yenye vyeo kwa mujibu wa katiba.

Huwezi pata halali toka kwa kharamu,hata siku moja.
 
Na bado hamjasema, moja Kati ya kanuni muhimu kwa mahakama ni security of tenure. Jaji mkuu anaishi kwa mkataba maana alishastaafu, ili aendelee na mkataba lazima afanye jambo jema kwa executive, na hatumtoi mpaka amuapishe samia na amalize kesi zote za uchaguzi wa 2025
 
Uko sahihi mkuu, na ndio maana serekali hii hufananishwa na mtu aliyejifunika barafu.. Wakati jua kali.
 
Na bado hamjasema, moja Kati ya kanuni muhimu kwa mahakama ni security of tenure. Jaji mkuu anaishi kwa mkataba maana alishastaafu, ili aendelee na mkataba lazima afanye jambo jema kwa executive, na hatumtoi mpaka amuapishe samia na amalize kesi zote za uchaguzi wa 2025
Bila machafuko ama mapinduzi ya kijeshi mtaendelea kuchezea mifumo ya utawala mtakavyo, hakuna tatizo tunatunza rekodi, ili siku ya mahesabu tusipoteane. Tambeni sana lakini mwisho unakaribia. Dhalimu magu aliamini Yuko juu ya Kila kitu, ila alichokutana nacho haamini Hadi Leo.
 
Back
Top Bottom