Huenda Makonda na makada wa CCM wakachochea mabadiliko katika mhimili wa mahakama

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,620
46,261
Kumekuwepo na mfululizo wa watu ambao ni makada wa CCM kuikosoa mahakama ambao unapaswa kuwa mhimili wa kutoa haki katika nchi za kidemokrasia.

Kauli ya hivi karibuni ya Makonda kuhusu utendaji wa chombo hichi ni muendelezo wa Wana CCM wenye majina makubwa kuupopoa mhimili huo. Wengine ni kama Rostam Aziz na Fatma Karume.

Rostam yeye alisema simu moja kwa majaji tu Kisutu inaweza kubadilisha hukumu ndio maana watu wanaofanya uwekezaji mkubwa wanataka kesi zao ziamuliwe nje ya nchi.

Fatma Karume kwa muda mrefu amekuwa akikosoa vikali utendaji wa mhimili huu. Ikiwemo pamoja na ucheleweshwaji wa kesi na hukumu na jinsi majaji wanavyosikiliza kesi moja kwa vipande vipande kwa muda mrefu sana kiasi kutia wasiwasi uthabiti wa kumbukumbu zao wanapotoa hukumu.
 
Hata Rais naye alisema majuzi tu hapa kuwa mahakama zetu zina shida, tafsiri yake ni kwamba walichosema Makonda, Fatma na Rostam ni kweli
 
Tangu Jaji Mkuu ajiingize kwenye majibizano kuhusu uchunguzi wa kesi ya Lissu, na kuanza kuponda wanaodai uchunguzi wa kwenye shambilio la Lissu, nikamuona hayupo impartial. Jaji Kaa mahakamani subiria kesi sio kuanza kuingilia mambo ya uchunguzi
 
Back
Top Bottom